Waziri Maige kapata wapi 500M za kumwaga jimboni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Maige kapata wapi 500M za kumwaga jimboni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Martinez, Jan 6, 2012.

 1. M

  Martinez JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  :A S embarassed:
  KAHAMA, 05 Jan 2012

  MBUNGE wa jimbo la msalala wilayani kahama, mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige ametoa shilingi milioni 500, zilizozutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
  Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii amesema fedha hizo zimetumika kuboresha elimu katika shule za sekondari za kata, barabara na ujenzi wa zahanati za vijiji.
  Akizungumza katika kata ya Busangi, Waziri Maige amesema fedha hizo zimetumika kujenga Mabweni kwenye shule ya sekondari ya kata ya Isaka, Lunguya na Segese na madawati300 yaliyogawiwa kwenye shule tisa za sekondari katika jimbo la msalala.
  Amesema katika fedha hizo, pia zimesaidia ununuzi wa mifuko 1200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za vijiji pamoja na ufungaji umeme wa Sora kwenye shule ya sekondari ya kata ya Ntobo na Ngaya pamoja na utafiti wa majiya visima virefu kwenye vijiji 32.
  Kutokana na idadi ya ufaulu kuongezeka wilayani kahama, Waziri Maige amewataka wananachi kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa madarasa mapya ya shule za sekondari.

  Maswali ya Kujiuliza

  1. Kapata wapi fedha hizo Milioni 500TZS ?
  2. Je, hayo siyo majukumu ya serikali ?
  3. Vipi sehemu ambazo hazina watu matajiri kama Maige ?
  4. Je, hili haliwezi kujenga hali ya serikali kuachia wabunge majukumu yake ?
  5. Je, hili haliwezi kupelekea wabunge wengine wenye nafasi kushindana kuiba ili nao wapeleke majimboni kwao?

  NB: Tukumbuke moja ya kazi za Mbunge ni kuongoza shughuli za maendeleo kutokana na fedha zinazotolewa na Serikali, na sio kugharamia shughuli za maendeleo.

  ...
   
 2. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,
  Kuna dili ngapi zinapigwa maliasili?
  Nani anayegawa vitalu vya kuwinda?
  Mgao wa Jairo huwa haufiki kwa mawaziri?
  Jibu liko wazi na Jepesi sana tu
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Moja kati ya wizara ambazo kila MBUNGE angependa kuteuliwa kuiongoza ni hii ya MaliAsili na Utalii.
   
 4. K

  Kinto Senior Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Why kuwa so sceptic jamani kwa mbunge kusaidia maendeleo jimboni kwake? si afadhali hata kama kapiga hayo madili AT LEAST ametumia kwa shughuli za kuwasaidia wananchi? Bila taarifa za uhakika kuwa hizo pesa ni za ki magumashi mjadala huu utakuwa ni wa kutengeneza majungu, kutomtendea haki maige na kushusha integrity ya JF. Kwani hizo milioni 500 amezitoa kwa kipindi gani? Ina maana Maige hawezi kuwa na milioni 500? level yake ni kuwa na milioni ngapi?
  Bila kujali zimetoka wapi, mie nampongeza Maige kwa kazi kubwa aliyoifanya ambayo haina ubishi.
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye red you don't know what you are saying,..kama katoa m.500,yeye kajibakishia mabilioni mangapi?mtumishi wa umma wa level yake mshahara ni milion 2.5 kabla ya makato..hizo hela kazipata wapi?huyu achunguzwe
   
