Waziri Mkuu: Sukari haitakuwa tatizo Ramadhani

Hili tatizo la sukari halikuwepo kabisa lakini kutokana na papara zao wakalileta na sasa wanashindwa kulimaliza. Bora wanyamaze kabisa tujihangaikie wenyewe maana hakuna nafuu yoyote kutoka katika matamko yao zaidi ya kututia hasira.
Mwendokasi kesha sema mnaoishi kama malaika ni wakati wa kuishi kama shetani
 
Hivi Sukari kwanini Inauzwa 3000 kama ipo kidogo Mbona haiiishi,haka ni ka mchezo tunachezewa.Nilitegemea wangeuza kwa 1800 au 2000 then kwa vile ipo kidogo basi ingeisha na wote tungekosa sukari Sasa sukari ipo tu ba bei ndo juu nini lengo la kupandisha bei?
 
Kabadili tena sio 1800 ni 2300

Hata mimi nashindwa kuelewa!!! Authority ya Serikali yetu inakuwa undermined na watu wachache au nini? Viongozi wetu wanapashwa kuwa na msimamo at all times.

Kama wanesema bei ni TSh.1800 basi wa stick to their guns, haya mambo ya kuonekana wako wobbly ni as if wana dance to the tune ya wafanya biashara hizi si dalili nzuri hata kidogo - Dk.Magufuli awe macho sana na baadhi ya wasaidizi wake they don't seem to run in sync na determination/maelekezo yake, now you begin to wonder nani ana-import sukari nchini, je, Serikali imewapa tena vibari wafanya biashara wale wale kuingiza Sukari na kufanya wapendalo mpaka wananchi kulazimika kununua kilo moja TSh.3500 -5000!! - kama hii ni kweli basi Dk.Magufuli a form an independent probe team ya watu wenye maadili wachunguze kinacho endelea nyuma ya pazia, wote watakao bainika ku undermine Authority ya Dk.Magufuli wachukuliwe hatua ya uhujumu uchumi nyadhifa zao notwithstanding - there's something seriously wrong downthe line - honestly.

Kwa nini viwanda vya sukari havikupewa jukumu la ku import sukari ya ku fill gap iliyopo - wenye viwanda hawawezi kufanya hujuma/ujanja wa kuflood market na cheap import, kupandisha bei ovyo ovyo au kukwepa kodi, kama viwanda havina fedha za kuimport (which I doubt) wangeweza kupewa mikopo na mifuko ya hifadhi ya jamii kuitikia a brilliant idea iliyo pendekezwa na Rais Magufuli naona hilo halikufanyika /lilipuuziwa badala yake Serikali inaonekana inaedelea ku reinvent the wheel kwa kurudia makosa yale yale ya kushirikiana na watu wale wale wa kuimport sukari - what do you expect at the end of the day, Taifa linajikuta bei ya sukari inapanda holela na kumuweka JPJM wa watu katika wakati mgumu kwa wananchi.

Binafsi naona tatizo hili la sukari na jinsi lilivyo shughulikiwa na keyplayers wa sekta ya sukari nchini kuanzia:Wizara ya Kilimo, Sugar Board of Tanzania, Wizara ya viwanda na Biashara na Ofisi ya Waziri Mkuu nk kuna baadhi ya sekta hizo tajwa zilikuwa so passive/awasemikitu mtu ungefikiri tatizo la Sukari haliwahusu kabisa - msukumo ulikuwa mdogo sana!!

Sina shaka tatizo hili la sukari nchini ni mtihani tosha kwa Dk.Magufuli kuwa wapima upya baadhi ya watu waliopo mawizarani na mashirika ya umna yanayo husu Sugar Industry chini achunguze kama kweli wapo pale 4 interest za Taifa letu na je, wanamsaidia kwa nia njema au la - hayo ndio maoni yangu nayasema kwa nia njema.
 
Hii ndiyo Magufuli for Change yaani anytime kuna mabadiliko. 1800, 2000, 4000, 6000, 2800, 3000,3500, 2300 yaani anytime changes
 
Uzuri Watanzania hatuna maneno. Sukari ilikuwa 2000 kabla ya maelekezo. Sasa ni 3500 na kuendelea wala hatuna neno. Tutanunua tu, tukishindwa tunapiga kimya au kulalamika huku mtaani kwetu.
 
Yaani uku kwetu sukari 3600 sasa hao wakuu wa mikoa walio agizwa wanaidhibiti vipi...? Mi naona ifike mahali siasa itenganishwe na professional issues maana hili ni swala raisi tu tulisoma darasani demand vs supply Wachumi wangeishauei serekali wanasiasa wakae kimya tu
 
Ukifuata bei elekezi familia itakosa chai bure ngoja mimi ninunue kwa bei atakayokuwa anauza muuzaji maana mwanangu Jesca ananiambia kila tukosapo sukari "baaaba leo mama hajanipa chai kanipa uji wa moto tu"
 
Hahaha ni bora mi nakunywa tu supu,mara ya mwisho kununua sukari ilikuwa 1kg tsh 1,000/=
Dah Me Pia Mwana last time kununua Sukari ilikuwa inauzwa 450 kwa kg 1 na baadae ikaadimika na iliporejea ikapanda ikafika 500 kwa 1kg Haya Majanga yapo tokea kitambo si mapya ila Magu alichemka baada ya kusikia minong'ono ya wenye Viwanda badala ya kukaa chini kwanza... na hili sakata nadhani Raisi katia Akili no more kusikiliza watu na kutake action maanahadi mchele ulishapigwa Stop... tungekula Ugali hadi tungekoma
 
Hawa viongozi wakati mwingine bora wakae kimya la sivyo watatutafutia vifungo maana kilo moja ya sukari ziwezi kumiliki seuze fine milioni saba?wacha ramadhani yangu iende kichumvichumvi tu maana hamna namna!
 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300.

Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha Mipango mjini hapa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.

Pia alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000 zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.

Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.

“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema.

“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”

Alisema suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo.

Katika miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini, imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka nje ili kukabili upungufu uliopo.
Thabit Kombo alisema -"Tuwe tunaweka akiba ya Maneno". ..
Majaliwa alitakiwa atuambie mbona Mwendokasi imechange gear toka 1800 mpaka 2300 kwanza , maana imezua maswali yasiyojibika
 


Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa salamu za Ramadhani kwa waisilamu na uzungumzia suala la vyakula kupanda bei na uhaba wa sukari
Amesema kuna wafanyabiashara wanaopandisha bei ya vyakula kwa makusudi kwa kuwa wanaona waisilamu wanahitaji chakula kingi kipindi hiki. Amekemea tabia hiyo na kusema kama serikali watasimamia bei ya chakula kuhakikisha hawapandishi ovyo na kuwachukulia hatua.

Akizungumzia suala la sukari amesema mahitaji ya sukari ni makubwa sasa hivi kwa kuwa yanatumika kwenye vyakula, amesema bidhaa hiyo inapatikana kwa uchache lakini wanajitahidi kuendelea kusambaza kanda zote na amewataka wafanyabiashara kuiuza kwa bei ya kawaida
 
Kingunge alisema wameishiwa pumzi ya kuongoza....hapo wanasumbuliwa na kuteswa na chai ya asubuhi,bado wananchi hawajala lunch wala dina,halafu eti wanasema wana hela ya ndege na meli
 
Back
Top Bottom