Waziri mpya wa Nishati na Madini, Simbachawene ashikilia msimamo wa Prof. Muhongo

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
WAZIRI mpya wa Nishati na Madini, George Simbachawene, amesema ni vigumu kupata mwekezaji mzawa katika kazi za uchimbaji wa gesi, kwa kuwa kazi hiyo ni gharama kubwa duniani na kampuni za uchimbaji gesi hazizidi kumi.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, Simbachawene alisema kauli kwamba wazawa hawawezi kuwekeza katika gesi, iliyotolewa na aliyemtangulia, Profesa Sospeter Muhongo, haikueleweka vizuri.

Alifafanua kuwa Watanzania wanaweza kuwekeza katika nyanja ya utoaji huduma kwa wachimbaji wa gesi na kuongeza kuwa mpaka sasa kuna maeneo ya huduma ambayo Watanzania wangeweza kuwekeza, lakini hawajafanya hivyo.

“Kuhusu kutoa vitalu kwa Watanzania kila mtu angependa kupewa kitalu cha gesi. Ukipata kitalu ndio umeshatoka, hata mimi ningependa kupata kimoja halafu nikitoka nakwenda Huston (Marekani) na kukiuza na kutoka,” alisema.

Alisema la msingi ni kuhakikisha mikataba ya uchimbaji gesi, inanufaisha Watanzania wote na katika kutoa huduma kwa wachimbaji, atapigania Watanzania wapate fursa ya kuwekeza huko. Alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi na kuongeza kuwa lakini katika ushirikiano huo, lazima kuwepo na uwiano kati ya ushirikiano na maendeleo ya wananchi.

Kuhusu jukumu la kusambaa umeme, Simbachawene alisema atachukua Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuanza nayo, ili kuhakikisha mafanikio ya usambazaji umeme yaliyopatikana chini ya uongozi wa Profesa Muhongo, yanaendelezwa na hatimaye Watanzania wote wapate umeme.

Naye Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema anajua Watanzania wengi wanateseka kwa kunyang’anywa ardhi katika maeneo mbalimbali na hasa Dar es Salaam.

Amesema kwa kuwa amewahi kufanya kazi katika jiji la Dar es Salaam, ambako alikuwa Mkuu wa Mkoa, anajua hali ya unyanyasaji katika ardhi ilivyo na kuwataka Watanzania wenye matatizo na ardhi, kutoa taarifa ili wasaidiwe.

Lukuvi alikiri kukabiliwa na changamoto ya baadhi ya watendaji wasio waaminifu katika sekta hiyo na kuongeza atajitahidi kukabiliana na changamoto hiyo kwa uaminifu.
Chanzo:Habarileo.
 
Siasa za Tanzania zinalipa sana!

Malipo ya siasa za Tanzania mara nyingi huwa ni chanya kwa kiasi kikubwa kama utasimama kwenye msingi wa vyanzo vyake!.

Kuna baadhi ya wabunge kwenye suala la akaunti ya Tegeta Escrow inasemekana walilipwa ili kuhakikisha baadhi ya Mawaziri wa wanadondoka, wakati huo huo kuna wengine walilipwa ili kuwatetea!.

Malipo kwa Mzee Samwel Sitta yanatokana na kusimama kwake kidede kwenye msingi wa vyanzo vyake kuhusiana na suala la Katiba Inayopendekezwa ili kuhakikisha matakwa ya watalawa yanatimia. Matakwa ya watawala baada ya kutimia, amepata malipo yake kwa kupewa Wizara yenye ukaribu na wananchi ili atimize malengo yake, lakini vile vile ni wizara ambayo imewekwa na CCM na serikali yake katika kundi la wizara zenye miradi ya kimkakati katika mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano (2011/12-2015/16).

Haikushangaza hata pale Rais Kikwete alipompa sifa na kumuita Mzee Sitta mwanasiasa maalufu wakati wa sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 baada ya kile Rais Kikwete alichokiita kusisitiza ubora na kuendelea kwa Muungano wa Serikali Mbili alizoasisi Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Mzee Abeid Amani Karume kwenye Bunge Maalum.

Rais Kikwete alisikika akisema, '' Sijui tungesema nini katika Sherehe za mwaka huu kama ndiyo tungekuwa na Katiba Inayopendekezwa yenye muundo wa Serikali Tatu''.

Ikumbukwe pia, kwenye makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa, Rais Kikwete alisikika akisema, Kulikuwa na makundi ndani ya NEC na Kamati Kuu ya CCM ambapo kuna baadhi walifikia hata kumhoji chanzo cha ajenda ya kuandika Katiba Mpya kwa sababu haikuwa ajenda ya CCM. Kwa maana nyingine, Mzee Sitta amemsaidia sana Rais Kikwete kuzijibu hoja za wanaCCM ndiyo maana baada ya matokeo ya kura za Katiba Inayopendekezwa, Mzee Kingunge alisikika akisema, hakuwa na mategemeo makubwa kama kura zitatosha.

