Waziri Mkuu apiga marufuku matumizi ya Shisha nchini

Shisha ni hatari kuliko sigara,na hivyo wanatia viroba na gongo badala ya maji baridi ni hatari zaidi, inashangaza eti mtu anauliza;

"Hivi ni idadi gani ya wananchi wanaotumia hili shisha mpaka lilete madhara kwa nguvu kazi?"

Kwa hiyo mlitaka serikali isubiri kwanza mpaka Shisha lisambae nchi nzima na kudhuru idadi kubwa ya watu ndipo serikali iingilie kati?

Ni vizuri kulikabili tatizo kabla halijakua.
hiyo shisha iko kwenye chupa au hebu tuwekee picha yake tuione
 
Tatizo la Nchi yetu ni vijana kutumia shisha au ndio usanii unaendelea tumechoka na ufisadi huduma mbovu za kijamii rushwa
 
Hongera Sana WAZIRI MKUU..

Ila mbona umekuwa kama BABA anayepoteza NGUVU ZAKE katika KUMSHINDILIA risasi JONGOO nje ya uzio wa nyumba wakati ndani ya NYUMBA kuna JOKA kubwa linalomalizia kutamfuna WATOTO limuanze MAMA?

PM ni kwanini NGUVU hiyo USIIPELEKE kwa JOKA linalomalizia vijana??

Inawezekana huyu nyoka akawa ANAFUGWA??
JONGOO anaharibu soko la nyama ya hili JOKA?
 
Wewe inakuletea pesa nyingi sana lakini serikali inapoteza nguvu kazi, inaongeza gharama za matibabu ya akili, familia zinakosa malezi bora. Ungeyajua haya sidhani kama ungetoa kauliya kebehi ya kijinga kiasi hiki.
Wahangaike na sukari mkuu, hicho ndio kilio cha watanzania angalau kwa sasa!!!!
Ujinga ujinga wa shisha, sijui mashoga hii ni matumizi mabaya ya ofisi.

Nilitaraji waielekeze bank kuu ihakikishe tunakuwa na hifadhi ya dhahabu angalau tani tano kwa mwaka (impact yake ni pamoja na kustabilize currency yetu)

Nilitarajia wataazimia kupeleka pesa kwenye michezo tuzalishe ajira kupitia vipaji vilivyopo nchini.

Nilitarajia watawaalika kwa ukarimu kabisa wataalam nchini kushiriki kulijenga taifa kwenye fani zao kwa kujitoa na kwa weledi uliotukuka,

SIONI HATA DALILI.

Wanakimbizana hovyo na wananchi, yaani ni kama tom and Jerry halafu wanajisifia ukuu wa vyeo tulivyowapa na wasivyo na soni wanatuomba tuwaombee kwa mungu!!!!! Yaani tuwaombee waendelee kukimbizana na wavuta shisha huku dhahabu inaondoka!!!!
 
Wanatakiwa wapige marufuku si shisha tu bali kuanzia viroba, zed, shisha, madawa ya kulevya, bangi, gongo ya siku hizi ya fertilizer mixed with horrible stuff. Yaani nguvu kazi hatuna tena hasa maeneo ya vijijini hata watoto hawazaliwi tena maana nguvu vijana hawana kabisa. Na mkemia mkuu wa serikali inabidi wapitie hivi vinywaji wajiridhishe na contents zake. Yaani nina hisia kazi hata hivi viwanda vya wenzetu wanaweza kutumaliza hivi hivi ili waendelee kututawala. Sorry kama nimeenda mbali but I am trying to think big.
 
Kwani vipi mke wng akinishauri afu kesho asubuhi niseme marufuku kula ugali na dagaa sababu inachochea ushoga!afu ndo nshasema hakuna kupinga
 
Hivi hii shisha ndio kitu kinaumiza uchumi wa tanzania kiasi cha kukomaliwa namna hii??? au ndio viongozi pumzi imekata.
Tumia akili wewe vijana ndio nguvu kazi,wakiachiwa watopee katika shisha,baada ya miaka mitano kila mtu teja
 
hiyo shisha iko kwenye chupa au hebu tuwekee picha yake tuione
Screenshot_2016-07-04-18-12-08.jpg
 
Pombe saa10, no shisha, no Mashoga, no bangi, no mirungi, no pool table, no mirungi, no viroba, sasa kimebaki nin???
 
Tunataka kuona kwa vitendo na siyo kutoa matamko wakati vijana wetu wanazidi kuangamia. Haya mambo yamekuwepo toka muda mrefu, na kwa mantiki hiyo wanatakiwa sasa kufanya maamuzi
 
Tumia akili wewe vijana ndio nguvu kazi,wakiachiwa watopee katika shisha,baada ya miaka mitano kila mtu teja
Tukiruhusu matumizi ya akili mbovu kama hii yako kujamiiana kungeshapigwa marufuku siku nyingi sana, maana UKIMWI hauna mchezo wala utani.
PUMBAVU MKUBWA WEWE (nimemnukuu mkapa)
 
Back
Top Bottom