Waziri Mkuu Pinda kasusa ofisi

Waziri Mkuu Pinda kasusa ofisi

Mara baada ya mkutano mkuu wa ccm uliofanyika dodoma, waziri mkuu hayupo ofisini, kuna tetesi toka kwa watendaji wa ofisi ya waziri mkuu wakidai kuwa mh. Pinda amesusa ofisi kutokana na kukatwa jina lake katika harakati za kugombea kuteuliwa kuwa mgombea wa ccm.

kweli wonders shall never end! yaan aliamini kabisa atasimamishwa yeye......! doh!
 
Baada ya kukatwa na "Kitengo" kuashiria kuwa hana maadili unadhani atakuwa na moral authority ya kiutendaji tena kweli! Yaani kwa maadili kapitwa na naibu waziri Makamba halafu atamwongozaje? Mungu atuepushe lisitokee la kutokea linalohitaji maamuzi mazito ya pamoja kwani kwa sasa ombwe ni kubwa kuliko wakati wowote!

Hilo neno, makamba atakuwa na uwezo wa kumtunishia kifua pinda
 
Ni sawa na kufanya mtihani arafu Mwalimu hata hasaishi anaweka tu zero. Inawauma sana kina P and the like.
 
Ni suala la muda na muda umefika, CCM inabidi wapumzike hawana hati miliki ya hii nchi..na haya yote n kutokana na uongozi mbovu WA chama..kuendekeza undugu na kuacha maadili ya chama. Kwa sasa hakuna WA kumwamin ndan ya chama.mamluki wengi kuliko wanachama hai..ni matunda ya mbegu waliyoipanda hivyo wasishangae...tunawaomba wakabidhi upinzani nchi kwa amani
 
Kukatwa kunauma sana. Wengi waliokatwa wamekuwa kimya sana akiwemo Membe.
 
mkuu nimepata abari kuwa membe pia kasusa, nakasema kamgaya kikete na ataki kucheza nae, pia hato mgawia ice cream akinunua...


Ila hajasikika sana popote tangu kikao kile katuni walimdondosha kwenye bench wakati wenzake watano wakishangilia na karatasi za tick. Siasa mbaya sana.
 
huyu huku analisha ng'ombe wake

attachment.php
 
Ila hajasikika sana popote tangu kikao kile katuni walimdondosha kwenye bench wakati wenzake watano wakishangilia na karatasi za tick. Siasa mbaya sana.

ha ha haaa alizimia kabisa!
 

Attachments

  • 1438710061777.jpg
    1438710061777.jpg
    12.9 KB · Views: 1,194
Mara baada ya mkutano mkuu wa ccm uliofanyika dodoma, waziri mkuu hayupo ofisini, kuna tetesi toka kwa watendaji wa ofisi ya waziri mkuu wakidai kuwa mh. Pinda amesusa ofisi kutokana na kukatwa jina lake katika harakati za kugombea kuteuliwa kuwa mgombea wa ccm.

Ametumia busara kuachia ngazi kwani chombo cha maadili cha CCM kimemkuta na hatia ya kutokuwa na maadili, na Dr. Magufuli ambaye walipishana kauli kwenye public juu ya kuvunja Millennium towers na Tanesco Ubungo kubainaka na maadili tele.
 
Makamu rais,mzee Wa kuweka mawe ya msingi,eti naye kasusa. Mawaziri nao wanaondoka kufuata safari ya matumaini. J K kazidiwa. Teh!teh!usishangae akiunda baraza jipya la mawaziri!!
 
Jaribuni kuwa makini muone wanaokibeba chama sasa hivi ni watu wengine kabisa hatukuliona hili kwakuwa ishu za CHADEMA zilituteka kabisa lakini kiukweli huko ccm mambo ni mabaya mara mia kuliko CHADEMA
Kwkuwa sasa mambo ya CHADEMA yanatulia baada ya wingu zito subiri sasa muone kinachotokea huko kijjanini
 
Back
Top Bottom