Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,510
- 7,755
"Siku moja hapa umeme umekatika Bungeni, kumetokea hitilafu. Ghafla bwana “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe kuja kuchunguza waala!.
Umeme umekatika kwenye uwanja wa mpira, “fukuza Waziri, fukuza TANESCO”. Kumbe ni mambo mengine. Jamani, sio wakati wote ni TANESCO, sio wakati wote ni Wizara.
Sisi tutachukua wajibu wetu pale inapotokea” Waziri wa Nishati, January Makamba.
Haya maneno yanatuongezea hamu na hamasa ya kupata matokeo. Sisi hamasa yetu ni imani ya Mheshimiwa Rais kwetu, hamasa yetu ni matokeo ya kazi yetu kwa uhai wa chama chetu.
Hamasa nyingine ni kuwasaidia Watanzania kwa majukumu tuliyopewa. Lakini hamasa ya mwisho ni maneno haya, mtu akikusema wewe hufai maana yake unajitahidi ili uonekane unafaa. Kwa hiyo haya maneno yanatusaidia. Lakini pia haya maneno yanatusaidia kwa sababu yanawaamsha wanaotupenda na wanaotutakia heri ili watuombee dua na sala.”- Waziri January Makamba
“Maneno haya yanatusaidia kwa sababu yanatufundisha ukomavu, yanatufundisha kuwa na subra, yanatufundisha kuwa na uvumilivu na yanatujenga kuwa viongozi bora zaidi. Sisi tumesema waendelee kwa sababu yanatusaidi. Sisi kisasi chetu ni MATOKEO. Hatutabishana, hatutatupa maneno, hatutajitetea, tutalipa kisasi kwa matokeo” Waziri wa Nishati, January Makamba.