Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,401
- 20,661
Hii sasa too much. Anakamatwa kwa kosa lipi?
Kama uhakiki utaonyesha hakuiba atafidiwaje? Na hao wananchi watafanywaje,? Naona kama bado tuko kwenye kipindi cha kampeni.Waziri Mkuu Majaliwa Kassim ameagiza Daktari wa Kituo cha Afya Mahuta Mtwara akamatwe, ni baada ya Wananchi kudai anahusika na wizi wa dawa kunakosababisha Wagonjwa kukosa dawa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo baada ya Wananchi kusimamisha msafara wake [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG]
Je alichofanya waziri mkuu ni sahihi? Je kama wananachi hawakuwa sahihi si atakuwa kamfedhehesha huyo daktari?
Hili si swala la imani. Lazima uthibitishe kabla ya kuchukua hatua. WM angeamuru uhakiki ufanywe halafu mhusika akamatwe ikithibitika.Wizi wa dawa na waganga wa Zahanati mkuu ni janga la taifa,kama lilivyo tatizo la matumizi mabaya ya fedha za Halimashauri na Wakurugenzi wa Wilaya.Naamini wananchi hawakukurupuka.Akamatwe tu.
una ushahidi kama kaiba au zinaibiwa,Wizi wa dawa na waganga wa Zahanati mkuu ni janga la taifa,kama lilivyo tatizo la matumizi mabaya ya fedha za Halimashauri na Wakurugenzi wa Wilaya.Naamini wananchi hawakukurupuka.Akamatwe tu.
Sawa we mkubwa,hivi si kuna registers zinazoonesha kiasi cha dawa kilichoingia na kutolewa(kutumika), je hao wananchi wana access kwa hizo taarifa au PM amejiridhisha kwa kuangalia hizo registers kisha kutoa hili agizo la daktari kukamatwa?
Hili si swala la imani. Lazima uthibitishe kabla ya kuchukua hatua. WM angeamuru uhakiki ufanywe halafu mhusika akamatwe ikithibitika.
Ninao ushahidi.Pambaf una ushahidi kama kaiba au zinaibiwa,
Hii serikali ya awamu ya tano imethibitisha kuwa haina uwezo, ila inachofanya ni "show tu". Unamsimamishaje mtumishi wa umma kwa tuhuma za kutolewa barabarani? Sawa inawezekana tuhuma hzo zikawa na ukweli (labda?), lakini kufanya kilichofanywa na PM ni kukaribisha vurugu na kudhalilishana, jambo ambalo linapunguza tija katika utendaji kazi. PM amefungua ukurasa ambapo mwananchi, kwa chuki zake tu, anaweza kumtuhumu mtumishi wa umma.Waziri Mkuu Majaliwa Kassim ameagiza Daktari wa Kituo cha Afya Mahuta Mtwara akamatwe, ni baada ya Wananchi kudai anahusika na wizi wa dawa kunakosababisha Wagonjwa kukosa dawa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo baada ya Wananchi kusimamisha msafara wake [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG]
Je alichofanya waziri mkuu ni sahihi? Je kama wananachi hawakuwa sahihi si atakuwa kamfedhehesha huyo daktari?
inaonesha una hasira sana na kikwete!Unataka kuniambia hizo registers zama za Kikwete zikikuwa hazipo? Jibu ni zilikuwepo always na bado jamaa wakawa wanakula njama kuhujumbu nchi kwa kuuziana dawa. Nilipokuwa nafanya kazi katika almashauri (jina kapuni) moja ya kazi zangu ilikuwa ni ukusanyaji data kama hizi na michezo michafu tuliijuwa na kutonya viongozi wetu. Kwa bahati mbaya hata viongozi wetu nao walihusika na ushenzi huu wa kuidanganya serikali.
Hayo ni majukumu ya taasisi zenye mamlaka za kiuchunguzi juu yake, ila waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali, alichokifanya yuko sahihi. Ni mwanakijiji gani atakayependa daktari wao mzuri, mwenye weledi na maadili aondolewe?Waziri Mkuu Majaliwa Kassim ameagiza Daktari wa Kituo cha Afya Mahuta Mtwara akamatwe, ni baada ya Wananchi kudai anahusika na wizi wa dawa kunakosababisha Wagonjwa kukosa dawa
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo baada ya Wananchi kusimamisha msafara wake [HASHTAG]#MillardAyoUPDATES[/HASHTAG]
Je alichofanya waziri mkuu ni sahihi? Je kama wananachi hawakuwa sahihi si atakuwa kamfedhehesha huyo daktari?