Waziri Muhongo: Gesi ya Mtwara itatoka!

Waziri Muhongo: Gesi ya Mtwara itatoka!

Pasco, VUTA-NKUVUTE,

..Prof.Muhongo anatakiwa aache lugha za kibabe.

..huyu ni Professor mwandamizi, sasa sielewi kwanini anashindwa "kuwasomesha" na kuwashawishi wananchi wa Mtwara mpaka wakaunga mkono mradi wa gesi.
Hili ndio tatizo lao despite having a clear argument, ukifutalia matatizo ya Tanesco na gharama za kuzalisha umeme kwa sasa, sababu za mwekezaji kutoa huo mkopo maana na yeye at the end anataka kuona hela yakee inarudi.

Kifupi ni kwamba gesi lazima iende dar, tatizo ni mbimu za kutoa elimu ndio hafifu na majibu ya kiburi.
 
Naomba itoke! Hatujachoka kuona damu ya Watanzania wenzetu ikimwagika bila sababu huku wakiwindwa kama swala, paa na digidigi, sembuse tembo mbugani? Tuwe na huruma. Wengi wamepata ulemavu wa maisha, wamechomewa nyumba zao na kusingiziwa mambo lukuki; au hamsomi magazeti? Kosa lao kubwa limekuwa kuhoji kwa nini Serikali imekwenda kinyume na ahadi ilizoziweka; wameuliza tu. Hawajasema gesi haitoki. Wamesingiziwa, huo ndio ukweli. Hivi sasa Mtwara ni kama imetangazwa hali ya hatari; Jeshi la Wananchi, badala ya kuwalinda raia, linawapiga, linawatesa, linawanyang'anya mali zao. Haki iko wapi?

Hii si Tanzania niliyojivunia kuwa raia wake. Jahazi linaenda mrama, nahodha hana habari. Iko siku litazama. Nani wa kutuokoa?

Ee Mungu tunusuru na dhahama hii, ona jinsi watoto wako tunavyoteseka.
 
Kuna maprofesa wengine ukiwafikiria unashindwa kujua wana kilo ngapi za ubongo, na ubongo walio nao ni wa aina gani. Ubongo wa binadamu umejengwa kutafsiri information za aina mbalimbali na kuzitolea maamuzi, lakini inaelekea kuwa maprofesa wetu wana ubongo unaotafsiri information za aina moja tu.
 
Pasco, VUTA-NKUVUTE,

..Prof.Muhongo anatakiwa aache lugha za kibabe.

..huyu ni Professor mwandamizi, sasa sielewi kwanini anashindwa "kuwasomesha" na kuwashawishi wananchi wa Mtwara mpaka wakaunga mkono mradi wa gesi.


Ndugu yangu.....
Nadhani na wewe unatambua hili;
Kwamba katika sakata la GESI INATOKA AMA HAITOKI NTWARA kuna pande 3

Upande wa Kwanza ni wa serikali,unasema GESI ITOKE kwa sababu ni rasilimali ya Taifa zima,ingawaje inajali kwamba walio katika eneo gesi inakotoka watafaidishwa kwa mpango maalumu....na imetoa Elimu hiyo kwa Wana Ntwara

Upande wa pili ni wa Wana Ntwara,ambao wao wanasikiliza maneno toka pande mbili,yaani serikali inawaambia nini,na wakati huo huo wanasikiliza upande wa tatu nitakaoutaja.....

Upande wa tatu ni wa Wanaharakati na Wanasiasa,ambao malengo yao ni mchanganyiko na hawako Organised...wengine wanataka kuwatetea wana Ntwara ili wapate kipande chao...na wengine ,hasa Wanasiasa,wanataka watimize malengo yao kwa kupitia mgongo wa kujifanya wanawatetea Wana Ntwara.....Kundi hili pia wapo wanaharakati ambao wao pia kutokana na kulobiwa/kupumpiwa na "maadui"(Taasisi,watu binafsi,makampuni makubwa) ambao wanaona hatari ya wao "kutokupata faida kutokana na uwepo wa bomba hilo la gesi"(maadui wa ndani na nje ya Nchi),basi wanapaza sauti za kuhakikisha kwamba mgogoro huu hauishi kama ambavyo SERIKALI NA WANA NTWARA wangelitaka.

Hivyo basi....Professor ana Kazi ngumu kwani kuweza kuwatimizia haja zao,hasa hawa wa Kundi la tatu ni ngumu sana...na hawa ndio "wanaongea lugha za Kijiweni zinazowapa mshawasha wana ntwara kujua kweli wanatetewa".....kUMBE WATU WANAPATA AJIRA KWA KUFUKISHA MGOGORO....WATU WANAPATA KURA KWA KUFUKISHA MGOGORO.....

Lakini pia,tunawashukuru wale ambao kwa Moyo wa Ukweli wanawaamusha wana Mtwara waweze kujua namna ya kuibana serikali ili mkataba uwe wa win-win formation....
 
Nina mashaka na the motive behind taarifa hii!.
Uchochezi!.
Mimi ni ssupporter mkubwa wa gesi ya Mtwara lazima itoke!.
Pasco
bora ume-declare interest.uzuri ni kwamba hiyo guts ya kutamka hayo unaipata ukiwa within the sphere of ur laptop/desktop/smartphone.dondoka mtwara saa hii halaf tamka hivyo ka sauti kuu.
 
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amekaririwa leo akisema kuwa gesi asilia ya Mtwara itatoka na Serikali itaendelea kutekeleza mipango yake kama ilivyopangwa.

