Ezekiel Kamwaga | Raia Mwema - Toleo la 331 | 25 Dec 2013
TANZANIA inatarajia kupata mgawo wa takribani shilingi bilioni 400 kutokana na mauzo ya hisa yaliyofanywa na kampuni ya Ophir kwa kampuni ya Pavillion katika vitalu vya gesi vilivyopo nchini, Raia Mwema limeambiwa.
Kampuni ya Ophir inamiliki asilimia 40 ya hisa katika vitalu namba 1, 3 na 4 huku asilimia nyingine 60 ikimilikiwa na kampuni ya BG, lakini Ophir wameamua kuuza hisa zao 20, mwaka huu.
Mauzo ya hisa hizo yanatarajiwa kuiingizia Ophir kiasi cha dola bilioni 1.3 (shilingi trilioni mbili) na kutokana na mauzo hayo, Tanzania itapata kiasi cha dola milioni 260 (shilingi bilioni 400) kama kodi.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufaidika na mauzo ya hisa za rasilimali zake kupitia Kodi ya Ongezeko la Mtaji (Capital Gain Tax) ambayo ilipitishwa na Bunge mwaka jana.
Kodi hiyo ilipitishwa na Sheria ya Fedha (Finance Act) ya mwaka 2012 baada ya kuwasilishwa kama mapendekezo binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe na kisha Bunge kuridhia.
Katika miaka ya nyuma, Tanzania haikuwa ikifaidika na mauzo yoyote ya hisa kwa makampuni yanayouziana rasilimali zake kwa sababu Kodi hiyo ya Ongezeko la Mtaji haikuwepo.
Kwa sababu mauzo hayo ya hisa yana thamani ya dola hizo bilioni 1.3, serikali ya Tanzania inatakiwa kupata asilimia 20 ya kiasi hicho ambayo ni dola milioni 260.
Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, alisema wanatarajia kupata fedha hizo wakati wowote mauzo hayo yatakapopitishwa.
"Inategemea na namna hao wanaouziana hisa watakavyokubaliana lakini sisi tunafahamu tu kwamba wakimalizana, yetu itakuwa asilimia 20. Kwa vyovyote vile, inaonekana mauzo yanaweza kufanyika kwenye robo ya kwanza ya mwaka ujao wa 2014," alisema Simbachawene.
Ophir ina makao yake makuu katika miji ya London, Uingereza na Perth nchini Australia na kwa mujibu wa tovuti yake, ilianzishwa mwaka 2004. Kampuni ya Pavillion Energy inamilikiwa na serikali ya Singapore.
Vitalu ambayo vimeuzwa katika uuzianaji huo vinaelezwa kuwa na ujazo wa mita za ujazo trilioni 15 na mauzo hayo pia yameenda sambamba na uuzaji wa hisa nyingine 17.6 katika makampuni yatakayokuwa yakifanya biashara za gesi hiyo hapa nchini.
Kwa mujibu wa Simbachawene, makampuni hayo matatu ni Ruvuma Pipeline Company Limited, Mzalendo Gas Processing Company Limited na Fahari Marketing Limited.
Simbachawene alisema nia ya serikali kwa sasa ni kutaka kutumia fedha hizo kwa ajili ya kulipa madeni na kuliboresha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ingawa alisema itategemea pia na mahitaji mengine yatakayokuwepo wakati fedha hizo zitakapopatikana.
"Hizi ni fedha za Watanzania wote na si za wizara yetu pekee. Tunataka kuliwezesha shirika letu la umeme ili lifanye kazi vizuri na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme kwa watu wengi zaidi.
"Hata hivyo, sisemi kwamba ni hela zote zitatumika kwa kazi hiyo au la lakini kuna mawazo hayo. Mambo mengine serikali itaamua kutokana na wakati fedha hizo zitakapopatikana. Huwezi kujua kutakuwa na nini wakati huo," alisema Naibu Waziri huyo.
