Waziri Mkuu amekemea Songwe, lakini ni aina tatu za watu zinatuponza

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Na Elius Ndabila
0768239284

Habari wanajamii forumu. Ni muda sijaandika hapa Zaidi ya kusoma. Nilikuwa msomaji kidogo , kwa hiyo mkiona kuna makosa kwenye andiko basi mjue ni uzee.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Majaliwa amehitimisha ziara yake ya kikazi jana Mkoani Songwe. Hotuba yake ya Majumuisho imezua mijadala mingi Kwenye mitandaoni ya kijamii hasa namna miradi ya maendeleo inavyochezewa Mkoani Songwe.

Waziri Mkuu alimkabidhi taarifa ya miradi ambayo inasuasua Mkuu wa Mkoa wa Songwe na kumpa miezi mitatu iwe imeisha.

Wananchi wameshitushwa na takwimu za miradi mingi ya maendeleo ambayo Serikali ilileta fedha tangu mwaka 2021 lakini mpaka Sasa haijaisha. Wengine wameenda mbali kwa kusema ipo miradi ambayo haijaisha lakini fedha zilikwisha isha. Tafsiri yake watu walikula fedha kabla ya mradi.

Kwenye magroup ya Whatsapp niliyojaribu kupitia mjadala huo hususani Ileje, Wananchi wanasema kama Waziri angeenda maeneo mengine ya Ileje angegundua uozo mkubwa kuliko alioondoka nao. Wananchi hao pia wamesikitika kuwa kwa nini Kila kiongozi mkubwa anapofanya ziara Ileje anapangiwa kutembelea hospital ya Wilaya ya Ileje? Je miradi mingine kwa nini Viongozi hawapangiwi hasa Tarafa ya Umalila na Undali?

Wakati ninapitia hotuba ya Waziri Mkuu na Mijadala mbalimbali ya watu, nimegundua kuna Makundi matatu ya Watu waliotufikisha hapa. Tunaweza kutumia Mkoa wa Songwe kama sampling, lakini tatizo hili la Songwe ni la nchi nzima.

Tuna Makundi matatu ya Watu yaliyotufikisha hapa. Makundi haya ni ACCORDERS, Dissenters and Latents. Ambatana nami ili ujue ni Makundi gani haya ya watu na wewe upo Kwenye kundi gani kabla hatujawalaumu Majizi wa mali za umma hasa wanaorudisha nyuma mipango ya Serikali.

1. ACCORDERS hawa ni watu ambao wanasimama na tabaka tawala kwa kitu chochote. Kila ngazi ma accorder . Wapo watu ambao Serikali ya kijiji ikifanya chochote kizuri au kibaya watatetea. Wapo ambao Viongozi wa kata wakifanya chochote kizuri au kibaya watakitetea. Wapo wengine Viongozi wa Wilaya wakifanya chochote kizuri au kibaya watatetea, halikadharika Mkoa mpaka Taifa. Hawa wapo Serikalini hata Kwenye vyama vya siasa. Yaani ukienda CCM, ukienda CHADEMA, ukienda TLP nk utawakuta ACCORDERS. Hawa accorders siku hizi kuna namna unaweza kuwafananisha na Chawa.

ACCORDERS ni watu wabaya sana, kwani hata ukikosea hawasemi. Bila kuwa na accorders basi miradi ambayo Waziri Mkuu ameikemea Jana basi watu Wema wangekuwa wameiona na kuwabana Viongozi. Lakini unaweza kushangaa Waziri Mkuu ametoka DODOMA ndiye amekuja kuanika uhuni wa watu kushindwa kusimamia vizuri fedha za umma. ACCORDERS wamewaponza. Walilewa sifa za accorders wakashindwa kusimamia miradi.
Tingekuwa na watu wakweli na wanaosimamia kweli ninaamini hii miradi isingekuwa na mkwamo huu. Nimpongeze Mhe Kyomo Diwani wa Ndola ambaye ninaweza kumtumia kama mfano bora. Pamoja na kituo chake Cha AFYA Cha Ndola kutajwa Kwenye orodha, lakini ninaamini Diwani amepambana sana kufika hapo

2: Dissenters hili ni kundi la pili ambalo kazi yake ni kupinga na kurudisha juhudi za Serikali au Chama nyuma. Kwa ufupi hawa ni Wapinzani wa kila kitu, isipokuwa wanaweza kukuunga kama utafanya kitu ambacho baadaye kitakuumiza wewe na wao kitawapa faida.

