Mkuu Jidu, kwa matumizi ya Force Account katika utekelezaji wa miradi, Prof. Mbarawa yuko right 100%, utaratibu huu uta save time, money and resources.
Kwa kawaida miradi inatekelezwa na makampuni ya makandarasi, makandarasi hao kuleta quotations za gharama kubwa ikiwemo consultancy fee kubwa, watekelezaji wa ujenzi ni local funds ambao watalipwa fedha mdogo tuu kama vibarua, kazi ya mkandarasi ni kugundua vifaa kwa bei ya juu baada ya kuweka cha juu, kisha kuwasimamia local fundis ambao ndio wanafanya all donkey jobs.
Matumizi ya Force Account ni kuiruhusu kuwa engage hawa local fundis directly na kusimamiwa na regional engineers, hivyo kununua vifaa locally na kuanza kujenga fasta bila lengthy tendering process, na ku save money kwenye makandarasi ambao huweka cha juu kikubwa, gharama zao za juu, kupelekea mradi kuwa ghali wakati ukitumia local fundis gharama ni nusu tuu.
Changamoto pekee za utaratibu huu ni 3.
1. Sheria zinataka miradi fulani ya thamani fulani lazima isimamiwe na contractors wa viwango fulani, mfano consulting engineer, structural engineers, electrical engineers, quantity engineers, etc, sasa hawa regional engineers wanaweza?.
2. Vifaa vya quality, lengo la local fundis ni saving money not quality, vifaa quality vya ujenzi ni gharama na vinapatika maduka mahsus huku Wachina wame flood cheap counterfeit products maduka ya mitaani, ambayo kwa local fundis ndio their best option.
3. Miongoni mwa cost kubwa za contractors ni guarantee na insurance, when things go wrong, kwa kutumia local fundis, there is no guarantee na no insurance likitokea la kutokea hivyo there is nobody to cover the losses.
P