Arnold Kalikawe
Senior Member
- Sep 28, 2016
- 147
- 341
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson amejiunga na kituo cha televisheni cha ‘GB News’ kilichopo jijini London, Uingereza.
BBC imeripoti kuwa Johnson, ambaye alijiuzulu ubunge mapema mwaka huu, atafanya kazi katika kituo hicho cha habari kama mtangazaji, mtayarishaji wa vipindi na mtoa maoni.
"Atakuwa na jukumu muhimu" katika matangazo ya uchaguzi wa Uingereza na Marekani mwaka ujao na ataangazia masuala tofauti "kuonyesha nguvu ya Uingereza duniani kote," shirika hilo la utangazaji lilisema.
Aliahidi kushiriki "maoni yake ambayo hayajabadilika" kuhusu mada tofauti.
Johnson ni mwanasiasa wa hivi karibuni kutoka Chama cha Conservative kujiunga na shirika hilo la utangazaji, baada ya aliyekuwa Katibu wa Biashara Jacob Rees-Mogg, Naibu mwenyekiti wa chama Lee Anderson, na wabunge Esther McVey na Philip Davies.
Katika video iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza amesema: "Ninafurahi kusema kwamba hivi karibuni nitajiunga nawe kwenye GB News.”
Hata hivyo Boris Johnson si mgeni katika taaluma ya habari kwani 1989, aliajiliwa kama mwandishi wa Brussels, baadaye akawa mwandishi wa safu ya kisiasa kwenye gazeti la ‘The Daily Telegraph,’ kabla ya kupanda daraja na kuwa Mhariri wa 'The Spectator' toka mwaka 1999 hadi 2005.