Waziri Muhongo ameyasema hayo baada ya Serikali kutia saini Mkataba wa Uzalishaji wa Umeme na Kampuni moja ya nchini China leo hii.Uzalishaji huo wa umeme utafanyika katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Waziri Muhongo amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaopinga kutumika kwa gesi asilia ya Mtwara.

Bomba la kusafirisha gesi hiyo litaanza kujengwa wakati wowote kuanzia sasa.'Hadi kufikia mwisho wa mwaka ujao,Tanzania itakuwa inauza umeme nchi za nje' aliongeza Waziri Muhongo.

Wananchi wa Mtwara wameshasikilizwa au ndio wamepuuzwa?

Chanzo: Mimi mwenyewe na East Africa Radio

Cc THE BIG SHOW na Sizinga

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kwa bei gani umeme utakao uzwa nje ya nchi,ndo ule we capacity charges inasemekana Tanzania ndo yenye umeme ghali east and central Africa, tutauza wapi ,Zambia wanao umeme wa uhakika kutoka victoria falls, Uganda wanao umeme wa uhakika kutoka Nile.
Msumbiji ambako kuna gesi nyingi sana mara 10 zaidi ya gesi tuliyo nayo, na wao watakuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme wao na kuuza kwenye soko kubwa Afrika kusini

,Malawi hatuna uhusiano mzuri sio hivyo ni likely watapata kutoka Zambia au
 
Siunge mkono mambo mengi jinsi serikali ya CCM inavyofanya lakini kwenye hili suala la gesi, wapo sahihi kabisa. Rasilimali ya gesi ni lazima itumike kwa namna iliyo bora kiuchumi. Bomba la gesi ni lazima liende Dar kwaajili ya uzalishaji umeme na matumizi mengine. Hatua kwa hatua, bomba hilo siku moja linatakiwa lifike Kigoma mpaka nchi jirani. KUSEMA GESI ISITOKE MTWARA NI FIKRA ZA AJABU LAKINI KUTAKA WANANCHI WA MTWARA KAMA WALIVYO WATANZANIA WENGINE, WAFAIDIKE NA RASILIMALI INAYOTOKA KATIKA ENEO LAO NI SAHIHI.
 
Pasco, VUTA-NKUVUTE,

..Prof.Muhongo anatakiwa aache lugha za kibabe.

..huyu ni Professor mwandamizi, sasa sielewi kwanini anashindwa "kuwasomesha" na kuwashawishi wananchi wa Mtwara mpaka wakaunga mkono mradi wa gesi.

Alishawaeleza kutosafirisha gesi kutaigarimu serikali pesa nyingi za ujenzi wa mitambo mipya huko Mtwara. So, ni kuisafirisha kwenda Dar kwenye mitambo.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ambapo sijaelewa ni pale aliposema mwishoni mwa mwaka tutauza umeme nje ya nchi. hapo hapo akasema mwisho wa mwaka umeme utakuwa umewafikia 30% ya watanzania wote.
Ina maana tutaanza kuuza umeme wakati kuna watanzania wengine hawajapata umeme?
 
Huyu Professor alianza kazi kwa kishindo kama Enzi za Augustine Lyatonga Mrema lakini keshapoteza mwelekeo yaani siasa mbele Uprofesa pembeni. Ndiyo maana wapiga kura wa Korogwe walimchagua Stephen Ngonyani "Profesa Majimarefu" elimu darasa la saba na kumkataa Joel Bendera "MBA" kutokana na kuchoka kudanyangwa na msomi mwenzetu.
 
Huyu Professor alianza kazi kwa kishindo kama Enzi za Augustine Lyatonga Mrema lakini keshapoteza mwelekeo yaani siasa mbele Uprofesa pembeni. Ndiyo maana wapiga kura wa Korogwe walimchagua Stephen Ngonyani "Profesa Majimarefu" elimu darasa la saba na kumkataa Joel Bendera "MBA" kutokana na kuchoka kudanyangwa na msomi mwenzetu.

Naona una ropokwa tu!
 
Mimi ambapo sijaelewa ni pale aliposema mwishoni mwa mwaka tutauza umeme nje ya nchi. hapo hapo akasema mwisho wa mwaka umeme utakuwa umewafikia 30% ya watanzania wote.
Ina maana tutaanza kuuza umeme wakati kuna watanzania wengine hawajapata umeme?
 
Nina mashaka na the motive behind taarifa hii!.
Uchochezi!.
Mimi ni ssupporter mkubwa wa gesi ya Mtwara lazima itoke!.
Pasco

Wasisahau ulinzi, kama wamefanikiwa kuwaleta wachina kuja kulijenga hilo bomba basi pia na walinzi wawe nao wakutosha. Ushauri wa bure nakupeni wakina Pasco na mafisadi wenzako, muwe na kitengo cha kukarabatri hilo bomba kila linapo haribiwa
 
Gesi ya Mtwara imeshatoka inakuja DSM tuongee mengine sasa kwa hili wapenda maendeleo wameshinda.

Hivi watu wa Mtwara hawataki hayo maendeleo? Fikra zako ni finyu sana. Mtwara imekosa opportunity ya maendeleo na watu wake walikuwa wanalilia maendeleo kwa akili yako ya kinguruwenguruwe maendeleo maana yake kuleta gesi dar na kule inakotoka kubaki maskini tu.
 
Back
Top Bottom