Waziri Muhongo: Gesi ya Mtwara itatoka!

Waziri Muhongo: Gesi ya Mtwara itatoka!

Alishawaeleza kutosafirisha gesi kutaigarimu serikali pesa nyingi za ujenzi wa mitambo mipya huko Mtwara. So, ni kuisafirisha kwenda Dar kwenye mitambo.

Ndugu yangu haihitaji uwe na PhD kuona ukweli wa jambo hili. Si kweli kwamba serikali itatumia pesa nyingi kwa kujenga mitambo Mtwara. Mitambo iliyopo pale Ubungo haina extra capacity iliyo-idle inayosubiri gesi ya ziada. Umeme unaotarajiwa kuzalishwa utatokana na mitambo mipya ambayo wawekezaji wake ndio kwanza wanatafutwa mfano kampuni ya GE ya USA; CPI ya China na nyinginezo ambazo ziko kwenye majadiliano na serikali. That means makampuni haya yataleta mitambo yake na kuisimika hapa Dar baada ya gesi ya kutoka Mtwara kufika Dar. Technically, serikali itakuwa imeingia deni la ujenzi wa bomba la gesi la gharama kubwa na kisha kuingia kwrnye mikataba ya uzalishaji umeme na kuuza. Hakutakuwa na unafuu wowote hapa kwa sababu tumeambiwa huenda umeme ukapungua kwa 6% tu. Wakati huo huo mkopo wa tillion za bomba la gesi utaendelea kuwaelemea wananchi kwa nyongeza za kodi n.k.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba iwapo mitambo ya umeme haijapatikana kuna tatizo gani mitambo hiyo kuwekwa Mtwara ambako kuna miundombinu ya usafirishaji wa mitambo mizito kwa njia ya baharini? Halafu baada ya kufanya hivyo gharama za bomba la gesi sio zingepungua na hivyo kupunguza deni la taifa na mzigo wa kodi kwa vizazi vijavyo?

Naomba watu wanaochangia mada kwa kutumia akili za akina Muhongo zilizopinda kama Mizengwe iliyopinda wajaribu kuangalia mambo in real world. Wao tayari wanaagenda zao. Labda kama na wewe ni -------- kama wao
 
CCM NEVER STOP TO AMAZE ME. Yaani Prof. wa Kweli kama Prof. Muhongo hana tofauti na Prof. wa Miti shamba Stephen Ngonyani.

wakati wa exploration ya gas wana Mtwara waliahidiwa hivi (na haya yako kwenye Ilani ya CCM)
  1. Banadari ya Mtwara itaboreshwa/itajengwa upya kurahisisha usafirishaji wa gas
  2. Mitambo ya kufua umeme ya gas asilia itajengwa Mtwara na kuingizwa kwenye grid ya Taifa

Baada ya gasi asilia kupatika Mtwara mambo yamekuwa hivi

  1. Bandari inayojengwa sasa ni ya Bagamoyo sio tena Mtwara
  2. Mitambo ya kuzalisha umeme wa gas asilia inajengwa Kinyerezi DSM na sio tena Mtwara

"Ukila na KIPOFU usimshike MKONO". Hata kama wananchi wa Mtwara ni VIPOFU, lakini kwa huu UNDUMILA KUWILI wa Serikali ya CCM, hakuna Mwananchi yeyote MAKINI wa MTWARA atakayeiamini serikali. PLUS kwamba wananchi wa Mtwara wameshaona kwa watanzania wenzao ambako MADINI yanapatikana jinsi walivyoingiza MKENGE, kwa mwamvuli huo huo wa Raslimali za nchi hii ni za Watanzania wote. Kumbe zinakwenda kuwanufaisha WARASIMU wachache wa DSM na wananchi kunapopatikana rasilimali hizo wakiachwa hohe hahe!

Tupende tusipende SERIKALI YA CCM ni Tatizo, kwasababu haiko kwaajili ya watanzania.
 
Wasisahau ulinzi, kama wamefanikiwa kuwaleta wachina kuja kulijenga hilo bomba basi pia na walinzi wawe nao wakutosha. Ushauri wa bure nakupeni wakina Pasco na mafisadi wenzako, muwe na kitengo cha kukarabatri hilo bomba kila linapo haribiwa
Kumbe na Pasco mimi fisadi!?.
Vandalism is criminal offence punishable by law!. Walinzi wa bomba watapewa delegated powers za kuwapunish vandals by capital punishment kabla vandalism haijafanyika!.

