Waziri Mkuu apiga marufuku matumizi ya Shisha nchini

Kule kijijini kwetu hakuna hata mmoja anayejua kitu kinaitwa shisha, sielewi kwa nini serikali inataka kulifanya kama jambo la kitaifa.

Sehemu wanapovuta bado ni chache na zinajulikana badala ya kutuma polisi kuwakamata wahusika instead wamekazana kushindana kwa matamko.
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.
Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi wote mtetezi wao ni chadema!!!

Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
 
Nijambo jema kukemea na kudhibiti upuzi nchini,heko Mh. PM. Hao wanaopinga ndowale raia uchwara wasojua jema!! Tusikalie siasa linapokuja swala la uhai na ustawi wa taifa.uzalendo kwanza
 
Hivi hii shisha ndio kitu kinaumiza uchumi wa tanzania kiasi cha kukomaliwa namna hii??? au ndio viongozi pumzi imekata.
Wewe inakuletea pesa nyingi sana lakini serikali inapoteza nguvu kazi, inaongeza gharama za matibabu ya akili, familia zinakosa malezi bora. Ungeyajua haya sidhani kama ungetoa kauliya kebehi ya kijinga kiasi hiki.
 
Nawashauri wanajf wenzangu,tukiona hawa jamaa wanataka kutusahaulisha,wanapoleta hizi habari zao sisi hapo hapo tuwakumbushe ya kwetu na mimi kwa mfano naanza hapa.

WAHESHIMIWA AHSANTE KWA CONCERN YENU KUHUSU SHISHA,VIPI NA ILE AHADI YA TATIZO LA MAJI KUISHA DAR?LILE BOMBA JIPYA BADO?
NA WAALIMU KUPANDA DALADALA BURE JE? NA KUWARUDISHA OMBAOMBA MAKWAO JE? NA KUGAWA SUKARI BURE JE? NA KUHAMISHA KITUO CHA MABASI YA MIKOANI UBUNGO JE? ETC.,ETC,.
 
Hapana namuunga mkono kwa jambo hili, shisha imeharibu watoto mno tena upuuzi wa shisha umechukua wa kike na wa kiume
Shisha ni hatari kuliko sigara,na hivyo wanatia viroba na gongo badala ya maji baridi ni hatari zaidi, inashangaza eti mtu anauliza;

"Hivi ni idadi gani ya wananchi wanaotumia hili shisha mpaka lilete madhara kwa nguvu kazi?"

Kwa hiyo mlitaka serikali isubiri kwanza mpaka Shisha lisambae nchi nzima na kudhuru idadi kubwa ya watu ndipo serikali iingilie kati?

Ni vizuri kulikabili tatizo kabla halijakua.
 
Chadema watatetea kila aina ya uozo mwaka huu.

Majizi, mafisadi, mashoga, vibaka, wakwepa kodi, wavuta shisha wote mtetezi wao ni chadema!!!

Hii ndio maana ya chama kubadili gia angani.
 
Hivi hii shisha ndio kitu kinaumiza uchumi wa tanzania kiasi cha kukomaliwa namna hii??? au ndio viongozi pumzi imekata.
Mkuu hii shisha inaonekana inaharibu sana nguvu ya taifa, kuna hatari kubwa ya vijana wengi kuingia kwnye matumizi hayo kwa sababu ni addictive
 
Pm mzima anazungumzia shisha? Kweli siku izi kick za makontena zimeisha sasa watu wanatafuta nitoke vp
 
MADAWA YA KULEVYA VIPI TENA..!!?

Mbona sisikii vita dhidi ya Madawa ya KULEVYA..? Nadhani madhara ya madawa ya kulevya ni mara 10 zaidi ya sigara au shisha.. Ningependa kwa priority zaidi wakomeshe madawa ya kulevya, Ushoga, kisha sisha then sigara...!!
 
Back
Top Bottom