Alisema kwa miaka ya nyuma, Tanzania isingepata kitu kutokana na sheria zilizokuwepo na akasema serikali itajitahidi kuboresha sheria zake ili kuhakikisha inafaidika na utajiri uliokuwepo.
Mmoja wa wachambuzi wa masuala ya gesi aliyehojiwa na mtandao wa Bloomberg kuhusiana na uuzaji huu wa hisa, Tony Regan wa kampuni ya Tri Zen Inc alisema uamuzi wa kununua hisa hizo ni wa "roho ngumu" kwa sababu Tanzania ni eneo bichi kwenye sekta ya gesi.
"Mpaka sasa hakuna sheria rasmi iliyopitishwa kuhusiana na masuala ya gesi na hivyo Singapore inaingia katika eneo bichi kabisa katika sekta hii. Kumbuka pia kwamba gesi ya kwanza itaanza kuvunwa mwaka 2020 kutoka kwenye vitalu hivyo na utaona kwamba huu ni uamuzi mzito," alisema.
CHANZO: Raia Mwema - Waziri Muhongo anasa bil. 400/-
Efforts pay off:
Tanzania: Activists Want Barrick Taxed On Gains | PWYP [h=1]Tanzania: Activists Want Barrick Taxed On Gains[/h]
Source: All Africa
Date: 22 Aug 2012
STAKEHOLDERS have called for the government to hurriedly charge and collect Capital Gains Tax from the African Barrick Gold (ABG) following reports that its mother company, Barrick Gold, intends to sell off its stakes to a Chinese investor.
The move follows information reported by foreign and local media last week that ABG had resolved to sell its 74 per cent stake in the Africa Barrick Gold (ABG) to the Chinese state owned China National Gold (CNG).
Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA) through its Publish What You Pay (PWYP) coalition was bitter over the move and warned in a statement yesterday that the 20 per cent property gains tax should be collected before the company packs and leaves.
"We remind and urge the government to set a strategy that will ensure recovery of 20 per cent capital gains tax and corporate tax arrears from ABG simultaneous with CNG acquisition of ABG goldmines," the statement stated in part.
According to ForDIA Executive Director, Mr Buberwa Kaiza, it has already been confirmed that Barrick Gold and ABG executives have started negotiations with CNG which might culminate in the latter's total acquisition of the former.
He said PWYP-Tanzania Coalition is of the opinion that ABG preparations to exit the country is something to worry, as it relates to government's competence to enforce payment of 20 per cent capital gains tax.
The capital gains tax refers to gains from the disposal of Tanzanian assets by non-residents, which is charged at 20 per cent on the realized net gains.
"Secondly, PWYP-Tanzania is worried whether the government has learnt any lessons with regards to achieving the goal of free fiscal regime offers to foreign large scale mining companies," he said.
"It is perplexing and inconceivable for the government to offer free tax incentives to richer multinational corporations, bankrolling the multinationals to make profits and later exit at their will without paying significant taxes to the government," the ForDIA boss noted.
According to the statement, PWYP-Tanzania coalition considers tax incentives offered to foreign large scale mining companies unjustifiable and looks forward to see a competitively, transparently and accountably transacted ABG-CNG deal.
Reports have it that ABG is cross listed at the London and Dar es Salaam Stock Exchange Markets with the total value of 2 billion US dollars, but since Initial Public Offer (IPO) was launched in March 2010, ABG has only operated in Tanzania with investments in Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited and Pangea Minerals operating Tulawaka and Buzwagi goldmine projects.
The Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI) reports published in 2011 and 2012 exposed ABG's tax payment history, showing that ABG does not pay the 30 per cent corporate tax it is obliged to the government.
A statement quoting ABG Chief Executive Officer, Mr Greg Hawkins, early last year indicated ABG's net profit rose by 237 per cent during 2010 to 222.6 million US dollars (over 330bn/-) from 66 million US dollars in the previous year, meaning Tanzania would have received 66.78 million US dollars had ABG paid its 30 per cent corporate tax obligation.