Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Mimi binafsi ni mfuasi wa ushirikiano na watu wengine, siamini kabisa kwenye kujitenga. Hivyo hatua yoyote inayochukuliwa kuimarisha mahusiano naunga mkono 100%
Ni kweli mahusiano yetu hayakuwa mazuri kwa kupind Cha awamu iliyopita ya yule mtu.
Lakini haimaanishi sasa kila kitu tutegemee wengine, tulishaona pia madhara yake huko siku za nyuma.
Kwenye suala la umeme nimeona mh. Makamba akienda kuzungumza na ubalozi wa US pamoja na ubalozi wa Uholanzi kwa lengo la kusaidia uwekezaji kwenye umeme.
Hapa ndio naona tatizo lipo, ni kweli kabisa kweye umeme hatuwezi kujitegemea wenyewe? Hatuwezi kuzalisha umeme wenyewe?
Bado nashinda kuelewa dhana nzima ya kuomba uwekezaji kwenye umeme ni nini, ni lini kwenye mambo Kama haya tutaacha utegemezi?
Yalishatokea miaka ya nyuma makampuni Kama symbiom na Dowans kuifilisi Tanesco, tunataka tena turudi huko?
Kwanini mikakati isiwe kuifanya Tanesco ijitegemee badala ya kutegemea makampuni ya nje kuja kuwekeza huku yakiishia kuifilisi Tanesco kwa mikataba ya ajabu?
Ninaamini kwenye umeme tunaweza wenyewe Kama watanzania, hivyo kuomba uwekezaji kwa mataifa ya nje sio sahihi.
Kwenye sekta ya uchimbaji gesi nauunga mkono uwekezaji kwa kuwa bado hatupo vizuri eneo hilo, Ila uwekezaji kwenye kutuuzia umeme Hapana.