Hatuwezi pia kumsahau Mama Anne Kilango Malecela kwa kazi aliyoifanya bungeni wakati wa Bunge Maalum la Katiba ili kuhakikisha ushindi kwa watawala.

Kwa wale waliofuatilia mjadala wa suala la akaunti ya Tegeta Escrow watakumbuka jinsi ambavyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage walivyokuwa wakijenga hoja na kuitetea serikali. Kwa sasa wamekumbukwa wote na kupewa Wizara ambayo walikuwa wanaitetea katika mchakato wa Tegeta Escrow account.

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ameponzwa na mtandao uliokuwa unampiga vita katika kiti chake ambao kwa sasa umetamalaki mpaka kwenye Gazeti la Jamhuri lililoko chini ya Manyerere Jackton na Deodatus Balile.

Christopher Chiza, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, ameponzwa na kelele zilizokuwa zinapigwa sana na Kinana akishirikiana na Nape Nnauye katika ziara zao nchini kuhusu matatizo ya kilimo, chakula na Ushirika mpaka walimwita ni mmoja wa Mawaziri ambao ni mzigo kwa CCM na Serikali yake.

Kweli simba mwenda pole ndiyo mla nyama!.
 
Hii habari imekaa kiumbea, kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani. Sijaona mahali Simbachawene amesema hela za escrow ni za Singasinga na wala sijaona aliposema watanzania wawekeze kwenye juice na soda na wala Lionchawene hajafanya mipasho na mtu yoyote. Amesema anaanza kazi from the ground, ilani ya chama chake, excellent speech
 
Siasa za Tanzania zinalipa sana!

Malipo ya siasa za Tanzania mara nyingi huo ni chanya kwa kiasi kikubwa kama utasimama kwenye msingi wa vyanzo vyake!.

Wewe piga majungu ukichoka utakwenda kutafuta riziki ya watoto wako.
 
Hawachoki majungu , ndiyo mtaji wao kuelekea Oktoba waache wambeeshe wakichoka watanyamaza .
 
Lukuvi chanzo cha migogoro ya ardhi dodoma.halafu anapewa wizara ya ardhi.
Mmh, Kama hiyo ndiyo hoja, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alifanya nini ili kupambana na migogoro hiyo?.
 
Ng'wamapalala, mara zote nimekuwa naheshimu sana michango yako hapa JF. Ni vema wakati mwingine kama unataka ufafanuzi, omba usaidiwe badala ya kuibuka tu la tuhuma. Sisi hatujamwandama Mwakyembe. Tumemwandana Kipande wa TPA. Tumeandika mengi kuhusu TPA na namna walivyokuwa waingie mkataba wa kuuza ufukwe wote wa Bandari. Tuliandika tukiamini Watanzania wa aina yako wataelewa, na kulaani ufisadi wa kutisha Bandari. Mwakyembe si mlengwa mkuu kwenye sakata hili, isipokuwa mhusika ni Kipande. Maajabu yaliyofanywa na Rais Kikwete ni kumwondoa Mwakyembe na kumwacha mhusika mkuu, Kipande. Rejea ripoti ya CAG kuhusu TPA uone maajabu! Mwisho, niseme kama ni udhaifu wa uongozi, tunaye Rais ambaye ni dhaifu kuliko marais wote katika ukanda huu wa Afrika Mashariki nas Kati. Mnyika aliposema, hatukumwelewa, lakini sasa wengi wetu tunaliona hilo.
 
Hawachoki majungu , ndiyo mtaji wao kuelekea Oktoba waache wambeeshe wakichoka watanyamaza .

Shembe mwana zeduze we. Sie tunafurahia jinsi serikali inavyoangushwa na ccm yenyewe hivyo 2015 ni kumalizia tu
 
Siasa za Tanzania zinalipa sana!

Malipo ya siasa za Tanzania mara nyingi huo ni chanya kwa kiasi kikubwa kama utasimama kwenye msingi wa vyanzo vyake!.

Kuna baadhi ya wabunge kwenye suala la akaunti ya Tegeta Escrow inasemekana walilipwa ili kuhakikisha baadhi ya Mawaziri wa wanadondoka, wakati huo huo kuna wengine walilipwa ili kuwatetea!.

Malipo kwa Mzee Samwel Sitta yanatokana na kusimama kwake kidede kwenye msingi wa vyanzo vyake kuhusiana na suala la Katiba Inayopendekezwa ili kuhakikisha matakwa ya watalawa yanatimia. Matakwa ya watawala baada ya kutimia, amepata malipo yake kwa kupewa Wizara yenye ukaribu na wananchi ili atimize malengo yake, lakini vile vile ni wizara ambayo imewekwa na CCM na serikali yake katika kundi la wizara zenye miradi ya kimkakati katika mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano (2011/12-2015/16).