Kwani baada ya kilichofanywa kwenye yale maandamano ya Chadema Arusha bila kibali umeowahi kuona wananchi wakijitokeza tena kwenye maandamano bila kibali?!.

Kitakachowakuta the would be vandals kitawafanya wengine wote wolione hilo bomba kama kituo cha polisi!. Apart from electrical bubbled wire plus armed man within every 100m with expressly order to .....
wee tuu!, unless kama pia tumepanga ku recruit suicidal vandals!.
Pasco
 
Pasco wait and see
 
Hivi watu wa Mtwara hawataki hayo maendeleo? Fikra zako ni finyu sana. Mtwara imekosa opportunity ya maendeleo na watu wake walikuwa wanalilia maendeleo kwa akili yako ya kinguruwenguruwe maendeleo maana yake kuleta gesi dar na kule inakotoka kubaki maskini tu.

Maendeleo ni kutumia rasilimali za nchi kwa maendeleo ya wote.

Wakiachiwa wananchi wa Mtwara wakachimbe hiyo gesi kwani itawanufaisha na nini?
 
Mzee acha kuweka uchochezi wa kipuuzi wanamtwara washaeleweshwa. Hisia za kijinga hizo hawana.

Kama WanaMtwara wameshaeleweshwa na kukubaliana na serikali kwa nini then Waziri anasema kuwa gesi itatoka?
 
Ndugu yangu.....
Nadhani na wewe unatambua hili;
Kwamba katika sakata la GESI INATOKA AMA HAITOKI NTWARA kuna pande 3

Upande wa Kwanza ni wa serikali,unasema GESI ITOKE kwa sababu ni rasilimali ya Taifa zima,ingawaje inajali kwamba walio katika eneo gesi inakotoka watafaidishwa kwa mpango maalumu....na imetoa Elimu hiyo kwa Wana Ntwara

Upande wa pili ni wa Wana Ntwara,ambao wao wanasikiliza maneno toka pande mbili,yaani serikali inawaambia nini,na wakati huo huo wanasikiliza upande wa tatu nitakaoutaja.....

Upande wa tatu ni wa Wanaharakati na Wanasiasa,ambao malengo yao ni mchanganyiko na hawako Organised...wengine wanataka kuwatetea wana Ntwara ili wapate kipande chao...na wengine ,hasa Wanasiasa,wanataka watimize malengo yao kwa kupitia mgongo wa kujifanya wanawatetea Wana Ntwara.....Kundi hili pia wapo wanaharakati ambao wao pia kutokana na kulobiwa/kupumpiwa na "maadui"(Taasisi,watu binafsi,makampuni makubwa) ambao wanaona hatari ya wao "kutokupata faida kutokana na uwepo wa bomba hilo la gesi"(maadui wa ndani na nje ya Nchi),basi wanapaza sauti za kuhakikisha kwamba mgogoro huu hauishi kama ambavyo SERIKALI NA WANA NTWARA wangelitaka.

Hivyo basi....Professor ana Kazi ngumu kwani kuweza kuwatimizia haja zao,hasa hawa wa Kundi la tatu ni ngumu sana...na hawa ndio "wanaongea lugha za Kijiweni zinazowapa mshawasha wana ntwara kujua kweli wanatetewa".....kUMBE WATU WANAPATA AJIRA KWA KUFUKISHA MGOGORO....WATU WANAPATA KURA KWA KUFUKISHA MGOGORO.....

Lakini pia,tunawashukuru wale ambao kwa Moyo wa Ukweli wanawaamusha wana Mtwara waweze kujua namna ya kuibana serikali ili mkataba uwe wa win-win formation....
Apollnary,

..hizi habari za kudai kuna "maadui" wa ndani na nje ya nchi huwa siziamini sana.

..sasa serikali ikishaamini kwamba wananchi, wanaharakati, na vyama vya siasa, wanashawishiwa na "maadui" wa ndani na nje unafikiri kutakuwa na muafaka hapo?

..baada ya hapo nini kinawazuia na wengine kuamini kwamba serikali nayo inashawishiwa na "maadui" wa ndani na nje?

..kitu cha msingi hapa ni kujadiliana huku tukiamini kila mmoja ana nia njema ya kuwasaidia wananchi. tujadiliane na tuchukue yale mazuri toka kila upande-- serikali, wanaharakati, vyama vya siasa, etc etc.

