Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Hapo nimekuelewaBwawa la nyerere likisimamiwa tutapata umeme wa kutosha sema watu wanaandaa mazingira ya upigaji
Kwa hio jamaa anazunguka kwenye mabalozi ili kupata mchongo
Hapo nimekuelewaBwawa la nyerere likisimamiwa tutapata umeme wa kutosha sema watu wanaandaa mazingira ya upigaji
Bado lipo hai hilo bandiko au mods wamepita nalo?Kuna bandiko liliwekwa asubuhi na mtu mkamuona kama mpuuzi ila alikuwa na point tena mambo aliyozungumza ndio haya haya ambayo Makamba anaelekea kuyafanya!
Mimi binafsi ni mfuasi wa ushirikiano na watu wengine, siamini kabisa kwenye kujitenga. Hivyo hatua yoyote inayochukuliwa kuimarisha mahusiano naunga mkono 100%
Ni kweli mahusiano yetu hayakuwa mazuri kwa kupind Cha awamu iliyopita ya yule mtu.
Lakini haimaanishi sasa kila kitu tutegemee wengine, tulishaona pia madhara yake huko siku za nyuma.
Kwenye suala la umeme nimeona mh. Makamba akienda kuzungumza na ubalozi wa US pamoja na ubalozi wa Uholanzi kwa lengo la kusaidia uwekezaji kwenye umeme.
Hapa ndio naona tatizo lipo, ni kweli kabisa kweye umeme hatuwezi kujitegemea wenyewe? Hatuwezi kuzalisha umeme wenyewe?
Bado nashinda kuelewa dhana nzima ya kuomba uwekezaji kwenye umeme ni nini, ni lini kwenye mambo Kama haya tutaacha utegemezi?
Yalishatokea miaka ya nyuma makampuni Kama symbiom na Dowans kuifilisi Tanesco, tunataka tena turudi huko?
Kwanini mikakati isiwe kuifanya Tanesco ijitegemee badala ya kutegemea makampuni ya nje kuja kuwekeza huku yakiishia kuifilisi Tanesco kwa mikataba ya ajabu?
Ninaamini kwenye umeme tunaweza wenyewe Kama watanzania, hivyo kuomba uwekezaji kwa mataifa ya nje sio sahihi.
Kwenye sekta ya uchimbaji gesi nauunga mkono uwekezaji kwa kuwa bado hatupo vizuri eneo hilo, Ila uwekezaji kwenye kutuuzia umeme Hapana.
View attachment 1968979View attachment 1968980
Sijui kama lipo hai maana title ilikuwa ina umagufuli flani katika phraseBado lipo hai hilo bandiko au mods wamepita nalo?
Ni ipi ya kigeni iliwahi kufanikiwa zaidi ya kutunyonya? Ni IPTL,SIMBION au DOWANS kwa ufahamu wangu wote walikuwa majizi ya kutamalaki mnataka kuturudisha huko? Safari hii tunanyie.Ni kampuni gani ya Serikeli iliwahi kufanikiwa?
Si kweli hapa unaweka madoido ili kurahisisha upigaji wenuSiyo rahisi kuacha utegemezi. Sera nyingi za nchi ambazo zinagusa uchumi huwa zinatengenezwa nje ya nchi. Zinapendekezwa na World Bank, IMF, na nchi zinazotoa mikopo na misaada. Ukiona serikali inakaribisha uwekezaji kwenye sekta fulani ujue ni lazima World Bank wamependekeza serikali wafanye hivyo. Na serikali haina nguvu ya kupinga. Nyerere mwenyewe alishindwa. Alikuwa hai anaangalia Mwinyi anauvuruga ujamaa wake, anaufungua uchumi, anabinafsisha mashirika ya umma. Nyerere akabaki kukasirika na kuona Mwinyi anaitwa Mzee Rukhsa. Alichofanya Mwinyi reforms zilizopendekezwa na Benki ya Dunia ili waendelee kuikopesha Tanzania. Kwa hiyo chochote watakachopendeza hao wakopeshaji wetu lazima tutakifanya.

Very useless .Spot on. January is useless.