Haikushangaza hata pale Rais Kikwete alipompa sifa na kumuita Mzee Sitta mwanasiasa maalufu wakati wa sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2014 baada ya kile Rais Kikwete alichokiita kusisitiza ubora na kuendelea kwa Muungano wa Serikali Mbili alizoasisi Mwalimu Julius Nyerere akiwa na Mzee Abeid Amani Karume kwenye Bunge Maalum.

Rais Kikwete alisikika akisema, ‘’ Sijui tungesema nini katika Sherehe za mwaka huu kama ndiyo tungekuwa na Katiba Inayopendekezwa yenye muundo wa Serikali Tatu’’.

Ikumbukwe pia, kwenye makabidhiano ya Katiba Inayopendekezwa, Rais Kikwete alisikika akisema, Kulikuwa na makundi ndani ya NEC na Kamati Kuu ya CCM ambapo kuna baadhi walifikia hata kumhoji chanzo cha ajenda ya kuandika Katiba Mpya kwa sababu haikuwa ajenda ya CCM. Kwa maana nyingine, Mzee Sitta amemsaidia sana Rais Kikwete kuzijibu hoja za wanaCCM ndiyo maana baada ya matokeo ya kura za Katiba Inayopendekezwa, Mzee Kingunge alisikika akisema, hakuwa na mategemeo makubwa kama kura zitatosha.

Hatuwezi pia kumsahau Mama Anne Kilango Malecela kwa kazi aliyoifanya bungeni wakati wa Bunge Maalum la Katiba ili kuhakikisha ushindi kwa watawala.

Kwa wale waliofuatilia mjadala wa suala la akaunti ya Tegeta Escrow watakumbuka jinsi ambavyo aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage walivyokuwa wakijenga hoja na kuitetea serikali. Kwa sasa wamekumbukwa wote na kupewa Wizara ambayo walikuwa wanaitetea katika mchakato wa Tegeta Escrow account.

Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ameponzwa na mtandao uliokuwa unampiga vita katika kiti chake ambao kwa sasa umetamalaki mpaka kwenye Gazeti la Jamhuri lililoko chini ya Manyerere Jackton na Deodatus Balile.

Christopher Chiza, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, ameponzwa na kelele zilizokuwa zinapigwa sana na Kinana akishirikiana na Nape Nnauye katika ziara zao nchini kuhusu matatizo ya kilimo, chakula na Ushirika mpaka walimwita ni mmoja wa Mawaziri ambao ni mzigo kwa CCM na Serikali yake.

Kweli simba mwenda pole ndiyo mla nyama!.

Mkuu naona unajenga hoja kwa misingi kwamba wizara fulani ni nzuri kuliko nyingine kwa kigezo cha fursa za wizi zilizopo. Sikuelewi unaposema Mwakyembe na Chiza "wameponzwa" na huku ukidai Sitta amelipwa fadhila wakati wote bado ni mawaziri kamili hakuna aliyeshushwa cheo na presumably mshahara wa mawaziri unafanana. Nilichoona hapo ni wizara zenye mianya mingi ya wizi wewe umeziona kama promotion kwa kuwa huko kwenu CCM hamfanyi kazi kwa lengo la kuwatumikia wananchi bali ni wizi na maslahi binafsi, no wonder mnaona wizara moja ni bora kuliko nyingine wakati mshahara ni ule ule
 
Hii habari imekaa kiumbea, kichwa cha habari na habari yenyewe haviendani. Sijaona mahali Simbachawene amesema hela za escrow ni za Singasinga na wala sijaona aliposema watanzania wawekeze kwenye juice na soda na wala Lionchawene hajafanya mipasho na mtu yoyote. Amesema anaanza kazi from the ground, ilani ya chama chake, excellent speech
Mkuu,

Gazeti halijasema misimamo ya Prof. Muhongo bali limesema msimamo wa Prof. Muhongo.

Huo ndiyo msimamo wake katika uwekezaji wa gesi ambao unaendana na msimamo wa Prof. Muhongo.
 
Wewe piga majungu ukichoka utakwenda kutafuta riziki ya watoto wako.
Mkuu,

Yale unayofikiria ni majungu kuna wengine wanafikiria katika mtazamo mwingine, kwa maana kuwa, kusema majungu haina maana kuwa ni majungu kama hujaweka hoja za kuubeba mtazamo wako.

Mambo ya riziki za watoto wala yasikupe shida katika mjadala huu kwa sababu ninaamini hufahamu hata kama nina watoto au sina watoto.
 
Back
Top Bottom