Waziri Nape akimkaribisha Maharage Chande Wizarani "Mshale Umerudi Nyumbani"

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Mshale Umerudi Nyumbani,ndio maneno ya Nape akimkaribisha Maharage Chande Mkurugenzi wa TTCL.
---
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amekaribisha Mkurugenzi Mkuu mpya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Maharage Chande aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo hivi karibuni.

“Kipekee kabisa nikukaribishe ndugu yangu, kaka yangu, rafiki yangu, Maharage Chande. Karibu rasmi kwenye familia ya wanamawasiliano, najua umetokea huku, ni mshale umerudi nyumbani. Namshukuru Rais kwa uteuzi wako, karibu sana,” amesema.

Hayo yalisemwa leo Jumatatu Septemba 25, 2023 katika hafla ya utiaji saini hati ya maridhiano na hati ya mkataba wa nyongeza kwenye miundombinu ya mkongo wa mawasiliano kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na umoja wa watoa huduma za mawasiliano nchini.
---

Je ni kijembe au ni pongezi? Waswahili karibuni mdadavue.

Mwananchi
 
Maharage amesoma electronics science. Kule TANESCO hakuna alichokuwa anakijua. Walikuwa wanamdangamya kama mtoto mdogo. Sijui waliomteua walidhani electrical engineering na electronics science ni kitu kimoja??

Kwa kifupi huko walikompeleka ndio haswaa kwenye taaluma yake. Pia huyo waziri wake ni walewale kama mtoto wa Makamba. Kwahiyo dili zao zitakwenda vizuri kwenye kuimaliza TTCL kwa maslahi ya akina Voda na nduguze.
 
Nyani wamekutana kwenye shamba la ndizi? AU
Fisi wamekutana kwenye mzoga wa tembo?
Nacheka utafikiri mazuri,ila huyu jamaa wamempa mahali sahihi sana,ingawa hata kule alikotoka pia kuna vitu kafanya anastahili pongezi,ukiachilia hii si tofahamu ya kukatika umeme ambayo sidhani kama anahusika mojo kwa moja...
 
Ku mreplace Eng. Peter Ulanga na Maharage Chande ni kiashiria cha kutaka kuliua kabisa shirika la mawasiliano.

CV plus experience ya Peter Ulanga ukiilinganisha na ya Ndugu Maharage Chande ni Mbingu na ardhi. Mama aangalie vyema hapa
Peter Ulanga kapelekww wapi?
 
Nchi ya ajabu sana hii. Mtu katolewa kwa incompetence halafu anahamishiwa kwenye shirika jingine ambalo liko kwenye mchakato wa kubinafsishwa. Unaona hata wanavyochekeana, hakuna userious kabisa hapo. Zero. Ni kweli mshale umerudi nyumbani na pia nakubaliana kuwa wanatuona sisi ni kama nyani kabisa.
 
Tayari huku!
Screenshot_20230925_195240.jpg

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Nchi ya ajabu sana hii. Mtu katolewa kwa incompetence halafu anahamishiwa kwenye shirika jingine ambalo liko kwenye mchakato wa kubinafsishwa. Unaona hata wanavyochekeana, hakuna userious kabisa hapo. Zero. Ni kweli mshale umerudi nyumbani na pia nakubaliana kuwa wanatuona sisi ni kama nyani kabisa.
incompetence ipi?
 
Mshale Umerudi Nyumbani,ndio maneno ya Nape akimkaribisha Maharage Chande Mkurugenzi wa TTCL.
---
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amekaribisha Mkurugenzi Mkuu mpya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Maharage Chande aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo hivi karibuni.

“Kipekee kabisa nikukaribishe ndugu yangu, kaka yangu, rafiki yangu, Maharage Chande. Karibu rasmi kwenye familia ya wanamawasiliano, najua umetokea huku, ni mshale umerudi nyumbani. Namshukuru Rais kwa uteuzi wako, karibu sana,” amesema.

Hayo yalisemwa leo Jumatatu Septemba 25, 2023 katika hafla ya utiaji saini hati ya maridhiano na hati ya mkataba wa nyongeza kwenye miundombinu ya mkongo wa mawasiliano kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na umoja wa watoa huduma za mawasiliano nchini.
---

Je ni kijembe au ni pongezi? Waswahili karibuni mdadavue.

Mwananchi
Hajapoa kaopolewa tena
 
“Kipekee kabisa nikukaribishe ndugu yangu, kaka yangu, rafiki yangu, Maharage Chande. Karibu rasmi kwenye familia ya wanamawasiliano, najua umetokea huku, ni mshale umerudi nyumbani. Namshukuru Rais kwa uteuzi wako, karibu sana,”

Mshale umepelekwa posta...
 
Back
Top Bottom