Waziri mkuu anapokwenda holiday na mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu anapokwenda holiday na mkewe

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Game Theory, Apr 8, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu hafit kuitwa mtoto wa Mkulima kwani he's an old Etonian born into priviledge and multi billionaire from Aristocratic family..kama kawaida ya watawala wa UK lakini.

  [​IMG]

  Hapa waziri mkuu yuko departure lounge ya KAWAIDA na sio VIP na mkewe wakisubiri kwenda Spain for holiday. Anatumia pesa zake binafsi, na anatumia budget airline ambayo haina Business wala first class

  [​IMG]
  Hapa washafika huko Spain na hakuna maduka kufungwa au watu kuzuiwa kufanya kazi zao eti kwa sababu kiongozi wa nchi jirani kaja bas mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa,sijui mpage gani shughuli zote zinasimama

  [​IMG]

  Badala ya kuwa na wapambe wa kumtolea pesa...jamaa anatumia cadi yake kutoa pesa kama watu wengine na ifact inasemekana ALIFUNGA foleni

  If only WATAWALA wetu wangekuwa kama huyu. Kama kuna mtu anayo picha ya MTAWALA wetu hata mmoja ambaye anafanya mambo ya kawaida kama sie watu wakawaida ailete hapa. Saa zingine utaambiwa eti ohhh sababu za kiusalama. Hivi kwenye ukishakuwa MAN OF THE PEOPLE unataka ulizni wa nini?

   
 2. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,875
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Aaaah kwa kweli huyu bwana anavutia kwa jinsi alivyokaa utafikiri mkulima tu!!! Hongera yake.
   
 3. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viongozi wetu wanapaswa kujifunza kwa viongozi kama hawa
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hivi kati ya huyu na yule wa kwetu nani ni mtoto wa mkulima???:mmph:
   
 5. A

  Abunuas JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 8,730
  Likes Received: 420
  Trophy Points: 180
  ndugu yangu sisi tupo katika stone age na wala si iron age period. Viongozi wetu wanajifanyia chochote wanachotaka. lakini haya mabadiliko yajayo yatatuondolea tongotongo machoni. Ewe mungu tusaidie.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,103
  Trophy Points: 280
  ..hivi hamkumuona Kikwete na Salma wamepanda bembea walipokwenda Jamaica?
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Hawafunziki...wao wanataka wawe kama Jay Z au Rambo......yaani mastaa...na hawaendi holiday...kwa vile hawafanyi kazi na hawachoki..wao holiday kila siku
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Kwa hela ya nani?
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  sasa hivi dar es salaam airport wameweka mpaka njia ambayo ni separate kutokea VIP mpaka Nyerere rd. Ubaguzi na dharau za hali ya juu ....sijui kama Mungu atawabariki!
   
 10. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  ni issue y a culture, kwanini ufanye kitu ambacho hukijui, au kama una kijua hakikupi raha. likizo zetu wengi ni kwenda kijijin kuwaona ndugu zetu na kupumzika kwenye mashamba.....sio kuzunguka sehemu za gharama kama wenzetu......mimi wacha wafanye chochote kile as long as kina wapa furaha na mapumziko ambay yatatoa akili zao kwenye maisha yao ya kila siku ya kazi na stress....
   
 11. B

  Bobby JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Yule wa kwetu theoretically ni mtoto wa mkulima lakini practically ni mtoto wa billionaire fulani hivi. Kuna thread moja humu ilitolewa picha ya msafara wake akiwa morogoro, OMG huo msafara sitaki kusema mengi. Huyo David Cameron kimatendo ni zaidi ya mtoto wa mkulima jamani tumpe haki yake though ametoka kwenye familia matajiri wa kutupwa. Hivi hamkumbuki zile salary cut down alizoingia nazo alipoanza kazi? Sikumbuki vizuri how much ila kuna savings za £ millions kutoka kwenye hilo. Hizi scenario mbili ukiziangalia vile zilivyo unaweza kudhani Tanzania ndio Donor na UK ni recipient wa misaada. Shame on us Tanzania.
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Obama wa Marekani awapo likizo anapanga msitani na wateja wengine kununua sandwich Mcdonald kwa pesa yake ya mfukoni, mkulu wetu je?
   
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Atakwambia hajui sandwich ni nini......kila kitu hajui
   
 14. c

  collezione JF-Expert Member

  #14
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  sisi nchi za kimaskini tupenda makuu sana...na tatizo ni kwamba viongozi wetu wenyewe wametokea kwenye shida, so kupanda uongozi ndo chance yao ya kula...
  kuna mwana-falsafa mmoja alishawahi kusema kuwa "average income people use the larger proportion of their income in uneccessary luxury expenditure than rich people, so as to show up the world NA WENYEWE WAPO KATIKA CHATIi"
  he he he he he
  ndo maana sishangai kuona seriakali ya TZ inatumia magari ya kifahari zaidi ya serikali zenye uchumi mkubwa kama UK
  hii ni kutokana ulimbukeni wa viongozi wetu
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Huyu ni Makamu wa JK.....YUKO LIKIZO NDANI YA KAUNDA SUIT........na wake WAWILI.....Resting for doing NOTHING at our EXPENSE!!!!!!!!!

  [​IMG]
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sisi bado tuko mbali sana mpaka tufike huko sio leo. Kiongozi kujishusha na kujichanganya na watu wa kawaida si rahisi sana kwani daima wanapenda waonekane wako juu; na pale wanapokuwa kati ya watu wanazungukwa kila upande na walinzi na wapambe wengine kiasi kwamba hata kumkaribia tu kiongozi ni tabu: unaweza kuambulia kipigo au kashkashi za ajabu. Ila viongozi wetu wanapokuwa nchi za nje (ulaya na marekani) inakuwa rahisi zaidi kuwashika mkono (salamu) na hata kupiga nao picha na watu wa kawaida kuliko wakiwa hapa bongo. Nakumbuka miaka ya nyuma, kwa mara ya kwanza kumsalimia kiongozi fulani mkubwa wa nchi yetu na kupiga naye picha ilikuwa huko majuu. Mambo yalikuwa poa kabisa, hakukuwa na longolongo za huku bongo. Alikuja na kuongea nasi (watanzania), tukasalimiana na kula naye na kupiga michapo. Nilishangaa! Kumbe wakiwa majuu na wao kidogo hujishusha au hushushwa na mazingira.
   
 17. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Unaijua sababu inayomfanya jirani yako kuendesha M.Benz lakini akakukopa pesa ya kununua petroli?
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Sijui yupi alikuwa 'zamu' usiku huo.....labda huyo wa msimbazi maana hata ishara ya mikono iko sawa

  [​IMG]
   
 19. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu viongozi wetu na raia wanaowaongoza ni maadui, kwahiyo hawawezi kuwa kama huyu. Wenzetu wanaishi maisha ya haki kwahiyo hawana uadui na raia wao ndo maana wana uhuru wa kuzunguka mitaani bila woga. Utakuta hata mawaziri wao wanaishi pamoja na raia wao bila hofu yoyote. Wanapanda treni na kuendesha baiskeli kama raia wa kawaida. Wa kwetu wanawaogopa raia kutokana na mioyo yao kuwasuta kwa mabaya wanayowatendea raia wao ikiwemo kujilimbikizia mali huku raia wakitaabika na maisha magumu. Rasilimali zetu wananufaika nazo wao na rafiki zao. Kwahiyo wamejijengea tabaka lao lisilochanganyikana na raia wa kawaida.
   
 20. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hizo picha za Cameron ni propaganda tupu.

  Kwanza hawana sababu ya kusafiri na budget airline even if they are paying for that holiday they are wealthy enough.

  Pili hiyo background security (bill) ya kumu-expose 'PM' kama hivyo bora angeenda panda ndege on a private ground and on a private jet.

  Then there is the security measures of where he was going, the route needs heavy survaillance.

  Yaani hii yote ni much more expensive more than an average billionaire's holiday, trust me. Hawa hawasafiri kimzaa mzaa kama akina kikwete, wanaenda na heavy security the more the leader is exposed, the more it costs the taxpayers.
   
Loading...