..binafsi naendelea kusisitiza kwamba Professor Muhongo angetumia lugha ya kistaarabu; angeelekeza badala ya kufokea na kutuhumu; basi angeweza kabisa kutuepusha na vurugu za Mtwara.

cc: Pasco, THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
Nina mashaka na the motive behind taarifa hii!.
Uchochezi!.
Mimi ni ssupporter mkubwa wa gesi ya Mtwara lazima itoke!.
Pasco

Pasco gesi itatoka lakini majibu na kishindonyuma watapata hapo 2015 watake wasitake, "liwalo na liwe" waacha wapigwe tu maana tumechoka.
 
Pasco, VUTA-NKUVUTE,

..Prof.Muhongo anatakiwa aache lugha za kibabe.

..huyu ni Professor mwandamizi, sasa sielewi kwanini anashindwa "kuwasomesha" na kuwashawishi wananchi wa Mtwara mpaka wakaunga mkono mradi wa gesi.
kuwa profesa haimaanishi kujali feelings za watu...
ninaamini kabisa huyu profesa anapoongea huwa hajali maneno yake yatachukuliwaje na watu, anaongea tu.
Nina uhakika hiyo wizara ingekuwa inaongozwa na mtu mwenye maneno matamu kwa wananchi wala wanamtwara wasingefika huko walikofika, maneno yake ndo yanawafikisha huko.
Sawa yeye ni mtaalamu wa mambo hayo ya gesi.... haiwezekani kukawa na msemaji wa wizara? ili yeye afanye maamuzi tu huko kwenye madokezo inapofikia swala la kuongea na wananchi basi afanye mwingine.
 
Siyo yeye tuu, bali ni serikali nzima.

Linapokuja suala la public relations, serikali inalazimisha kile ambacho inakiamini hata kama kina makosa.

Hawapendi kusikiliza upande wa pili, even hata constructive criticisms. Wanalazimisha mambo tuu.

Juzi tuu waliomba ushauri kutoka kwa watu huko Ulaya, wakaandikiwa ripoti nzuri ikiwashauri tena kwa wema kabisa kuwa serikali iwe inawahusisha wadau katika uvunaji wa rasilimali kama gesi.

Wakashauriwa kuwa wananchi washirikishwe katika kujua kilichokubaliwa kwenye mikataba ya madini, gesi, n.k.

Wakashauriwa mawasiliano kati ya serikali na wadau ni muhimu sana katika sekta ya madini. Baada ya kushauriwa hivyo, walichokifanya ni Wizara ya Nishati na Madini kufungua ID hapa JF probably kama sehemu ya kurahisisha mawasiliano. Whether hiyo ID inatumika ipasavyo kufanya hayo mawasiliano sijui.

Lakini wakati huo huo, Waziri wa Wizara husika yuko kwenye redio akisema eti gesi itatoka tuu kama vile anataka kuwakomoa wanananchi wa huko.

Nae Waziri Mkuu anakuja na vitisho eti wana majina ya watu ambao wanaendesha kampeni ya gesi haitoki.

Kwa nini wasitumie huo muda kukaa na watu na kuwawasikiliza? Kwa nini serikali isifuate ushauri iliyoomba yenyewe ambapo ilishauriwa kuwa ni muhimu sana kuwasikiliza wadau na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na wadau?

Kwenda mbele ya mic ya redio iliyoko Dar na kuwaambiwa watu wa Mtwara kuwa gesi itatoka ndiyo kuwasilikiliza na kufanya mawasiliano na hao wadau?

Kuna watu hata communication skills za kuwasiliana na watu wanaowaongoza hawana.

Watu hawa watatendelea kuwa watawala na siyo viongozi. Viongozi wanawasikiliza wanaowaongoza. Watawala kazi yao ni kutawala tuu na wanaamini kuwa wako sahihi kwa kila kitu.

Ndiyo maana wanadai kuwa gesi lazima itoke. Kiongozi wa ukweli angesema tujadiliane tuone jinsi gesi itakavyotoka.
 
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amekaririwa leo akisema kuwa gesi asilia ya Mtwara itatoka na Serikali itaendelea kutekeleza mipango yake kama ilivyopangwa.

Waziri Muhongo ameyasema hayo baada ya Serikali kutia saini Mkataba wa Uzalishaji wa Umeme na Kampuni moja ya nchini China leo hii.Uzalishaji huo wa umeme utafanyika katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Waziri Muhongo amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaopinga kutumika kwa gesi asilia ya Mtwara.

Bomba la kusafirisha gesi hiyo litaanza kujengwa wakati wowote kuanzia sasa.'Hadi kufikia mwisho wa mwaka ujao,Tanzania itakuwa inauza umeme nchi za nje' aliongeza Waziri Muhongo.

