Waziri Mbarawa aweka jiwe la msingi ujenzi Uwanja wa Ndege Chato. Kuligharimu Taifa Sh. Bilioni 39

the deadline

Member
Sep 26, 2013
62
106
PIC+CHATO.jpg


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano - Profesa Makame Mbarawa ameweka jiwe la msingi katika uwanja wa ndege wa Chato wenye kiwango cha daraja la 4C unaojengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 39.15.

Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliofanyika Novemba 4 , 2017, Waziri Mbarawa amesema ujenzi wa kiwanja hicho unaojengwa na mkandarasi Mtanzania kinajengwa kwa kiwango cha kimataifa.

“Tunahitaji maendeleo na serikali hii imefufua shirika la ndege na tayari imenunua ndege sita ambazo zitafanya kazi ndani na nje ya nchi na kila mkoa utakua na kiwanja cha ndege cha kisasa kitakachohudumia wananchi wasiopungua 100” amesema.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara nchini(TANROADS) Patrick Mfugale amesema kiwanja hicho kina urefu wa kilometa tatu ambapo kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 hadi 300.

Ujenzi huo ulioanza Septemba 2016 umeshajengwa kwa asilimia 52 na unategemewa kuchochea shughuli za maendeleo katika wilaya ya Chato na mkoa wa Geita kwa ujumla.

=======
My Take:

JE KULIKUWA NA UMUHIMU WA UWANJA ULE WILAYANI CHATO KUWA TAYARI KATIKA KARNE HII WAKATI UWANJA WA MWANZA BADO NI MDOGO NA HAUSAPOTI NDEGE KUBWA?
 
Kama 20km toka uwanja,Tunahifadhi kubwa ya Kisiwa cha Rubondo,kina wanyama wengi,samaki,ndege aina nyingi.Pia itapunguza garama,muda msafara mkuu wa nchi.Hii nchi si maskini ni huduma ya msingi kutanua fursa na maeneo mengine
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom