Waziri Ummy aagiza usajili zahanati 10 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi iItilima

Jul 20, 2016
31
27
Na Mwandishi wetu Itilima, Simiyu

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza kukaguliwa na kusajiliwa kwa zahanati 10 zilizojengwa kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi Wilayani Itilima.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha Wananchi Wilayani Itilima wanapata huduma za afya karibu na mazingira wanayoishi Ili kutimiza azma ya Serikali katika kutoa huduma bora za Afya.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo Tarehe 11 Julai 2023 Wilayani Itilima baada ya kupokea Taarifa ya Hali ya utoaji huduma za Afya Wilayani humo ambapo katika Taarifa hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Bw. Costantine Emanuel Constantine alieleza uwepo wa Zahanati ambazo zimejengwa Kwa nguvu za Wananchi ambazo bado hazijasajiliwa.

Waziri Ummy amesema zahanati hizo zianze kufanya kazi mara moja baada ya ukaguzi kukamilika na kusajiliwa.

"Tusicheleweshe mambo, ili zahanati isajiliwe lazima iwe na nyumba ya mtumishi tutaangalia namna ya kufanya lakini kwa sasa ni muhimu zahanati hizo kusajiliwa na zianze kufanya kazi mara Moja"alisisitiza Ummy.

20230712_180631.jpg
 
Back
Top Bottom