Waziri Mkuu Achangisha Bilioni 1.2 Serengeti Girls, Tembo Warriors, Asifu Ubunifu wa Wizara ya Michezo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Waziri Mkuu Achangisha Bilioni 1.2 Serengeti Girls, Tembo Warriors, Asifu Ubunifu wa Wizara ya Michezo

Na John Mapepele.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 24, 2022 amechangisha zaidi ya bilioni 1.2 kwa ajili ya kuchangia timu za Serengeti Girls na Tembo Warriors.

Harambee hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka timu hizo zichangiwe na wadau baada ya kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Duniani.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ameipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa ubunifu, usimamizi na kutangaza shughuli za michezo kimkakati.

Aidha, amewapongeza wadau wote waliochangia ambapo amesema wameonesha uzalendo wa hali ya juu na kuwa sehemu ya kuzifanya timu hizo kushinda kwenye mashindano hayo.

Katika tukio hilo mbali na kupatikana kwa ahadi ya fedha hizo, wadau wameweza kutoa tiketi za wachezaji kwenda kwenye mashindano hayo na kurejea nchini, BIMA za afya kwa wachezaji wakiwa katika mashindano hayo na vifaa mbalimbali vya wanamichezo.

Amesema kutokana na kufanya vizuri kwenye michezo ndiyo sababu Tanzania imekuwa ikipata heshima ya kuandaa matukio makubwa ya kimichezo.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya awamu ya sita (6) inaendelea kufanya jitihada kubwa za kuongeza bajeti ya kuhudumia timu za Taifa, ukarabati wa Viwanja na kuanzisha shule maalum za Michezo ili kuvumbua na kuendeleza vipaji na hatimaye kupata timu bora za Taifa.

"Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga jumla ya TSh. Bilioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa Viwanja vya majiji, TSh. Bilioni 2 kwa ajili ya ukarabati wa wa miundombinu ya michezo ya shule maalum za michezo na zaidi ya Bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vipya na kituo maalumu cha Michezo katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya" amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha,ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kukarabati viwanja viendane na sifa na matakwa ya CAF ili kutekeleza azma ya kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.
 
Attachments

  • IMG-20220825-WA0032.jpg
    IMG-20220825-WA0032.jpg
    26.6 KB · Views: 3
  • IMG-20220825-WA0029.jpg
    IMG-20220825-WA0029.jpg
    44.5 KB · Views: 3
  • IMG-20220825-WA0025.jpg
    IMG-20220825-WA0025.jpg
    34.9 KB · Views: 3
  • IMG-20220825-WA0027.jpg
    IMG-20220825-WA0027.jpg
    62.3 KB · Views: 3
  • IMG-20220825-WA0028.jpg
    IMG-20220825-WA0028.jpg
    53.9 KB · Views: 3
  • 20220825_093903.jpg
    20220825_093903.jpg
    63.9 KB · Views: 4
  • 20220825_093852.jpg
    20220825_093852.jpg
    67.4 KB · Views: 3
  • 20220825_093859.jpg
    20220825_093859.jpg
    62.5 KB · Views: 4
Waziri Mkuu Achangisha Bilioni 1.2 Serengeti Girls, Tembo Warriors, Asifu Ubunifu wa Wizara ya Michezo

Na John Mapepele.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa leo Agosti 24, 2022 amechangisha zaidi ya bilioni 1.2 kwa ajili ya kuchangia timu za Serengeti Girls na Tembo Warriors.

Harambee hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka timu hizo zichangiwe na wadau baada ya kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Duniani.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ameipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa ubunifu, usimamizi na kutangaza shughuli za michezo kimkakati.

Aidha, amewapongeza wadau wote waliochangia ambapo amesema wameonesha uzalendo wa hali ya juu na kuwa sehemu ya kuzifanya timu hizo kushinda kwenye mashindano hayo.

Katika tukio hilo mbali na kupatikana kwa ahadi ya fedha hizo, wadau wameweza kutoa tiketi za wachezaji kwenda kwenye mashindano hayo na kurejea nchini, BIMA za afya kwa wachezaji wakiwa katika mashindano hayo na vifaa mbalimbali vya wanamichezo.

Amesema kutokana na kufanya vizuri kwenye michezo ndiyo sababu Tanzania imekuwa ikipata heshima ya kuandaa matukio makubwa ya kimichezo.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya awamu ya sita (6) inaendelea kufanya jitihada kubwa za kuongeza bajeti ya kuhudumia timu za Taifa, ukarabati wa Viwanja na kuanzisha shule maalum za Michezo ili kuvumbua na kuendeleza vipaji na hatimaye kupata timu bora za Taifa.

"Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga jumla ya TSh. Bilioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa Viwanja vya majiji, TSh. Bilioni 2 kwa ajili ya ukarabati wa wa miundombinu ya michezo ya shule maalum za michezo na zaidi ya Bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vipya na kituo maalumu cha Michezo katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya" amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha,ameongeza kuwa dhamira ya Serikali ni kukarabati viwanja viendane na sifa na matakwa ya CAF ili kutekeleza azma ya kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.
Kama CCM inaweza kuchukua pesa za serikali ili ikarabati miradi yake, kwanini hawa wachangishiwe badala ya serikali kutoa fungu kwenye wizara?
 
Back
Top Bottom