Wananchi wa Mtwara wameshasikilizwa au ndio wamepuuzwa?

Chanzo: Mimi mwenyewe na East Africa Radio

Cc THE BIG SHOW na Sizinga

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
afaahamu ya kuwa habari inevuja kuwa ni mradi wake na boss wake maana ukweli ametuonyesha obama aliposaini mradi wa simbion kumaliza tatizo la umeme tz wakati yeye alidai gesi ni kwa ajili ya umeme wa tz jana anasema umeme wa kuuza nje ya nchi
 
Ndo maana mimi naamini ifike mahali sasa wataalamu wabaki kuwa wataalamu na wana siasa wawe wanasiasa. kuiletea nchi maendeleo siyo lazima uwe mwanasiasa?
simfahamu Muhongo, lakini nasikia ni mtaalamu mzuri tu wa hayo mambo ya resources, lazima atakuwa anafahamu vizuri ili hizo resources ziweze kuisaidia nchi nini kifanyike, hata kama siyo mchumi......
kwani kulikuwa na shida gani JK angemteua kuwa mshauri wa hayo mambo ya resources akiwa huko huko UD bila kuwa waziri wa Nishati?
sasa mbona mimi naona kama reputation/credibility yake inashuka sana baada ya kuwa waziri?
nakumbuka wakati anateuliwa watu walimsifia sana hapa na nje kuwa tumepata kichwa, mbona mambo yamegeuka?
Jamani uongozi ni more than kujua in and out ya kitu.
Siyo yeye tuu, bali ni serikali nzima.

Linapokuja suala la public relations, serikali inalazimisha kile ambacho inakiamini hata kama kina makosa.

Hawapendi kusikiliza upande wa pili, even hata constructive criticisms. Wanalazimisha mambo tuu.

Juzi tuu waliomba ushauri kutoka kwa watu huko Ulaya, wakaandikiwa ripoti nzuri ikiwashauri tena kwa wema kabisa kuwa serikali iwe inawahusisha wadau katika uvunaji wa rasilimali kama gesi.

Wakashauriwa kuwa wananchi washirikishwe katika kujua kilichokubaliwa kwenye mikataba ya madini, gesi, n.k.

Wakashauriwa mawasiliano kati ya serikali na wadau ni muhimu sana katika sekta ya madini. Baada ya kushauriwa hivyo, walichokifanya ni Wizara ya Nishati na Madini kufungua ID hapa JF probably kama sehemu ya kurahisisha mawasiliano. Whether hiyo ID inatumika ipasavyo kufanya hayo mawasiliano sijui.

Lakini wakati huo huo, Waziri wa Wizara husika yuko kwenye redio akisema eti gesi itatoka tuu kama vile anataka kuwakomoa wanananchi wa huko.

Nae Waziri Mkuu anakuja na vitisho eti wana majina ya watu ambao wanaendesha kampeni ya gesi haitoki.

Kwa nini wasitumie huo muda kukaa na watu na kuwawasikiliza? Kwa nini serikali isifuate ushauri iliyoomba yenyewe ambapo ilishauriwa kuwa ni muhimu sana kuwasikiliza wadau na kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na wadau?

Kwenda mbele ya mic ya redio iliyoko Dar na kuwaambiwa watu wa Mtwara kuwa gesi itatoka ndiyo kuwasilikiliza na kufanya mawasiliano na hao wadau?

Kuna watu hata communication skills za kuwasiliana na watu wanaowaongoza hawana.

Watu hawa watatendelea kuwa watawala na siyo viongozi. Viongozi wanawasikiliza wanaowaongoza. Watawala kazi yao ni kutawala tuu na wanaamini kuwa wako sahihi kwa kila kitu.

Ndiyo maana wanadai kuwa gesi lazima itoke. Kiongozi wa ukweli angesema tujadiliane tuone jinsi gesi itakavyotoka.
 
Kwa nn wachina waje kuwekeza kwenye gas hapa?jana kama ulimsikiliza yule professor wa china kule chuo kikuu nalisema lazima Tanzania wawe na mikakati na si wengine watuwekee mikakati ndo tuendelee.hapa la kujiuliza te mikakati ya Tanzania ni ipi???

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
...nakumbuka wakati anateuliwa watu walimsifia sana hapa na nje kuwa tumepata kichwa, mbona mambo yamegeuka? Jamani uongozi ni more than kujua in and out ya kitu.

Yea, watu walimwagia mafisa hapa.

Kiongozi mzuri siyo lazima profesa.

Sometimes, ni shida pia kuanza siasa ukubwani.
 
Back
Top Bottom