Waziri Jafo apiga marufuku Majeshi na Shule kutumia kuni na mkaa kama nishati ya kupikia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amepiga marufuku shule zote za sekondari (Binafisi naza Serikali) nchini kutumia kuni na mkaa kama nishati ya kupikia, na badala yake wajikite katika matumizi ya nishati mbadala.

Waziri Jafo amesema matumizi ya kuni na mkaa yanachochea uharibifu wa mazingira hali inayosababisha misitu kuisha na kuzitaka taasisi za majeshi, Shule za Sekondari kote nchini kujikita katika matumizi ya nishati mbadala.

Meneja masoko na uhusiano ya umma kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Geofrey Meena amesema shirika hilo limezindua matumizi ya mkaa mbadala ili watu wasikate miti kwa lengo la kutunza mazingira.

Waziri Jafo amewataka STAMICO kuongeza kwa wingi uzalishaji wa mkaa mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa Watanzania na taasisi mbalimbali hapa nchini.

Chanzo: Swahili Times
 
Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amepiga marufuku shule zote za sekondari (Binafisi naza Serikali) nchini kutumia kuni na mkaa kama nishati ya kupikia, na badala yake wajikite katika matumizi ya nishati mbadala.
Mbona makaa ya mawe yanatoa kaboni nyingi zaidi kuliko kuni?
 
Hawa wamelewa baadaye tusitumie Moto Mana vinyesi vinaangamiza samaki mtoni. Serikali Ni mtu mmoja anaendesha Taifa zima. Hilo Samia umelitoa kwa wauza mkaa mbadala ama msoga wamekuambia Cha kufanya.

Wao watoe matamko Ila siku raia wakichoka Ni machafuko ya hatari mno. Shida yetu akili ndogo Askari naye anatumika kumlinda jamaa na analipwa hela zetu.


Ujue wazungu wakiitaka bidhaa yako fulani isitumike ili wauze ya kwao wanawarubuni wanasayansi wanasema matumizi ya hii ya muda mrefu yanaleta kansa.

Majuzi hapa wamesema eti ulaji wa mchele ama wali mweupe unaleta Aina fulani ya kansa,watabe wa USA ,Sasa bwana wa Asia kwa vile Ni their staple food wakawashambulia kuwa yaani mnaziacha burger za MacDonald na junk food mnakomaa na rice.

Yaani Yanvari marope alivyogawa mitungi ana discourage matumizi ya kuni na mkaa ili aliyempa cheo wauze gesi yao kupitia kwa rostam na Taifa gesi yake ili biashara yake ikue hisa zipande value ,huyu angekuwa na wanasayansi angewahonga hela watoe research ya side effects zake Tena watu wanapewa hela wanalazwa ocean roads ,muhas,cuhas kuwa wametolewa huko vijijini kwa kutumia mkaa Ni wagonjwa wamelazwa wanapigwa mionzi ya chemotherapy.

Mbona sigara ,majuisi yaliyojaa unga na flavor zake baresa,mo,Jambo,sayona, na soda za pepsi,coca zilizojaa masukari ili kuwapa watu short term pleasure ,ya kutoka Kenya, ulaya,sauzi,hayapigiwi kelele kuwa hayana faida zozote zile mwilini Ni ujinga wa watu kuendekeza hisia ama utamu wa mdomoni wanakunywa wanawapa watt wadogo, kuwa Yana negative side effects.

Sigara haipigiwi marufuku kuwa inachafua ama kuuua mapafu na mazingira ya mwili wa mtumiaji Kama harufu, meno ,lips kuchafuka wao wanaicheki mazingira ya miti na mito na maziwa na bahari.

Jiulize hizo soda tokea Karne na Karne umeshasikia kuwa mtu aliugua na upungufu wa kukosa soda mwilini.
Ila bana kisa mtu kuwa kiongozi,elimu fulani,pesa unadhani wasio navyo hawawazi ama hawana akili.

Africa yangu I cry for you. Bora sijui mkoloni mweupe Ila kuliko blacks wenzako.

Jiulize why black Americans wameshajua chimbuko lao wengine mpaka makabila yao Ila hawadhubutu kamwe kurudi Africa wanaona Ni Bora wafie mikononi mwa weupe kuliko weusi wenzao.

Am in mission to migrate to any country in Europe.
First am looking for apartment payment 💰 💰.
 
Upigaji marufuku ni amri isiyotekelezeka. Wakiweka ruzuku ili bei ya gesi ipungue ya kutosha kuvutia wengi, ukataji wa miti utapungua tu.
 
Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amepiga marufuku shule zote za sekondari (Binafisi naza Serikali) nchini kutumia kuni na mkaa kama nishati ya kupikia, na badala yake wajikite katika matumizi ya nishati mbadala...
Huu ujinga wa watawala wetu ''kutuongoza'' kwa kutumia maonyo, vitisho na matamko utaisha lini? Kiongozi kazi yake ni kuonyesha njia na siyo kutoa vitsho.

Ni kweli wengi tunaunga mkono kusitisha matumizi ya kuni na mkaa, lakini hili jambo linatakiwa lifanywe kwa kutoa muda na taratibu.

Huwezi kuamka na kutoa tamko kama ulikuwa unafukuzwa na simba. Andaa jamii, waonyeshe njia, wape muda.
 
Kwa hiyo miti kukatwa sana au

Basi sawa,wafanye gesi iwe nafuu kila mtu aweze imudu

Ova
Mkuu hawa watawala wanatuongoza siyo kwa kutuonyesha njia, bali kwa kututisha, kutukaripia na kutukataza. Hili siyo jambo la kukurupuka. Linahitaji muda ili shule zijiandae. Na serikali inatakiwa kutoa mchango wake, kwa kupunguza bei au kodi kwa wahusika. Gadeeeem!
 
Back
Top Bottom