the deadline
Member
- Sep 26, 2013
- 62
- 106
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano - Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika uwanja wa ndege wa Chato wenye kiwango cha daraja la 4C unaojengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 39.15.
Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliofanyika Novemba 4 , 2017, Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa kiwanja hicho unaojengwa na mkandarasi Mtanzania kinajengwa kwa kiwango cha kimataifa.
“Tunahitaji maendeleo na serikali hii imefufua shirika la ndege na tayari imenunua ndege sita ambazo zitafanya kazi ndani na nje ya nchi na kila mkoa utakua na kiwanja cha ndege cha kisasa kitakachohudumia wananchi wasiopungua 100” amesema.
Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini(TANROADS) Patrick Mfugale amesema kiwanja hicho kina urefu wa kilometa tatu ambapo kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 hadi 300.
Ujenzi huo ulioanza Septemba 2016 umeshajengwa kwa asilimia 52 na unategemewa kuchochea shughuli za maendeleo katika wilaya ya Chato na mkoa wa Geita kwa ujumla.
=======
My Take:
JE KULIKUWA NA UMUHIMU WA UWANJA ULE WILAYANI CHATO KUWA TAYARI KATIKA KARNE HII WAKATI UWANJA WA MWANZA BADO NI MDOGO NA HAUSAPOTI NDEGE KUBWA?