Waziri Mkuu: Wananchi wapunguze matumizi ya kuni na mkaa, watumie nishati mbadala

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndugu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati mbadala.

Swali langu ni nishati mbadala kwa mwananchi wa kipato Cha chini ni ipi?
 
Wanasema tusitumie kuni na mkaa kupikia sasa tutumie nini? Majiko ya gesi na gesi yenyewe bei zake ziko juu mno hatuwezi kuzimudu, umeme ndo usiseme. Wanataka tule vyakula bila kupika?
Gesi bei kubwa, pia hali ikibana huwezi kupata gesi ya buku 3. Lakini mkaa na kuni unapata,
Nashauri gesi iuzwe kwa kupima kuanzia kilo moja, siku hali ikiwa ngumu unaenda na mtungi unapimiwa,
 
Sina uhakika kama waziri mkuu anaelewa anacho ongea.kama kweli amezingatia maisha ya watanzania kwa sasa,sina hakika.
 
Ni ishara tosha ya madhara ya michango,mikopo,misaada na ukosefu wa elimu za athari za Maendeleo.

Wezesheni wananchi badala ya kuwawezesha wafanyabiashara.

Wezesheni wananchi uwezo wa kupata kipato na kukuza kipato ili waweze kumudu maisha yao bila shuruti zenye kuongeza sintofahamu.

...i.
nilisikia bungeni, na nimeona milingoti ya sementi ya kushikilia nyaya za umeme kama mbadala wa kutumia miti, hili, nafikiri linafanyika ili -kupunguza kasi na makali ya kukatwa miti- lakini sijasikia kama uuzwaji wa miti hiyo nje ya nchi umepungua, Kwanini? Sijui
.
Je kupunguza utumiaji wa kuni na mkaa utaenda sambamba na kusitishwa kabisa, yaani fullstop uuzwaji wa miti nje ya nchi?? Sidhani, lakini nitafarijika ikiwa itakuwa hivyo.

Halikumhali...

Nina uhakika hili jambo lilikubaliwa Paris bila ridhaa ya wananchi-sasa mnasokomeza yale mliyoyakubali bila kutizama au kuridhia athari zake wakati mkijua sintofahamu za mabilioni yaliyotolewa??? mweee

...nitasema kuwa, Serikali isiwe chombo cha kulazimisha masoko kwa Wananchi wengi ambao bado wana sintofahamu za athari za Maendeleo. Serikali isiwe chombo cha wawekezaji uchwara wanaotafuta masoko kwa kasumba ili mradi tu kuwanufaisha hao wawekezaji kwa kulazimisha masoko ya bidhaa zao bila kuangalia kwa umakini shida watazokuja kupata wananchi.

Ushauri kwenu, tumieni fedha hizi kununulia magari ya umeme kwa Serikali yote. Wahenga wanasema charity starts at home.
 
Dar es Salaam mtungi wa 30Kg ni 57,000/= ambayo roughly ni kwa mwezi. Ni wananchi wangapi wa Tanzania hii wenye uwezo wa kumudu bei hiyo kila mwezi kwa ajili ya nishati peke yake? Tulitegemea serikali ije na mikakati inayotekelezeka badala ya kauli za jumla jumla!
 
Mambo ni ngumu kuliko Viongozi wanavyofahamu.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndugu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati mbadala.

Swali langu ni nishati mbadala kwa mwananchi wa kipato Cha chini ni ipi?
Huyo mpumbaa kwanini asikeshe kwenye ujenzi wa bwawa la umeme ili likamilike umeme ukiuzwa UNIT 4 SH1000 hapo ndiyo utakuwa mwisho wa mkaa tz nasi vinginevyo watu wanatumia nishati iliyo nafuu zaidi kama bei ya gesi inapandishwa kila siku na mafisadi yeye anategemea nini?
 
Dar es Salaam mtungi wa 30Kg ni 57,000/= ambayo roughly ni kwa mwezi. Ni wananchi wangapi wa Tanzania hii wenye uwezo wa kumudu bei hiyo kila mwezi kwa ajili ya nishati peke yake? Tulitegemea serikali ije na mikakati inayotekelezeka badala ya kauli za jumla jumla!
Poleni. Viongozi wetu siyo wazalendo. Pm na ukoo wake pengine hawajui hata bei ya gesi Wala nishati yoyote kwa maana wanazitumia at zero cost. Hawawezi kuona uchungu na maisha ya binadamu wengine kabisa
 
Gesi bei kubwa, pia hali ikibana huwezi kupata gesi ya buku 3. Lakini mkaa na kuni unapata,
Nashauri gesi iuzwe kwa kupima kuanzia kilo moja, siku hali ikiwa ngumu unaenda na mtungi unapimiwa,
Pengine waziri ana ubia na makampuni ya nishati mbadala kwahiyo hii kauli ni kama tangazo la biashara
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndugu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati mbadala.

Swali langu ni nishati mbadala kwa mwananchi wa kipato Cha chini ni ipi?
Hawa watu hawako serious. Gas bei ghali kiasi kwamba mwananchi wa kipato cha chini hawezi kuafford. Kuni na mkaa hawawezi kuacha kamwe.
Wakitaka watu wapunguze matumizi ya mkaa inabidi gas iwe bei chee sana. Kama dar mtungi wa oryx size ya kati ni 56000, sijui mkoani itakuaje
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndugu Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa na kutumia nishati mbadala.

Swali langu ni nishati mbadala kwa mwananchi wa kipato Cha chini ni ipi?

Hivi waziri mkuu anaishi nchini? Hajui waliongeza kodi kwenye gas sasa wangapi watamudu kununua hiyo gas?
 
Jamani njia mbadala hamuelewi? 😅😅 Kama mtu haelewi shauri yake 😅 mimi nishaelewa.
 
Back
Top Bottom