Waziri Mkuu Tanzania - Mtu wa sita kwa hadhi nyuma ya wazanzibari wanne

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Siku ya jana kulifanyika ibada kubwa pale Zanzibar, na viongozi wakuu wa kitaifa walikuwepo. Nilishangazwa kwa jinsi protokali ya nchi hii ilivyomuweka Pinda nyuma ya JK, Bilal, Shein, Hamad na Idd. Kama ni waziri mkuu wa serikali ya muungano, basi hata rais wa Zanzibar anapaswa kuwa chini yake kwa maana Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

Hii imenifanya nimwone PM kama kiranja wa 'Bara'. Mtu wa sita kwa hadhi Tanzania atasema nini Zanzibar ilhali juu yake kuna wazanzibari wanne? Najua katiba za Zanzibar ilifanyiwa marekebisho kwa kupeana vyeo lukuki, lakini ni lini katiba yetu imerekebishwa na kumshusha hadhi PM kwa kiasi hiki. Kwangu mimi jaji mkuu chande hata mama Makinda wana hadhi kubwa zaidi ya rais wa Zanzibar kwa sababu wanaweza kurithi urais wa Tanzania.

kuna baadhi ya wachangiaji wanahoji ati thread hii inasaidia nini kupunguza umaskini Tz........

Watu wenye hadhi ya juu ndio wenye ushawishi wa maamuzi yote. Ndio maana mataifa makubwa huya yanahangaika kutafuta "who are the most influencial" na hao ndio waamuzi wa mambo ya dunia likiwemo hilo la umaskini. Kuwa na "top layer" ya wazanzibari wanne ni kuweka mustakabali wa nchi yetu kwenye mikono yao, sawa na kuweka rehani 'utajiri' wetu kwa minajili ya kukubaliana kisiasa. "Our progress depends much on who rules and what shall happen if we are ruled by zanzibaris?
 
Haya ya protokali hiki ni kizaazaa kingine?Uhu nao utata mwingine ambao ndio maana hatimae ya yote jibu la haya yote ni katiba mpya.
 
Mimi kinachonitesa, siyo nani yuko juu ya nanai.

Ila nchi kma yetu kuwa na viongozi wa juu sita!!!

Sijui lakini namjua rais na makamu wake kule US, Namjua Waziri Mkuu wa UK, namjua Chancelor wa Ujerumani peke yake!! Sasa sisi....

Marais wawili, Makamu wa rais watatu, Waziri Mkuu .....

It is too much.

matokeo yake hata hao watu wa protokali wanashindwa kupanga who is on top of who!!
 
Si yeye ndio alisema zanzibar siyo nchi...ameonyeshwa wenye nchi yao ni kina nani? ok...

Hilo li-pinda nalo PM au mzigo..ni mzito kiakili na hata kikaazi...kweli anafaa awe analima tu tena muhogo..maana mahindi hawezi kupalilia alivyo lazy..
 
Katiba ya TZ hawatambui makam wawili wa Zenji inamjua waziri kiongozi so hata wao wakija huku hawajulikana kazi zao wala hawana viti vya kukalia..Ila sijui kama hili nalo ni issue katika msiba tulioupata.. Protocol ziko na zitandelea kuwepo cha msingi tuwasaidie jamaa wa 1st class waliko kwenye MV Spice mpaka sahv hakuna hata mmoja aliyetoka!
 
Watu kama Tundu Lissu wenye muono wa mbali wakitahadharisha juu ya athari za baadaye endapo "vijitatizo" kama hivi havitatafutiwa dawa mapema wanaishia kuzomewa na kuzodolewa Bungeni na hao ambao mwisho wao wa kuona ni usawa wa pua zao.