Kundi hili la watu linaweza kumfanya kiongozi kuwa njiapanda kufanya maamzi. Maana hawa kila jambo jema linapotaka kufanyika watalitafutia kikwazo ili likwame. Utafiti unaonyesha kuwa hata miradi mingi imekwama kwa sababu ya migogoro inayofanywa na hawa Dissenters. Watu wa Izyila Halmashauri ya Mbeya ni mfano mzuri wa hili ambao mpaka sasa wameshindwa kuwa na kituo Cha AFYA kwa sababu wanavutana. Hili nalo ni kundi hatari kwa maendeleo ya Taifa.

3. LATENTS hawa ni kama popo. Hawa hawaeleweki hadharani, ila gizani wanaeleweka. Kwa ufupi ni watu neutral. Hawa ni watu wabaya kuliko kundi lolote. Ni watu wanaojipendekeza kote kote. Yaani wapo katikati ya Accorders na Dissenters. Wanajua kucheza na akili za Makundi yote na wakabaki salama.

Hawa wanaweza kwenda kwa DC wakamwambia Mhe Mkuu wa Wilaya yale madarasa ya Ibaba Sekondari yamejengwa chini ya kiwango, nenda uchukue hatua. Mtu huyo huyo akitoka kwa DC anaenda kwa Injinia Makwazo anamwambia bwana taarifa za KIINTEREJENSIA zinasema DC anataka kuja kukukaanga, andaa utaratibu wa namna ya kumalizana naye. Huu ndiyo umalaya wa akina latents/neutral. Hawa ni watu wa hovyo.

Hawa hawataki ubaya na mtu hata kama yanaenda mrama. Wanaangalia masilahi yao kwanza.
Nimejaribu kutumia mifano hii ya Makundi ya watu ili niweze kujenga hoja ya kwa nini miradi mingi haiishi? Ukweli ni kuwa miradi mingi ya Serikali haiishi pamoja na Mhe Rais kutafuta fedha na kuzipeleka site kwa kuwa raia hawajui wajibu wao katika kusimamia hii miradi. Wananchi hawasomewi mapato na matumizi na hawahoji kwa kuwa wapo Kwenye Makundi hayo matatu.

Miradi yote iliyokwama ipo Kwenye ngazi za chini kabisa ambapo Wananchi wangejua wajibu wao wangekuwa wanapambana na majangili hawa wa Mali za umma mchana na usiku hata kabla ya Viongozi wakuu kufanya ziara.

Mwisho ninaomba kushauri kuwa kuwe na kitengo Maalumu Kwenye Ofisi ya RAIS au Waziri Mkuu, kitengo ambacho kazi yake itakuwa ni kupokea kero tu za Wananchi wa kawaida. Yaani liwepo Dawati Maalumu kama ilivyo Kwenye simu ambao Wana Dawati la dharura. Hilo Dawati Wananchi wapewe namba ya kupiga kunapokuwa na jambo Kwenye maeneo Yao. Wakati mwingine watu wanaogopa kutoa Taarifa Wilayani kwa kuwa wanaweza kujenga bifu. Lakini kukiwa na Dawati la kero itasaidia watu kufikisha kero na Serikali kuvamia maeneo ya kero bila hata kuwaarifu Viongozi wa kata au Wilaya. Ninaamini Serikali ikifanya hivyo itasaidia kudhibiti mikwamo mingi ya maendeleo na kuwanyima nafasi wezi.
 
Usalama wa Taifa na TAKUKURU huko chini wana kazi gani!!??
Hizi taasisi zinapaswa ziundwe upya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom