Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Mbarawa amewasilisha bajeti ya Mwaka 2022/23 na kuliomba Bunge kuidhinisha zaidi Tsh. Trilioni 3.55

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 30 leo Mei 22, 2023.



Hotuba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, akiwasilisha Bungeni mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2023/24:

Ujenzi wa madaraja 2 ya JPM (Kigongo-Busisi, Mwanza) umefikia 72%
Ujenzi wa madaraja 2 ya JPM (Kigongo-Busisi, Mwanza) umefikia 72% na kwa daraja la Pangani (Tanga) ujenzi umeanza na umefikia asilimia 3. Manunuzi ya Makandarasi kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mengine 6 yapo kwenye hatua mbalimbali. Aidha, ukarabati wa Daraja la Kirumi utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha.

Upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja 2 ya Mtera na Nzali umekamilika na kwa madaraja 4 ya Malagarasi Chini, Nguyami, Chakwale na Mbangala Upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina unaendelea.

Miradi ya barabara za mikoa iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/23 ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 103.01 zinazohusisha kilometa 61.82 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na kilometa 41.19 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.

Kazi nyingine ni kufanya ukarabati kwa kiwango cha changarawe wa barabara zenye urefu wa kilometa 1,042.43 zinazohusisha kilometa 672.77 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na kilometa 369.66 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.

Aidha, Wakala ulipanga kujenga na kufanya ukarabati wa madaraja /makalavati 31 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 44 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.

Magari 7,669,368 yamepimwa katika vituo 70 vya mizani
kuhusu udhibiti wa uzito wa magari, hadi Aprili, 2023 jumla ya magari 7,669,368 yalikuwa yamepimwa katika vituo 70 vya mizani iliyopo nchini ambapo kati ya hayo, magari 21,527 sawa na asilimia 0.28 yalikuwa yamezidisha uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito unaoruhusiwa.

Jumla ya Shilingi bilioni 5.478 zilikusanywa kutokana na tozo ya uharibifu wa barabara. Aidha, vibali 47,420 vilitolewa na jumla ya Shilingi 12,323,391,709.00 zilikusanywa kutokana na tozo ya upitishaji wa mizigo maalum.

Vilevile, Wizara kupitia TANROADS ipo katika hatua mbalimbali za kujenga mizani mpya katika mtandao wa Barabara Kuu nchini ili kudhibiti uharibifu wa barabara unaosababishwa na uzidishaji uzito wa magari.

Mizani hizo ni pamoja na mizani ya Rubana mkoani Mara ambapo ujenzi wa barabara za maingilio, majengo ya Ofisi na eneo la mizani unaendelea, mizani ya Matundasi katika barabara ya Chunya-Makongorosi mkoani Mbeya, mizani ya Bulamba katika barabara ya Bulamba-Kisorya mkoani Mara, mizani ya Igagala katika barabara ya Njombe-Moronga-Makete mkoani Njombe, mizani ya Mingoyo za upande wa pili mkoani Lindi itakayopima uzito wa magari yanayotoka mikoa ya Ruvuma na Mtwara, mizani ya Mdori mkoani Manyara ambayo itapima uzito wa magari yanayotoka Singida na Dodoma na mizani ya Kizengi mkoani Tabora.

Ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP), Wizara inaendelea na manunuzi ya Makandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Expressway kutoka Kibaha-Chalinze- Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Hadi sasa kazi inayoendelea ni uchambuzi (evaluation) wa Makandarasi walioonesha nia (Expression of Interest) ya kutekeleza mradi huu kwa sehemu ya kutoka Kibaha-Chalinze yenye urefu wa kilometa 78.9. Kwa sehemu ya Chalinze-Morogoro yenye urefu wa kilometa 126.1, Mshauri Elekezi anaendelea na kazi ya Upembuzi Yakinifu.


Barabara kiwango cha lami urefu wa kilometa 179.18 kimekamilika
Wizara ya Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ina jukumu la kusanifu, kujenga, kukarabati na kufanya matengenezo ya barabara kuu na za mikoa zenye jumla ya kilometa 36,760.29 kwa mujibu wa tathmini ya mwaka 2022.

Hadi kufikia Aprili, 2023, ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara zenye urefu wa kilometa 179.18 umekamilika na ujenzi wa kilometa 290.82 unaendelea ambapo kilometa 161.49 za tabaka la juu la msingi (basecourse), kilometa 192.03 za tabaka la kati la msingi (Sub - Base) na kilometa 259.94 za tuta la barabara zimejengwa.

Tsh. 184,459,708,389.61 zimetolewa kwa malipo ya madeni
Kutokana na malipo ya hati za madai ya makandarasi na washauri elekezi kufanyika kwa wakati, kasi ya utekelezaji wa miradi imeongezeka.

Tunaishukuru sana Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuwalipa makandarasi na washauri elekezi ambapo katika Mwaka wa Fedha 2022/23 jumla ya shilingi 184,459,708,389.61 zimetolewa kwa ajili ya malipo ya madeni.




Miradi ya madaraja/makalavati asilimia 88.82
Utekelezaji wa miradi ya madaraja/makalavati ulifikia asilimia 88.82 ambapo madaraja madogo 40 yalijengwa kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na madaraja madogo 26 yalijengwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.

Wizara ya Uchukuzi kupitia TANROADS ipo katika hatua mbalimbali za kujenga mizani mpya katika mtandao wa Barabara Kuu nchini ili kudhibiti uharibifu wa barabara unaosababishwa na uzidishaji uzito wa magari.

Mizani hiyo ni pamoja na mizani ya Rubana (Mara), mizani ya Matundasi (Chunya), mizani ya Bulamba (Mara), mizani ya Igagala(Njombe), mizani ya Mingoyo (Lindi), mizani ya Mdori (Manyara) na mizani ya Kizengi (Tabora).

Historia ya miradi mikubwa Nchini
"Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kuwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya kilometa 2,035 na ambayo itagharamu zaidi ya shilingi Trilioni 3.7 kutekelezwa kwa wakati mmoja kwa utaratibu wa uhandisi, usanifu, manunuzi, ujenzi na utafutaji wa fedha (EPC+F)"

"Kuhusu ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP), Wizara ya Uchukuzi inaendelea na manunuzi ya wa kandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Expressway kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro (KM 205). Hadi sasa kazi inayoendelea ni uchambuzi (evaluation) wa wakandarasi walioonesha nia (Expression of Interest) ya kutekeleza mradi huu"

Barabara ya Kibaha-Chalinze-Morogoro
Kutokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya waendao haraka (express way) Kibaha-Chalinze-Morogoro, hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kuwa na mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara hapa nchini ambao utatekelezwa kwa utaratibu wa PPP (ubia kati ya sekta binafsi na serikali).

Mwendokasi Mbagala 90%
"Kazi za ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka awamu ya Pili (CBD – Mbagala, Km 20.3) zimefikia asilimia 90 na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya tatu (CBD – Gongolamboto km 23.33) zimefikia asilimia 5. Taratibu za manunuzi ya mkandarasi wa kazi za ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya nne (Ali Hassan Mwinyi – Morocco – Mwenge – Tegeta na Mwenge – Ubungo (km 30.12) zinaendelea"
 
Back
Top Bottom