Akiwa anahojiwa kutoka katika televisheni ya Wasafi (Wasafi TV) Waziri Nape amesema kuwa serikali haina matatizo na Starlink, kinachofanya washindwe kutoa huduma zao nchini ni sababu hawajakamilisha masharti, na kama wakikamilisha basi wataruhusiwa kutoa huduma nchini.
Msikilize hapa
====
"Nimezungumza hapa, kama nchi tunamchakato wa kuwa na Satelite ambao tutaukamilisha mapema tu, iwe ni alternative yah hizi cable. The best ni cables lakini satellite ni njia mojawapo, na Starlink ni kama watoa huduma wengine ambao wanaleta huduma za mawasiliano walikuja wakaomba leseni.
"Sasa mfumo wetu wa lesseni unaoingia kwenye mtandao kidijitali unajaza taarifa mbalimbali, sasa baadhi ya nyaraka walikuwa hawana, kwahiyo walipoenda wakafika mahali wakagota na nyaraka zile hawana, sisi tuliwaambia kamilisheni. Wakikamilisha maombi yao na yakaletwa mezani kwangu siku hiyo hiyo nasaini, hatuna matatizo nao.
"Nasikia watu wanasema wamezuiwa, hatujazuia mtu. Tumewaambia kamilisheni utaratibu. Hatuwezi kubadilisha taratibu tulizoziweka ambazo watoa huduma wote wamezifuata kwasababu ya mtu mmoja ambaye hana cheti chake cha form four sijui cha wapi. Fuateni utaratibu tu na kila kitu kipo mtandaoni wala hauitaji kwenda kusoma. Kwahiyo wakikamilisha watakuja.
"Lakini hata baadhi ya nchi ambazo wanapata huduma hiyo ya Starlink na wenzake ni katika nchi zilizoathirika. Kwahiyo kwenda kudanganyana kwamba eti ndio suluhu la mwisho kabisa, tunadanganyana. Mimi najua katika nchi 11 karibia nchi 2..3 zinapata huduma na zimeathirika."
====
Wameweza kukamilisha documents kwa nchi nyingine halafu ndio washindwe kukamilisha kutoa documents Tanzania, nchi ndogo ambayo inajikongoja kwenye karibu kila kitu?
Nape tuambie ukweli, acha kuzunguka zunguka, ukiangalia uchaguzi mkuu upo puani na historia imetufundisha vyema vile mnatufanyia wananchi linapokuja suala la mtando.
Kwa ninavyoona Serikali itakuwa imetoa sharti kwa Starlink na Elon Musk kuzima mtandao kila serikali itakapotoa agizo hilo, na kwakuwa Elon ni champion wa uhuru wa kujieleza akawatolewa nje basi na nyie serikali mkashupaza shingo.
Inaonesha mwakani ngoma nzito kiasi kwamba mko tayari hata kuacha taifa liingie hasara ya mabilioni ya pesa sababu ya kukosekana kwa internet ili tu mjihakikishie kuendelea kubaki madarakani.
Wakuu, maonaje kuhusu hili? Sababu hii ina mashiko? Kama haina mashiko unafikiri ni sababu gani au document gani ambayo Sterlink wameshindwa kutimiza ili wapewe leseni ya kuhuduma ya mtandao nchini?
Msikilize hapa
====
"Nimezungumza hapa, kama nchi tunamchakato wa kuwa na Satelite ambao tutaukamilisha mapema tu, iwe ni alternative yah hizi cable. The best ni cables lakini satellite ni njia mojawapo, na Starlink ni kama watoa huduma wengine ambao wanaleta huduma za mawasiliano walikuja wakaomba leseni.
"Sasa mfumo wetu wa lesseni unaoingia kwenye mtandao kidijitali unajaza taarifa mbalimbali, sasa baadhi ya nyaraka walikuwa hawana, kwahiyo walipoenda wakafika mahali wakagota na nyaraka zile hawana, sisi tuliwaambia kamilisheni. Wakikamilisha maombi yao na yakaletwa mezani kwangu siku hiyo hiyo nasaini, hatuna matatizo nao.
"Nasikia watu wanasema wamezuiwa, hatujazuia mtu. Tumewaambia kamilisheni utaratibu. Hatuwezi kubadilisha taratibu tulizoziweka ambazo watoa huduma wote wamezifuata kwasababu ya mtu mmoja ambaye hana cheti chake cha form four sijui cha wapi. Fuateni utaratibu tu na kila kitu kipo mtandaoni wala hauitaji kwenda kusoma. Kwahiyo wakikamilisha watakuja.
"Lakini hata baadhi ya nchi ambazo wanapata huduma hiyo ya Starlink na wenzake ni katika nchi zilizoathirika. Kwahiyo kwenda kudanganyana kwamba eti ndio suluhu la mwisho kabisa, tunadanganyana. Mimi najua katika nchi 11 karibia nchi 2..3 zinapata huduma na zimeathirika."
====
Ni masharti gani hayo yanayosemwa kila mara kuwa Starlink hawajatimiza? Yaani Nape anataka kutuamisha kabisa kuwa Starlink wamekosa cheti cha kutoa hudumu nchini? Wameweza kukamilisha documents kwa nchi nyingine halafu ndio washindwe kukamilisha kutoa documents Tanzania, nchi ndogo ambayo inajikongoja kwenye karibu kila kitu?