Frankly speaking, hili la Muungano wa Tn na Zn lisipotafutiwa dawa ya kudumu, regardless itakuwa chungu namna gani, ni bomu baya kuliko hatari nyingine yoyote itakayoukabili ukanda huu wa Afrika Mashariki muda si mrefu ujao. Bomu hili lina sura zote chafu na za hatari zaidi kwa wakati huu - UTAIFA (sisi, wao; chetu chetu, chao chetu), UDINI (dini yetu tuko wengi, dini, dini, dini, ...), na UGAIDI. Inahitajika busara, umakini, na uthubutu wa hali ya juu kukabiliana na dude hili liitwalo muungano.
 
Kama katiba ya TZ haiwatambui makam wa rais wawili, Juzi Seif Sharif Hamad alifungua majengo Tanzania bara kama nani?
 
Tundu lissu ni sehemu ya tatizo..anatumiwa na wanajumuia
 
Kama katiba ya TZ haiwatambui makam wa rais wawili, Juzi Seif Sharif Hamad alifungua majengo Tanzania bara kama nani?

Kwani Ibara gani ya Katiba ya Muungano inataambuwa hicho cheo cha Maalimu?

Kufungua miradi hata wewe unaweza kama ukialikwa na hipo pia inayofunguliwa na mbio za mwenge, Mabalozi wa nchni za nje, na wageni mbali mbali wanao tutembelea, hata ile inayofunguliwa na watu kama Mama Clinton! Hao sidhani kama ni viongozi wa Kitaifa.
 
Mwenzenu niliachwa hoi na kitu kingine kabisaaaaaaaaaaaaaaa!
.....................ALHAJI DOKTA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE! Halafu wakafululiza ma-alhaji kadhaa kabla ya Mzee wa kulialia!!
 
Wengine tunasema kila siku kuwa muungano ni mtaji wa Nyerere na mwenzie Karume ambao pengine ulikuwa unalipa enzi hizo. Hatuwezi leo kuendelea na dhana ambayo imepitwa na wakati. Watanganyika tudai Tanganyika yetu kamili na tukatae hii dini ya Unyerere ambayo imejaza raia uoga na kujaza unafiki kwenye serikali.
Sijui watu wanaong'ang'ania kuungana na hao Wazanzibari wanatafuta nini. Mtanganyika ukiwa kule ni bugudha na adha mtindo mmoja sawa na foreigner lakini huku kwetu wao wako raha mustarehe.
Tunahitaji muelekeo mwingine haraka ili tubaki kivyetu na wao kivyao kama ilivyokuwa kabla ya 1964.
 
Mimi kinachonitesa, siyo nani yuko juu ya nanai.

Ila nchi kma yetu kuwa na viongozi wa juu sita!!!

Sijui lakini namjua rais na makamu wake kule US, Namjua Waziri Mkuu wa UK, namjua Chancelor wa Ujerumani peke yake!! Sasa sisi....

Marais wawili, Makamu wa rais watatu, Waziri Mkuu .....

It is too much.

matokeo yake hata hao watu wa protokali wanashindwa kupanga who is on top of who!!
Duuuuh imebidi nincheke kuna ukweli ....hahahahaha
 
Tanzania tuna protocali 2. Ya JMT na ya ZNZ. Protocal ya JMT on top ni
1. President
2. VC
3.PM
4. Spk
5. CJ
Note kwenye protocal yetu, rais wa ZnZ na makamo wake wawili are all nobody in TZ ila wakija wanapewa heshima tuu.

Vivyo hivyo protocal ya ZnZ ni
1. Rais wa ZnZ na M/K wa BLM
2. 1st VC (boya with no executive
powers and nothing to do)
3. 2nd VC ambaye ni CM
4. Spika wa BLW
5. CJ wa ZnZ
Jk, Pm wetu na viongozi wowote wa bara are nothing in Zanzibar bali heshima tuu.

Haya ni baadhi tuu ya mapungufu kwenye structure ya muungano. Haya na mengine mengi yatakuwa taken care kwenye katiba mpya itakayoanza kutumika 2016 baada ya CCM kuitumia iliyopo kurudi madarakani 2015!.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom