MlimaSayuni
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 7,279
- 13,681
Watu washaanza kuhofia utendaji wa Mbarawa
Mkuu umeongea kweli kiasi fulani, lakini umeongea vile vile kama mwanasiasa anayetetea jimbo au maslahi.Mkuu Jidu, kwa matumizi ya Force Account katika utekelezaji wa miradi, Prof. Mbarawa yuko right 100%, utaratibu huu uta save time, money and resources.
Kwa kawaida miradi inatekelezwa na makampuni ya makandarasi, makandarasi hao kuleta quotations za gharama kubwa ikiwemo consultancy fee kubwa, watekelezaji wa ujenzi ni local funds ambao watalipwa fedha mdogo tuu kama vibarua, kazi ya mkandarasi ni kugundua vifaa kwa bei ya juu baada ya kuweka cha juu, kisha kuwasimamia local fundis ambao ndio wanafanya all donkey jobs.
Matumizi ya Force Account ni kuiruhusu kuwa engage hawa local fundis directly na kusimamiwa na regional engineers, hivyo kununua vifaa locally na kuanza kujenga fasta bila lengthy tendering process, na ku save money kwenye makandarasi ambao huweka cha juu kikubwa, gharama zao za juu, kupelekea mradi kuwa ghali wakati ukitumia local fundis gharama ni nusu tuu.
Changamoto pekee za utaratibu huu ni 3.
1. Sheria zinataka miradi fulani ya thamani fulani lazima isimamiwe na contractors wa viwango fulani, mfano consulting engineer, structural engineers, electrical engineers, quantity engineers, etc, sasa hawa regional engineers wanaweza?.
2. Vifaa vya quality, lengo la local fundis ni saving money not quality, vifaa quality vya ujenzi ni gharama na vinapatika maduka mahsus huku Wachina wame flood cheap counterfeit products maduka ya mitaani, ambayo kwa local fundis ndio their best option.
3. Miongoni mwa cost kubwa za contractors ni guarantee na insurance, when things go wrong, kwa kutumia local fundis, there is no guarantee na no insurance likitokea la kutokea hivyo there is nobody to cover the losses.
P
Asante sana kwa ilmu hii.Mkuu umeongea kweli kiasi fulani, lakini umeongea vile vile kama mwanasiasa anayetetea jimbo au maslahi.
Utaratibu wa Serikali kuu siku zote ni kuuza kazi kwa makandarasi kwa mtindo ambao ni best practice.
Best practice ni pamoja na wote wahusika kufanya yanayopaswa ili kufanikisha mradi.
Bahati mbaya kila aliyejenga nyumba yake anaishia kufikiri ana jua sana masuala yote ya ujenzi.
Tuanze kudadavua kwanza hallmark ya mradi wa ujenzi wa kiserikali kwa njia ya zabuni.
Mara zote Client-serikali , inabuni mradi wa ujenzi ili kutatua tatizo mahsusi la kijamii, say hospital.
Client anatafuta wataalam wa kumshauri namna gani jengo litasimama, toka idea hadi kutumika kwa jengo hilo la hospitali.
Kwanza mbunifu majengo- Architect, ataanza kuchora jengo.
Baada ya hapo Engineer ata design namna bora jengo litajihimili na kusimama.
Engineers wengine wa huduma, services, watachora umeme, maji,vipooza hewa, na funiture fittings.
Baada ya hapo ni ukadiriaji gharama za ujenzi inayofanywa na Quantity Surveyor.
Hivyo basi GHARAMA ZA UJENZI ZINAFAHAMIKA HATA KABLA YA KUANZA KAZI.
Hivyo mtu anayesema makandarasi wanajaza gharama za juu, hajui utaratibu wa kufikia gharama za ujenzi, na Pasco hili linakuhusu.
Baada ya gharama(estimates) kufahamika ndipo tender huitishwa ili kupata mkandarasi atakayekidhi masharti ya kazi.
Mkandarasi atakaye shinda lazima akidhi viwango ikiwa ni pamoja na dhamana ya kazi(performance bond) ambapo mkandarasi huwa ameweka nyumba kama dhamana.
Na mkandarasi akitaka advance payment ataongeza dhamana ya nyumba nyingine bank(Advance payment Bond).
Hivyo kwa serikali hakuna namna inaweza kupata hasara maana dhamana huwa wamezishikilia.
Na pindipo mkandarasi atajapo shindwa kazi dhaman hizo huuzwa.
Huo ndo utaratibu wa ujenzi wa miradi ya umma duniani kote.
Matatizo ambayo ma layman(na layman anaweza kuwa kiongozi) hawayaoni, na yanawaathiri vibaya makandarasi , ni pamoja na serikali kutokuwa na hela za mradi.
Mara zote serikali inapokuwa haina fedha za miradi, au fedha inatolewa kwa kusua sua, anaye athirika moja kwa moja ni mkandarasi.
Kama mkandarasi amekopa benki ili afanye mradi wa serikali na serikali HAINA fedha au inalipa kwa kusuasua sana, benki wanauza nyumba ya dhamana.
Umasikini kama huu umewakuta makandarasi wengi tayari.
Tatizo lingine ni wataalam wasimamizi kutofika kabisa eneo la mradi.
Tukumbuke kuwa michoro ya miradi ni mistari tu kwenye karatasi iliyochorwa na wabunifu.
Kuelezea maana halisi ya mstari kwenye karatasi ni jukumu la mchoraji na msimamizi.
Hso wasipokuwepo eneo la mradi wakati wote, kwa sababu yoyote ile kazi inasimama.
Hivyo Pasco unapo hadhithia ujenzi as if watu wako pale kula tu na kucharge bei nzito nzito, hiyo ni laymans point of view.
Kwa maelezo haya marefu Wizara ya Maji kuamua kujitwika ujenzi kwa matamko ya hadharani, hapo si tu tuwaonee huruma kuwa hawajui watendalo bali tuwaombee vile vile.