Waziri Muhongo ni muongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Muhongo ni muongo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwinukai, Aug 27, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Licha ya kusema bungeni kuwa suala la mgao wa umeme ni HALIKUBALIKI lakini sas naona limeanza kukubalika kutokana na mgao wa umeme ambao hautangazwi bila shaka ni kwa lengo la kuficha aibu, Je mgao wa umeme kurudi kinyemela hii haimanishi kuwa WAZIRI MUHONGO NI MUONGO?
   
 2. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mafisadi wanamhujumu ili aonekane muongo. Usicheze na wenye pesa!!!!!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wanafanya kila hila kumuhujumu ili aonekane hafai; laki kwa vile tumemtanguliza MUNGU watashindwa tu!!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  wewe ndo mwoongo tumuache proff afanye kazi yake umeme kukatika ni miundombinu mibovu tuuu!
  KUMBUKENI MLIKOTOKA BANA, MWAKA JANA KAMA LEO HII MGAO NI MKUBWA SANA!
   
 5. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Labda wanafanya ukarabati wa mitambo
   
 6. s

  siyabonga Senior Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha post za kinafiki! Mpeni prof nafasi afanye kazi.

  Bila shaka magamba yamemzunguka aonekane hafai, ingawa amejimbanua tayari kuwa ana uchungu na wananchi.

  Mtu huyu, ni sawa ni yule aliyeomba akumbukwe katika ufalme ujao.

  Prof, wakikuboa, rudi kafundishe. Utaitendea vema nchi yako kwa kusimama imara. Utakumbukwa.
   
 7. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Waongo ni Mhando, Mboma, wenye mikataba isiyo na tija kwa Taifa (Symbion) na majenereta yao pamoja na mafisadi walionyimwa tenda ya kuuzia Tanesco mafuta kwa bei ya juu maana kama tuna uwezo wa kufua umeme kuliko hitaji la Taifa, mgao utakubalikaje? Sisi tunakubali kukatika umeme (kwa muda mfupi tu) kabla ya marekebisho kutokana na miundo-mbinu chakavu lakini hatukubali migao. Ukikubali mgao hukosi miongoni mwa makundi tajwa hapo juu au wafaidika na mfumo huo! Wizara ikishindwa kuwakabili kwa hujuma zenu, nguvu ya umma itawaonyesha adabu na majenereta yenu mliyorithishana toka Richmond!
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Toa upuuzi hapa. Inamaana serikali inazidiwa nguvu na mafisadi, basi si bora tuwape nchi watuongoze wao.
   
 9. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu serikali yako inayongozwa na legelege JK ni serikali DHAIFU, wala hauitaji kupigwa fimbo ili uelewe... Wanachojua viongozi wako ni lini anatakiwa aende kubadili damu...
   
 10. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa maana hiyo KPI ya Muhongo usitegemee kuwa bora ktk mazingira ya mambo LEGELEGE!
   
 11. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Haitakuwa ajabu kwa Muhongo kuwa mwongo maana ni bonge la TISS!!

  Moja wapo ya sifa ya kuwa TISS, ni lazima uwe mwongo. Mwanagalie JK, Kikula wa UDOM, n.k.
   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Unaweza kufikisha ujumbe bila hata kutukana. Hili la mafisadi kuwa na nguvu kuliko serikali ya kikwete halina ubishi kwani hata Pinda aliwahi kukiri hivyo.
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Nimetukana wapi? Hii sio serikali ya kikwete ni serikali yetu, Kikwete ni mtu mdogo sana kwenye serikali yetu, kama tukiamua hata leo hawezi kuitwa rais tena, kwa hiyo mnapotokea na kutoa maneno ya kufedhehesha namna hii mimi binafsi ninachukia sana.

  Ukifuatilia msingi za wanaosema Muhongo anafanywa nini sijui na mafisadi utagundua kwamba wanatembea na hoja ile ile ya Kikwete ni imara ila mawaziri wake ndio wanamuangusha, waziri mzima mambo yaliyo ndani ya mamlaka yake yanahujumiwa vipi na mtu wa namna yoyote ile? Kama ni hujuma wanahujumiana wao kwa wao, ccm wanatuhujumu watanzania, hakuna fisadi asiye mwanaccm nchini hii, kwa kifupi uwezo mzima wa ccm kusimamia serikali umedhoofika sana, hatuhutaji kusikia kisingizio chochote kile, na matusi ni haki yao washenzi hawa.
   
 14. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu, upo sahihi na wala hujatukana mtu, hiyo ndo lugha pekee iliyobaki ya kuwaambia hawa MAFISADI, MAJAMBAZI na WANYANG'ANYI wanaliibia taifa la Tanzania mchana kweupe huku viyoyozi vikiwapepea. kwa kweli mkuu hawa ccm ni WASHENZI, sio kuwatukana ila ndo sifa wanayostahili. we ngoja kiama chao kinakaribia, ngoja tuwaamshe wananchi waamke wajue umuhimu wa KULINDA KURA.
   
 15. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  duara ni lile lile ukijichanganya na wachafu utachafuka tu !
  Prof. Endelea na style yako SHOKA 1 MBUYU CHINI.
   
 16. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sanagarara elewa kwamba mafisadi wapo ndani ya serikali pia na serikali kwa namna moja inawatetea! Kama hawana nguvu mbona serikali imeshindwa kuchukua hatua kuhusu vitendo vingi vya kifisadi km richmond, rada, EPA, deep green, meremeta nk? Ndugu ushauri wa bureee funguka!!!!!
   
 17. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kumbuka kiraja mkubwa wao aliwahi kusema mjengoni hatari ya hawa watu
   
 18. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tusianze kumlaumu Prof Muhogo bali kumpa moyo. Kubadilisha mfumo uliokuwepo kwa zaidi ya miaka hamsini ni kazi kubwa. Tumpe muda angalau mwaka mmoja tuone. Bila shaka tutaridhishwa na kazi yake kama mafisadi hawatamhujumu.
  Mbona serikali imeshindwa kutakeleza kauli mbiu yake ya Maisha bora kwa kila mtanzania kwa takribani miaka saba sasa? Watanzania tuache tabia ya kulalama na kunyooshea wengine vidole bila sababu za msingi.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  ....[/QUOTE]

  Hakuna kitu kama hicho, serikali ndio imejisalimisha kwa mafisadi kwa maslahi binafsi ya viongozi, na sio kweli kwamba mafisadi wameizidi nguvu serikali, unataka kuniambia mafisadi wanaweza wakasema mchakato wa uandikaji katiba mpya usitishwe na ukasitishwa?

  Na kama kweli unataka tukae hapa tufunguane kwamba mafisadi wameishinda serikali kuna mantiki gani sasa ya kutaka kukiondoa chama cha mapinduzi kuingoza serikali yetu.

  sisi ndio serikali, watu tuliowapa dhamana ya kuiongoza serikali wametusaliti, alafu sielewi ni kitu gani kinawasukuma watu kutoa kauli zinazowatenganisha mafisadi na CCM, naona kama kuna hoja mfu inaota mizizi hapa.
   
 20. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wengi hamuelewi kinachoendelea mnaongea siasa tu kama za prof. muhongo muongo, bila kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme zaidi mgao upo pale pale, kwa hali ilivyo mgao hauepukiki subirini muone, watanzania manadanganyika kirahisi sana.
   
Loading...