DOKEZO Waziri Mkuu kapotoshwa? Katika Sekta ya Afya, Muuguzi na Mkunga ni watu muhimu sana

DOKEZO Waziri Mkuu kapotoshwa? Katika Sekta ya Afya, Muuguzi na Mkunga ni watu muhimu sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Inashangaza kuona Waziri Mkuu akitoa taarifa ambazo hazijafanyiwa uchunguzi mbele ya umati wa watu.

Katika sekta ya afya nchini Muunguzi na mkunga ni kiungo muhimu sana, ni vibaya na aibu kuona viongozi wenye dhamana wakiwazungumzia vibaya.

1. Mnaua taaluma ya uuguzi na ukunga inchini

2. Mnawapa mashaka wanainchi wanaopata huduma kwenye vituo vya afya inchini

3. Mnaharibu psychologia ya mtoto anae tamani kua na ndoto ya kufanya kazi ya kutibu watu.

Hapa nchini, wauguzi na taaluma nyingine wamekuwa ya changamoto za kimiundo na miaka nenda miaka rudi mmekaa na nyaraka maofisini.

Kila Waziri akipewa hii sekta hatekelezi, wauguzi wanakabiliwa na changamoto kama zifuatazo:

1. Mishahara haiendani hali ya maisha ya sasa

2. Miundo ya kiutendaji,, Nurse ana degree ila usimamizi wa kituo kapewa Clinical officer mwenye diploma

3. Miundo ya mishahara imebakia kua wimbo wa wanasiasa majukwani, na jambo lisilo tekelezeka.

4. Kuhusishwa kwa taaluma ya uuguzi nq ukunga kwenye tuhuma ambazo hawajahusika nazo.

5. Kutolipwa malipo ya motosha na masaa ya ziada hili ni tatizo inchi nzima.

6. Mazingira duni ya kutendea kazi hii iko kote mijini na vijijini,, national hospita,, referral hospital na district hospital.

Hivyo basi, Viongozi wenye dhamana fanyieni kazi changamoto zao na sio kutoa tuhuma kwenye majukwaa ya kisiasa. Mfano ni tukio lililotokea Tabora bila taarifa kamili ya uchunguzi Waziri Mkuu akatoa tuhuma kwa wauguzi, hili halijakaa sawa.
 
Ungeambtanisha taarifa yake pia wengine tukajua kinachoendelea
 
Tena waziri mkuu ni mpumbavu kabisa kumfukuza mganga mfawidhi kumzalisha mjamzito nyumbani wakati nchi zilizoendelea zinahimiza na ktuoa msaada kwa wajawazito wanaozalia nyumbani

1773276195556.png
 
Back
Top Bottom