Sina hakika kama nimekuelewa hususani hapo uliposema $ 60 billion...labda ungeweka hiyo source hapa tukaisoma vizuri ndipo tungejadili vizuri. Hata hivyo, ngoja nijaribu kukujibu kama nilivyokuelewa.
Kwanza kabisa nikukumbushe ni hiyo Production Sharing Agreement(PSA) ndiyo inayotoa 65% kwa serikali(kupitia TPDC) na 35% Kwa investor. Arrangement iliyopo ni kwamba, mwenye leseni ya vitalu ni TPDC..so, mwekezaji anaenda kwa TPDC na (assume no ufisadi) ku-prove ana uwezo wa kufanya kazi; financially and in terms of technology among other things. Sina hakika mwenzangu una PSA ya mwaka gani lakini the latest PSA, ime-include payments on signing license, ambayo zamani haikuwapo, na pia imeongoza Royalty Fee. Na kingine kilichobadilika ni training fee kwa locals ambayo imepanda kutoka $ 150,000/ to 500,000/ kwa mwaka.
Hivyo basi, investor akishapata vitalu, either solely or in partnership kama ilivyokuwa kwa Ophir na BG; vile vile kuna room kwa TPDC ku-share production costs...but all in all; mwisho wa cku, TPDC anachukua 65% ya profit na mwekezaji anachukua 35%. Hii ndiyo latest PSA.
Sasa tukirudi kwenye hoja ya hapo juu ni kwamba, origin partnership ni ya Ophir 40% na GB 60%. Hii maana yake ni nini, profit share ya BG ni 60% ya hiyo 35% ambayo ni 21% wakati Ophir ni 40% ya hiyo 35% ambayo ni 14% ambapo aggregate profiti sharing itakuwa TPDC 65% + 21%+14%=100%.
Hata hivyo, Ophir ameuza 20% ya share zake. Kama reference yetu ni among investors, ni kwamba wameuza 20% ya ile 40% ambayo itakuwa ni 8% na mwenyewe kubakiwa 32% na hatimae inakuwa BG 60%+Ophir 32% + Pavillion 8%. Lakini linapokuja suala la Profit sharing (assuming profit sharing itatokana na umiliki wa mradi), maana yake ni kwamba Ophir ameuza 20% ya 21% ambayo ni 4.2% na mwenyewe kubakiwa na 16.8%...so, the whole sharing itabadilika na kuwa TPDC 65%+BG 21%+Ophir 11.2% + Pavillion 2.8%=100%. So, in either way, percentage ya TPDC inabaki palepale.
Sasa hoja hapa ni hiyo 20% ya 40% ambayo Ophir ameuza. Kama nilivyosema hapo awali, nimeshindwa kabisa kukuelewa uliposema "gas iliyouzwa ina thamani ya $60billion." Je, unamaanizisha kwamba hiyo 20% ya share zake ameuza kwa $ 60 billion? Ungeweka hapa hiyo link ingekuwa vizuri. Lakini hata kama ndicho unachokimaanisha, bado nami ndicho hicho hicho nilichokisema hapo kabla. Nisome hapa chini kwenye RED
Hizi siasa za kugombea fito Watanzania sijui sitatufikisha wapi! Hapo kila mmoja ame-play role yake vizuri!
Zitto, kama mbunge ametekeleza wajibu wake na ameleta mswada wenye maslahi kwa taifa! Lakini Muhongo na wenzake nao wame-play part yao vizuri...kusimamia uuzaji na kuhakikisha taifa linapata stahiki yake. Hao wengine wasiolipa kodi si kwamba hakuna sheria; zipo na hawalipi.
KImsingi hapa hoja sio hiyo mnayoshindana nayo nyie; hoja ni kwamba je, hizo 20% ambazo Ophir wameuza kwa USD 1.3 Billion, kweli hiyo ndiyo thamani waliyouza? Let me keep it this way ili mpate kunielewa. Assume unanunua gari Japan kwa USD 250 million. Lakini unafahamu wazi kwamba, hiyo gari ya USD 250 million, TRA watachukua nyingi sana za kwao. Ili kukwepa panga zito la TRA, unaamua ku-collude na Seller na kisha anaandika Stakabadhi mbili; moja anaandika USD 250 million(hii unabaki nayo) na nyingine anaandika USD 100million (ndiyo unayoenda kuonesha TRA). Hii ilikuwa inafanyika sana; tena sana hadi TRA walipoamua kuanza kufanya evaluation wenyewe! Sasa basi, kodi ambayo ilibidi itokane na USD 250million, will eventually come from USD 100 million! Meaning that, at the end of story, TRA watachukua chini ya 50% ya kodi halisi!!
Hivyo basi, kama hakuna ushenzi wowote(Watanzania kutokana na kutopea uhalifu, mnaita "ujanja") na kwamba ni kweli kabisa Ophir wameuza hisa husika kwa USD 1.3 billion; then congrats to all waliohakikisha national interest zinazingatia hata kama ni wajibu wao kufanya hivyo...coz' they're being paid to do so.