Kwa wanaoifahamu vyema wizara ya madini na nishati na mfumo mzima wa hujuma ndani ya TANESCO wanaelewa Prof. anachosema. Ukweli ni kwamba wizara hiyo haijawahi kumpata mtu wa aina ya Prof. Muhongo ambaye kwa sasa anashambuliwa toka kila upande ili aachie ngazi, awaachie mafisadi mwanya wa kupumua. Alichojaribu kukifunuaa Prof. ni "Tip of an iceberg" pole pole ukweli utajifungua na mkweli kuthibitika, kama si kaatika awamu hii ya serikali angalau ijayo.
Prof. Muhongo anahitaji kutiwa moyo na kupata "support" ya watanzania wotekwani si mnafiki kama baadhi tunaoamini ni "wachapakazi" kumbe ndani yao ni ufisadi mtupu!