Waziri Mkuu wa Canada azomewa msikitini, aambiwa "huna haya"!

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,648
3,938
Hali inazidi kuwa mbaya kwa wafuasi wa iblis

Wakati wa ziara yake ya kutembelea msikiti mjini Toronto, Waziri Mkuu wa Canada amezomewa na hadhirina kotokana na msimamo wake kuhusu mauajii yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza huko Palestina ambako amepatwa na tahayuri asijue la kufanya.

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, akikabiliana na umati wa watu waliokuwa wakimzomea, huku baadhi ya waliohudhuria msikitini wakitoa nara: "aibu juu yako". Waandamanaji hao Wamewataka waandaaji wa mkutano huo wasimruhusu Justin Trudeau kuzungumza.

Pia, wakati Trudeau anatoka kwenye jengo la msikiti, alikumbana na waandamanaji waliokuwa na mabango yenye maandishi yanayowaunga mkono watu wa Palestina.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada ilitangaza baada ya tukio hilo kwamba: Trudeau alikuwa msikitini hapo kuhudhuria programu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu ya Toronto ili eti kuonyesha uungaji mkono wake kwa jamii ya Waislamu ambao wameathiriwa na matukio ya kutisha katika Mashariki ya Kati. Waandamanaji waliokuwa eneo hilo wameitambua ziara hiyo ya Waziri Mkuu wa Canada eneo la msikiti wa Waislamu mjini Toronto kuwa ni unafiki na kukosa haya, hasa baada ya kutangaza uungano mkono wake kwa mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, kama viongozi wengine wengi wa nchi za Magharibi, amewakasirisha Waislamu wa Canada na maeneo mengine ya dunia kwa kusema kuwa, Ottawa inaunga mkono haki ya Israeli ya kujilinda, wakati huu ambapo utawala huo ghasibu ukiendelea kuua raia wasio na hatia wa Gaza. Waziri Mkuu wa Canada ametoa matamshi hayo huko Israel ikiwa tayari imeua raia zaidi ya elfu nne wa Gaza.
 
Hao raia nao waache unafiki, wanafanya nini huko Canada si warejee kwenye nchi zao hizo hizo zinazounga mkono ugaidi.

Wamekimbia kutoka kwenye mataifa yao yasiyo na uhuru na kwenda kwenye nchi ambayo unaruhusiwa kumpinga hadharani kiongozi mkuu wa serikali. Huyo waziri mkuu ana kosa gani wakati huo ndio msimamo wa nchi yake. Wanafiki wakubwa hao.
 
Hao raia nao waache unafiki, wanafanya nini huko Canada si warejee kwenye nchi zao hizo hizo zinazounga mkono ugaidi.

Wamekimbia kutoka kwenye mataifa yao yasiyo na uhuru na kwenda kwenye nchi ambayo unaruhusiwa kumpinga hadharani kiongozi mkuu wa serikali. Huyo waziri mkuu ana kosa gani wakati huo ndio msimamo wa nchi yake. Wanafiki wakubwa hao.
wewe ndio mnafiki na roho mbaya juu, na fanya hima ujirekebishe kabla mauti hayajakukuta
 
Ingekua ndio hapa kwetu, sipati picha namna raia wangekula virungu na kutiwa korokoroni, na juma tatu wangefikishwa kwa pilato na kusomewa mashtaka....😜
 
wewe ndio mnafiki na roho mbaya juu, na fanya hima ujirekebishe kabla mauti hayajakukuta
Nenda Saudis Arabia, Iran, Oman uandamane eti unampinga rais au mwana mfalme uone kitakachokupata. Pia nashangaa watu middle East kukimbilia mataifa ya Ulaya ambayo yana mila ambazo ni kinyume na uislam.
 
Back
Top Bottom