Waziri Mkuu apiga marufuku matumizi ya Shisha nchini

Hizi tabia za kuiga zinatusaidia nini? Tunaneemeka nini kuona jamii yetu inatekea kwa madawa na ulevi uliopindukia? Waziri Mkuu yuko sahihi
 
Hii safi sana , hivi vilevi vinavyo dhuru afya na kufanya watu wanapoteza muda mrefu katika magenge na kuwa wavivu ni lazima vimulikwe
 
Yaani kabisa na tai yangu na suti yangu naacha changamoto zote za wananchi wangu nakaa mbele ya Camera nazungumzia shisha?!
Hivi shisha ina percentage ngapi ya madhara ya kiuchumi na kijamii kwa mamilioni ya vijana wa Tanzania?
Hili ndilo tatizo kubwa kabisa kwa vijana kuliko mengine?
Huu mchezo wenu wa kutusahaulisha madai yetu ya msingi kwenu viongozi tumeugundua.
Shisha waachieni wazazi watashughulika nao,vipi ajira?Vipi ile mikopo?Vipi ubora wa elimu?Vipi pembejeo?vipi uhaba wa waalimu?Vipi thamani ya shilingi?Vipi afya?Vipi michezo?
Kuna mambo ya msingi hatutayasahau,nyie zungukeni wee,mkija tutawauliza haya haya,hakuna cha shisha wala shushu hapa!
Ngoja nilog off watu hawa wanatia hasira kweli!
Acheni upuuzi kwenye mambo ya msingi,na msilete siasa kwenye maisha ya watu,siyo kila jambo ni kupinga tu hata kama madhara ni kidogoo bac yazuiwe yasikue zaidi,au mnataka wakianza kuugua mje kulaumu kwann shisha haikuzuiwa toka mwanzo,mpaka sasa nimeielewa serikali na hilo katazo kwa sababu imeona mbali
 
kuchanganya na madawa ni uamuzi wa watumiaji.....shisha inatumia tumbaku ya kawaida........sawasawa na pombe mtu amue kutumia gongo ......NB: Tumbaku zote zina madhara
He kweli ni kichwa, kwahiyo serikana haina sababu ya kusimamia Afya za wananchi wake, kumbe hata wanapowashitaki watu wanakusudia kujinyonga wanakosea, kwa sababu ni uamuzi wao.
 
Yaani kabisa na tai yangu na suti yangu naacha changamoto zote za wananchi wangu nakaa mbele ya Camera nazungumzia shisha?!
Hivi shisha ina percentage ngapi ya madhara ya kiuchumi na kijamii kwa mamilioni ya vijana wa Tanzania?
Hili ndilo tatizo kubwa kabisa kwa vijana kuliko mengine?
Huu mchezo wenu wa kutusahaulisha madai yetu ya msingi kwenu viongozi tumeugundua.
Shisha waachieni wazazi watashughulika nao,vipi ajira?Vipi ile mikopo?Vipi ubora wa elimu?Vipi pembejeo?vipi uhaba wa waalimu?Vipi thamani ya shilingi?Vipi afya?Vipi michezo?
Kuna mambo ya msingi hatutayasahau,nyie zungukeni wee,mkija tutawauliza haya haya,hakuna cha shisha wala shushu hapa!
Ngoja nilog off watu hawa wanatia hasira kweli!
Umenena. Waache kutubabaisha. Kama muna nia ya dhati kupiga marufuku hivi vitu tungeni Sheria zifuatwe wacheni kuropoka ovyo.
 
Shisha kwa kichaga ni SAFI/NZURI naomba serikali ije hewani na vitu vya msingi.Namkumbuka sana Amina Chifupa wa Mpakanjia alivyoachwa kuungwa mkono na serikali hii hii ya CCM
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili kuwaokoa vijana.

Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na kufuata popote.

Asisahau na sigara maana yote kundi moja.
 
Shisha ni hatari kuliko sigara,na hivyo wanatia viroba na gongo badala ya maji baridi ni hatari zaidi, inashangaza eti mtu anauliza;

"Hivi ni idadi gani ya wananchi wanaotumia hili shisha mpaka lilete madhara kwa nguvu kazi?"

