waziri mkuu mizengo pinda "mtoto wa mkulima", amesema kazi ya john pombe magufuli ni kushughulikia rushwa iliyokithiri ujenzi na si kubomoabomoa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara na kwa hivyo amemtaka aache bomoabomoa.
My take:
Pinda anataka kutuambia kwamba magufuli kazi yake ni kupambana na rushwa ujenzi kwa hiyo tusahau ujenzi wa miundo mbinu, no wonder sijasikia ujenzi wowote uloanza pamoja na uchapakazi wa magufuli. Ahadi hii tuisahau.
Lakini pinda kwa matamshi yake haoni kwamba anavunja sheria kwa kuruhusu watu kujenga kwenye eneo la hifadhi ya barabara? Pinda nilitegemea awe wa kwanza kukemea uvunjaji wa sheria. Hatuna waziri mkuu.
Hivi serikalini bado hakuna collective responsibility? Mambo aliyokuwa anayafanya magufuli ni kwa kukurupuka kwake, hawakuamua kwa pamoja. Hivi tuna serikali kweli au vurugu na fujo?
Mheshimiwa magufuli umedhalilishwa, yaani jitihada zote hizo ni bure, ningekushauri ung'atuke, jiunge chadema, gombea ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa chato utakaofanyika baada ya wewe kujiuzulu, utapewa huo uwaziri baada ya cdm kuchukua nchi.
Kitaratibu, kiutawala, kikatiba, kisheria, ni jambo gani ambalo ni lazima lipitie Baraza la Mawaziri?
Kumbuka Ngeleja alipotangaza kulipa Dowans, Sitta na Sumaye wakasema "haijapita baraza la Mawaziri." Kumbuka kuuzwa nyumba za serikali zilizopita Baraza la Mawaziri, watu wakasema haijapita Bungeni. Kumbuka Mkataba wa Richmond Mwakyembe alioandika hajaona kumbukumbu ya kikao cha baraza. Jambo gani ni lazima lipitie Baraza la Mawaziri, na imeandikwa wapi?
magufuli ajiuzulu kwa kuzuiwa kufanya kazi yake kwa ufanisi! That is the next step forward....
Jatropha nimekuelewa vizuri lakini kama na wewe umenielewa ugomvi wangu ni kwa waziri mkuu kutamka hivyo hadharani, haoni kwamba hata wale ambao walisitisha ujenzi maeneo husika wataendelea kwa kuwa wameruhusiwa kufanya hivyo.waziri mkuu tunaye sana, tatizo lako kapotolo umelishwa propaganda za magufuli na wewe kuzichukulia zilivyo. Imebidi waziri mkuu aingile kati ili kuokoa fdha za serikali kulazimika kuwalipa watu fidia baada ya kushinda kezi zao mahakamani kama ilivyotokea 2001 wakati magaufuli alapoagiza petrola station mjini mwanza ibomolewe kwa kuwa imejengwa katika hifadhi ya abarabara kumbe sio kweli hata kidogo. Serikali ililazimika kulipa fidia ya bilini 3 kwa mmiliki wa petrol station iliyobomolewa. Baadaye ukweli halisi ulifichuka kuwa magufuli alikuwa na chuki na mahndisi wa jiji la mwazana mahandisi tizeba toka hapo wizarani, tume ya jiji mpaka alipohamishiwa jiji la mwanza kama mhandisi wa jiji la mwanza. Aliwahi hata kufanya jitihada za kujaribu jina la mhandisi huyo kufutwa katika orodha ya wahandisi waliosajiliwa hapa nchini. Katika kutimiza kiu ya chuki zake na mhanddisi huyo ndipo akaamuru ibomolewe.
Jumamosi iliyopita ulikuwepo na mkutano wa waathirika wa eneo la ubugo kimara, zaidi ya watu 50 wana hati miliki, na nyumba zao tayari zimechafuliwa kwa kuweka alama ya x na "maneno bomoa mali ya tanroad" je huo si ukiukwaji wa sheria za nchi? Mtu kama huyu unaweza kusema nafuta sheri kweli? Kwani magafuli anatumika serikali ipi na ni serikali ipi iliyowapatia wananchi hao hati miliki?
