Waziri Mhagama akabidhiwa Kipande cha Sehemu ya ujenzi wa uwanja wa Mashujaa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amekabidhiwa kipande cha sehemu ya ujenzi wa uwanja wa mashujaa, katika Mji wa Serikali Mtumba, Jijini Dodoma mapema Julai 2, 2023.

Ujenzi huo unaotekelezwa na kampuni ya SUMA JKT,Umekamilisha kipande cha sehemu ya kwanza ya ujenzi wa uwanja wa Gwaride ambao unategemewa kutumika katika Maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa Julai 25, 2023.

Akiwa kiwanjani hapo Waziri Mhagama alisema, Serikali pamoja na kuhamia Dodoma imejenga miundombinu yenye hadhi ya makao Mkuu ya Serikali, na jamii inashuhudia majengo ya Serikali makubwa na miondombinu mingine ikiendelea kukamilishwa.

Akiongelea Ujenzi wa Uwanja huo, Waziri Mhagama alisema, ujenzi utakapo kamilika utakuwa ni wa mfano Barani Afrika.

"Eneo hili ni sehemu ya kwanza ya ujenzi wa eneo la maadhimisho ya uwanja wa mashujaa, hii ni Parade Ground ambayo itakuwa na Mnara wa Mashujaa,wa ubora na viwango vya juu kabisa.” Alieleza Mhe. Mgahama

Aliendelea kusema kuwa, awamu ya pili itakuwa na bustani kubwa, ambayo itakuwa na mvuto wa aina yake, na tayari Taasisi mbali mbali za Serikali zimeonesha nia ya kuwekeza na kushirikiana, kuhakikisha kutakuwa na bustani hiyo yenye migahawa, viwanja vya michezo na burudani mbalimbali, ambazo zitakuwa katika eneo hilo ambao leo amekabidhiwa kipande kidogo tuu kama sehemu ya kwanza ya ujenzi.

Alifafanua zaidi kuwa, sehemu ya tatu itahusisha ujenzi wa mnara mrefu wa zaidi mita 110 ambao utakuwa mnara wa kwanza Barani Afrika, ambao utakuwa ni kivutio kwa watalii na kuongeza pato la Taifa.

Kwa Upande Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi alisema uwanja huo utakapokamilika uteaongeza uzuri na ubora wa Jiji la Dodoma na Serikali itahakikisha kwamba mnara pamoja na uwanja wake unakuwa wa kupendeza na kuwa na mvuto wa kipekee huku akizishuruku sekta nyingine zilizoonesha ushirikiano katika utekelezaji wa ujenzi huo na kuhakikisha miundombinu muhimu inapatikana kwa wakati ili eneo hilo liweze kupata huduma hizo na kazi kwenda vizuri.

F0EJb-uXwAE2NX_.jpg
F0EJb-wWcAIUkvK.jpg
F0EKXAbXwAAEJk7.jpg
WhatsApp Image 2023-07-03 at 11.41.37.jpeg
 
"Eneo hili ni sehemu ya kwanza ya ujenzi wa eneo la maadhimisho ya uwanja wa mashujaa, hii ni Parade Ground ambayo itakuwa na Mnara wa Mashujaa,wa ubora na viwango vya juu kabisa.” Alieleza Mhe. Mgahama

Aliendelea kusema kuwa, awamu ya pili itakuwa na bustani kubwa, ambayo itakuwa na mvuto wa aina yake, na tayari Taasisi mbali mbali za Serikali zimeonesha nia ya kuwekeza na kushirikiana, kuhakikisha kutakuwa na bustani hiyo yenye migahawa, viwanja vya michezo na burudani mbalimbali, ambazo zitakuwa katika eneo hilo ambao leo amekabidhiwa kipande kidogo tuu kama sehemu ya kwanza ya ujenzi.
Kipimo cha viwango hivyo vya aina yake ni kipi
 
Back
Top Bottom