Waziri Mkuu tafadhali ongeza tu na Vyuo katika Orodha yako

Lugumgya

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
629
1,997
Naipongeza Serikali kwa jitihada na hatua walizo chukua kama sehemu ya tahadhari ya kujikinga na kupunguza kusambaa kwa ugonjwa wa Corona. Waziri Mkuu umesikika ukitaja shule za msingi na Sekondari kufungwa kwa siku 30 na baada ya hapo serikali itatoa tena tamko. Ni sawa kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Tamko lako hilo Mh: Waziri Mkuu, lilenge pia na vyuo kwani pia ni sehemu ya mkusanyiko. Labda hamkugusa vyuo kwa kuwa mnahisi ni watu wazima hivyo watakuwa na hadhari zaidi kuliko wa ngazi za chini? Sijui! Lakini naiona hatari kubwa vyuoni pengine kuliko ngazi ya sekondari na msingi kwa sababu zifuatazo;

1. Vyuo vyetu vinahusisha Wanafunzi wengi wa kigeni ambao kama taifa hamjawazuia kuingia, watakuja watafika KIA wataonekana hawana, tutafanya nao discussion baada ya wiki hali yao itabadilika sampuli ikipelekwa DAR watakutwa na visa tayari.

Kwanye hizo discussion na Wageni watahusika watu wenye familia, ambao wakirudi nyumbani watavipeleka nyumbani, ndo hivo ugonjwa utaendelea kusambaa kwa Kasi. Mfano, Chuo kama UDOM kina Wanafunzi zaidi ya 20,000 (Sina takwimu sahihi), UDSM unaweza kuta 9,000-12,000, SAUT Mwanza, Vyuo vya Kati nk. Fungeni kwanza ndugu zangu, tusije tukachuma janga!

2. Vyuoni ndo ku-hug na kubusiana hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo vilikuwa vimefungwa ni balaa. Hivyo wanafungua wakiwa wamekumbukana (kumisiana) hivyo, itakuwa full waaoooooooo, full mwaaaaaaaaaaa! Nachukua experience kutoka kwenye mpira, wanasema wasishikane mikono, lkn mechi ikiisha, wanashikana! Goli likiingia wanakumbatiana! Furaha wakati mwingine inatusaulisha! Tunaomba mtunusuru kwa maamzi yenu.

TAHADHARI NYINGINE MAOFISINI

Kunawa sawa, lkn Kama mjuavyo hatujazoea na naamini tutajishau! Hivyo ofisini wasambaze gloves! Hii ni kutokana na ukweli kwamba, mtu aliyeambukizwa Virus anaweza kushika file na anapolisukuma kwa mtu mwingine, huyu wa pili nae akajikuta anakontaminate hiyo Corona( Sina uhakika na njia hii ya Usambazaji) lkn nafikir inaweza kutokea


USHAURI

1. Fungeni Vyuo

2. Waziri Mkuu, nakuombeni zile fedha za Mwenge japo mnunue vifaa vya kupima Corona, mviweke katika zone maana hii ya kutegemea Dar tu inatia shaka kidogo. Kama hazitoshi, ile ndege ya tisa isubiri, maana tunanunua cash, hiyo cash inunue vifaa tiba. Tusije tukanunua ndege ambayo haitoweza kubeba hata maiti au ikabeba watu wa mataifa yaliyochokua tahadhari wakati huku sisi mishumaa na RIP zikiwa zimetawala.


Naamini utaliona hili kwa jicho lingine ili Vyuo navyo visiruhusiwe kuanza au kuendelea na masomo.

Naomba Kuwasilisha!

Lugumya.
IMG-20200317-WA0023.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani una akili kuliko serikali yenye nyenzo zote za kupata taarifa na maelezo yote kuhusu corona?

Hebu utulie huko! Usitake kuleta taharuki zisizo na sababu!
 
Hao wageni wawekwe karantini kwa siku 14 kama inavyofanyika katika nchi zingine. Kisha waungane na wenzao kupiga msuli.

~I moved your cheese! So what?~
 
Sioni haha ya kufunga vyuo kwasasa,hata shule za boarding ,hatari ilikua kea Hawa wadogo wanaoenda na kurudi homu,Hapa katikati usafiri Ni tatizo,
Hawa wa boarding kuanzia kesho Bora shule ziwatoe kea awamu maana itakua mafuriko stand na ndio Hapo shida ilipo
 
Ni sawa. Kumbuka hata hao wa vyuoni hawakai hostel wote
Sioni haha ya kufunga vyuo kwasasa,hata shule za boarding ,hatari ilikua kea Hawa wadogo wanaoenda na kurudi homu,Hapa katikati usafiri Ni tatizo,
Hawa wa boarding kuanzia kesho Bora shule ziwatoe kea awamu maana itakua mafuriko stand na ndio Hapo shida ilipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MHESHIMIWA Waziri Mkuu toa maelekezo kwenye vyombo vya habari vyote siyo tbc tu.

Nasema hivyo kwa sababu hapa dar kesho watoto WATAENDA shuleni ni wa shule za Msingi.
 
Ni sawa. Kumbuka hata hao wa vyuoni hawakai hostel wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure,as long as Ni watu wazima,wakichukua tahadhari Ni sawa tu,kwani wakirudi home SI watakua mtaani?,kwahiyo Ni yale Yale tu,tofauti na watoto wao hawajui kitu,wanacheza,wanapigana mieleka etc,Hawa ndo lazima kubaki home chini ya uangalizi
 
Back
Top Bottom