Ibara ya 2 ya sheria ya barabara ya 1967 inatamka wazi wazi kuwa hifadhi ya barabara zote kuu (trunk roads) hapa nchini itakuwa futi 75 au mita 22.86 kila upande sawa na futi 150 au mita 45 pande zote mbaiuli. Ibara ya 27 ya kanuni za sheria ya barabara ya 2007 zilizopitishwa kupita tangazo la serikai na 21 la tar 23 januari 2009 inatamka kuwa upana wa chini kabisa wa "lane" moja ya barabara kuu hapa nchin utakuwa si chini ya ni mita 3.25. Hivyo eneo la hifadhi ya barabara la mita 45 lina uwezo wa kuzalisha lane 14; lane 7 za kwenda upande mmoja na lane 7 za kwenda upande mwingine. Nitajie barabar gani hapa nchini imewahi kutumia na kumaliza upana huo uliotengwa kiasi cha magafuli kuwavamia watu walioko mita 120 kutoka katakati ya barabara? Hivyo ni propaganda kudai kuwa msongamano wa magari unasababsihwa na watu kujenga katika hifadhi ya barabara.
Kifungu cha 15 na 16 cha sheria ya aradhi namba 5 ya 1999 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanyikia wakati wa operesheni vijiji ni halali (soma attachement) hivyo sheria ya barabara ya 1967 anayotumia magufuli mwaka 2001 hadi 2010 imeshafutika na haiapo kabisa. Maaufuli anatakiwa kwanza kujenga lane 14 katika hifadhi ya barabara iliyopo ndipo aje kuwaingilia walioko nje ya eneo hilo. Kwa hali hii utagundua kuwa mambo anayoyafanya magufuli ni matokeo ya kukurupuka kwake katika yote hamshirikishi ofisi ya waziri mku, wizara zingine, ngazi za mkoa, wilaya, manispaa, serikali za mitaa
ndiyo maana inasemwa siku zote - ni vigumu kuwa mwadilifu ndani ya serikali isiyo na uadilifu. hao akina magufuli, sita, mwakyembe hawawezi kuwa effective ndani ya serikali ya chama cha sasa.
Wazee nimesikia kwenye taarifa ya habari usiku huu kupitia RFA kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesitisha ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara nchini kote. Najua ubomoaji huo ulikuwa unafanywa kwa amri ya Mhe. Pombe Magufuli. Hii amri ya Pinda, imekaaje wazee? Au ndiyo mwendelezo wa tabia ile ile ya serikali yetu ya sasa ambapo kila kiongozi anafanya kazi na kutoa statements kadri anavyojisikia? Mhe. Magufuli atajisikiaje?
jatropha nimekuelewa vizuri lakini kama na wewe umenielewa ugomvi wangu ni kwa waziri mkuu kutamka hivyo hadharani, haoni kwamba hata wale ambao walisitisha ujenzi maeneo husika wataendelea kwa kuwa wameruhusiwa kufanya hivyo.
Na kitu kiinge angemwita ofisini amweleze bwana hili unalofanya litatugharimu, ili wananchi tubaki tunajua kwamba kujenga kwenye hifadhi ya barabara ni kosa, lakini walojenga kwa hizo sheria za zamani wasibomolewe.
Halafu naamini magufuli sio mbumbumbu wa sheria kiasi hiki, nadhani anafahamu anachokifanya, incidencies za makosa zipo unapotekeleza majukumu yako. Mimi nadhani magufuli aendelee kusimamia sheria hata kama waathirika wa usimamizi wake wataendelea kumpinga akiwemo pm pinda.
kwaheshima na uungwana mgufuli jiudhulu wachie wafanye wanavyotaka.
Huwezi jua labda Magufuli alikataa kutii hiyo amri na akampa masharti labda atangaze mwenyewe Pinda. Unajua Magufulu hapendi kuwa kigeugeu, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa aliambiwa akakataa sababu kubomoa ni kutii sheria na Magufuli ni mtii sheria siku zote kwa hiyo hawezi kupindisha sheria kisiasa kama Pinda.
Pinda ni mwanasiasa wa kigeugeu tu ili mradi asimuumize mtu, anataka asilaumiwe, hatuna waziri mkuu hapo.
huyu pinda anajaribu kulaghai hasira za wananchi tu hakuna lolote hapo.wanajua wananchi wana hasira na serikali yao na hayo ameyaongea kule bukoba unategemea nini. angekuwa na busara angemwita magufuri wakae chini waone nini cha kufanya then anmwachia maghfuri mwenyewe atangaze kubadilisha maamuzi mpk itakapotangazwa tena. kamdhalilisha waziri wake tu kwa kuonyesha kwamba bomoa bomoa yake haiona baraka ya mabosi wake, kuanzia sasa mawaziri hawataweza tena kufanya maamuzi magumu na nchi ndio itakwenda kubaya mpaka tutajuta, tusubiri tuone. Mambo mengine nchi hii yanatia hasira jamani, natamani kujilipua katikati ya kikao cha baraza la mawaziri akiwepo raisi mwenyekiti wao tuunde serikali mpya, mbwa hawa wanachezea maisha yetu na ya vizazi vyetu vijavyo.