Waziri Mkuu Mizengo Pinda "Mtoto wa Mkulima", amesema Kazi ya John Pombe Magufuli ni kushughulikia Rushwa iliyokithiri Ujenzi na si kubomoabomoa Nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara na kwa hivyo amemtaka aache bomoabomoa.
My Take:
Pinda anataka kutuambia kwamba Magufuli kazi yake ni kupambana na rushwa ujenzi kwa hiyo tusahau ujenzi wa miundo mbinu, no wonder sijasikia ujenzi wowote uloanza pamoja na uchapakazi wa Magufuli. Ahadi hii tuisahau.
Lakini Pinda kwa matamshi yake haoni kwamba anavunja sheria kwa kuruhusu watu kujenga kwenye eneo la hifadhi ya barabara? Pinda nilitegemea awe wa kwanza kukemea uvunjaji wa sheria. Hatuna waziri mkuu.
Hivi serikalini bado hakuna collective responsibility? Mambo aliyokuwa anayafanya Magufuli ni kwa kukurupuka kwake, hawakuamua kwa pamoja. Hivi tuna serikali kweli au vurugu na fujo?
Mheshimiwa Magufuli umedhalilishwa, yaani jitihada zote hizo ni bure, ningekushauri ung'atuke, jiunge Chadema, gombea ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Chato utakaofanyika baada ya wewe kujiuzulu, utapewa huo uwaziri baada ya CDM kuchukua nchi.