Wasaidizi wawili wa karibu wa Kikwete, Waziri Mkuu na Makamu wa Raisi walijitokeza kuwania kuchukua nafasi ya bosi wao, lakini wote walikatwa kwa sababu walionekana kuwa hawana maadili.
Jambo hili linashangaza sana, kwamba waziri mkuu amedumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 8 na makamu wa raisi amedumu kwenye nasafi hiyo kwa miaka mitano, kumbe kipindi chote hicho taifa limekuwa likiongozwa na watu wasiokuwa na maadili, licha ya kuwa raisi kwa kipindi cha jumla ya zaidi ya miaka 3 amekuwa hayupo nchini na nchi imekuwa chini ya uongozi wa hao wasaidizi wake. Leo anawachijia baharini, kisa hawana maadili.
Leo hii unataka waziri mkuu asiyekuwa na maadili aingie ofisini kufanya nini?
Hali hii ni udhibitisho na uhakika kuwa kwa kipindi cha miaka 10 taifa la Tanzania limeongozwa na watu wasiokuwa na maadili.