Kwa hiyo mlitaka serikali isubiri kwanza mpaka Shisha lisambae nchi nzima na kudhuru idadi kubwa ya watu ndipo serikali iingilie kati?

Ni vizuri kulikabili tatizo kabla halijakua.
Ndani ya hio shisha wanatia viroba na gongo?
angalau ungesema wanaweka bangi.
msiropokwe tu vitu musivyovijua.
ni kweli ni hatari kuliko sigara, maana kumaliza kile kipande cha tumbaku ni sawa na kukaribia pakti mbili za sigara. ila usidanganye watu kama wanawake gongo utachekwa
 
Acheni upuuzi kwenye mambo ya msingi,na msilete siasa kwenye maisha ya watu,siyo kila jambo ni kupinga tu hata kama madhara ni kidogoo bac yazuiwe yasikue zaidi,au mnataka wakianza kuugua mje kulaumu kwann shisha haikuzuiwa toka mwanzo,mpaka sasa nimeielewa serikali na hilo katazo kwa sababu imeona mbali
Soma post namba 186.Kama hutaielewa rudia tena na tena hadi uelewe.
 
Ndani ya hio shisha wanatia viroba na gongo?
angalau ungesema wanaweka bangi.
msiropokwe tu vitu musivyovijua.
ni kweli ni hatari kuliko sigara, maana kumaliza kile kipande cha tumbaku ni sawa na kukaribia pakti mbili za sigara. ila usidanganye watu kama wanawake gongo utachekwa
Mbona comment yako kama umekunywa maji machafu? Nime quote maneno ya PM na ndio maana nikasema "na hivyo wanavyotia gongo na viroba ndio hatari zaidi" hukumsikia PM akisema maneno hayo? Mimi najua Shisha hutiwa maji baridi kwenye ule mtungi wake, umenielewa wewe Punguani?
 
Yaani kabisa na tai yangu na suti yangu naacha changamoto zote za wananchi wangu nakaa mbele ya Camera nazungumzia shisha?!
Hivi shisha ina percentage ngapi ya madhara ya kiuchumi na kijamii kwa mamilioni ya vijana wa Tanzania?
Hili ndilo tatizo kubwa kabisa kwa vijana kuliko mengine?
Huu mchezo wenu wa kutusahaulisha madai yetu ya msingi kwenu viongozi tumeugundua.
Shisha waachieni wazazi watashughulika nao,vipi ajira?Vipi ile mikopo?Vipi ubora wa elimu?Vipi pembejeo?vipi uhaba wa waalimu?Vipi thamani ya shilingi?Vipi afya?Vipi michezo?
Kuna mambo ya msingi hatutayasahau,nyie zungukeni wee,mkija tutawauliza haya haya,hakuna cha shisha wala shushu hapa!
Ngoja nilog off watu hawa wanatia hasira kweli!
mkuu, tatizo linapaswa kuwa kubwa kiasi gani ndio lianze kupigwa marufuku???!!!!!!!!!!!!!!
 
He kweli ni kichwa, kwahiyo serikana haina sababu ya kusimamia Afya za wananchi wake, kumbe hata wanapowashitaki watu wanakusudia kujinyonga wanakosea, kwa sababu ni uamuzi wao.

nilichokuwa namaanisha SHISHA NI KAMA TUMBAKU NYINGINE...wanaoitumia kwa kuchanganya na madawa ni kwa uraibu wao binafsi lakini shisha haina madawa ya kulevya.... .ilipaswa kupiga marufuku matumizi ya tumbaku zote kwa sababu zote zina madhara ya kiafya kwa binadamu na sio kuichagua shisha tu...ndo maana nikasema nb..tumbaku zote zina madhara
 
Umeeleweka mkuu, wakati mwingine lazima tukae upande wa pili, ili kuona mawazo na michango ya wengine.
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili kuwaokoa vijana.

Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na kufuata popote.

Kauli zinatolewa bila utafiti na ushahidi wa kutosha ni hatari sana
 
Back
Top Bottom