 6. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Jamani mgao wake wa wale vifalu na Tembo wetu walieonda kula tende na haluwa Oman kupitia KIA.
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  We shukuru tu hii nchi ni shamba la bibi otherwise usingeongea huu upuuzi. Kama sheria zingekuwa zinafuata huyu Mige angekuwa under scrutiny tujua kapata wapi hiyo fedha na kipato chake ni kipi. Kwa haraka haraka kwa kipato alichotangaza hapo Mh Maige alitakiwa KULIPA KODI YA MAPATO TRA ISIYOPUNGUA SHILINGI MILIONI 200 KWA KIPINDI HICHO CHA MWAKA MMOJA. JE AMELIPA KIASI HICHO CHA KODI YA MAPATO? KAMA HAJALIPA INA MAANA KIPATO CHAKE HICHO CHOTE SI HALALI, NCHI ZA WENZETU SAIZI ANGEKUWA ANACHEKEA CHOONI...
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  inatakiwa ieleweke wazi kua mbunge kazi yake si kugharamia shuhuki za maendeleo jimboni ni kusimamia maendeleo yaliyopangwa na serikali kuu au fedha za wahisani si kutoka mfukoni kwake, kwa kufanya ivyo anataka kutengeneza dhana kwamba ili kua mbunge pre requisite ni uwe tajiri so kiongozi hata kama ni mzuri ila akiwa maskini basi hana nafasi ya kua mbunge! mwisho kabisa mapato yake halalia kwa kipindi chote atachokua mbunge hayafiki mil 500 yeye kazipata wapi? kama ni kwa wqafadhili kuna utaratibu wa kuzipeleka maeneo husika si kuzitoa kana kwamba zinatoka mfukoni mwako!
   
 9. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Kazipatia labda pale Airpot GGM
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Maige hayuko peke yake. Kila siku tunasoma kwenye mageziti jinsi viongozi mbalimabli (vyama vyote vya siasa) wanavyomwanga misaada. Swali la kujiuliza, wanapata wapi pesa? Na huyo anayewapa pesa anapata nini in-return? Tunavyoongea umatonya sio tu kwenye serikali kuu bali hata kwa wabunge. Nadhani tume ya maadili ingetakiwa kuangalia kwa kina misaada ya viongozi inapatikanaje na kwa nia gani? Hakuna lunch ya bure hivyo tusishangilie sana hii misaada bila kujua kama tunaweka nchi rehani. Tayari wanyama wanasafirishwa, madini yanazidi kuchimbwa, lakini sisi tunapiga vigelegele kupewa vyandarua vya mbu!
   
 11. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Akiruhusu kusafirisha tembo moja, chui moja ,simba moja fisi moja, twinga moja, pumdamilia moja , nyati moja, kiboko moja, nyani moja, mamba moja na,,,,,,,,,,,,,,,,moja moja wakiwa hai hiyo TZS 500 million mbona inapatikana kirahisi tu jamani
   
 12. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kwani mapato ya TANAPA, Ngorongoro na Vitalu vinaenda wapi na zina udhibiti kiasi gani?
   
 13. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Yaani muda unapotea kuuliza kazipata wapi? Kwa nini muda usitumike kufikiri zingine zaidi zitatoka wapi, viongozi wa namna hii ndio wa kupigiwa mfano mkono mtupu haulambwi na maendeleo ni fedha. Kwa umaskini tulionao kiongozi lazima aweze kutafuta pesa kwa ajili ya watu wake na kuwawezesha wao wenyewe kupiga hatua na si kujaza thread JF.

  Pesa za magumashi asingezitangaza, na wanasiasa wanajumlishaga na pesa za wafadhili, marafiki, serikali na hata michango ya wananchi kusema wametoa wao. Na ndio maana USAID wanaongezea kutoka kwa watu wa marekani. Kuna wengine wabunge toka uhuru lakini wanapiga hela wao na familia zao na vimada wao tu.

  Kuna Jembe lingine liko moshi mjini - Chadema, issue za wananchi anamaliza mwenyewe kitambo tu mbona hajaulizwa anatoa wapi pesa - Mzee NDESA
   
 14. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kwani mapato ya TANAPA, Ngorongoro na Vitalu vinaenda wapi na zina udhibiti kiasi gani?
  Kwa hiyo tusishangae Waziri akichangia 500m/=
   
 15. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wizara ya mali ya siri na uizi
   
 16. K

  Kinto Senior Member

  #16
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sawa kaka... u know what you are saying....mie nasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni ikiwa ni pamoja na kumpongeza kwa kazi alizofanya jimboni...hii haizuii kufanyika kwa uchunguzi, lakini kuanza kumtupia mawe kwa dhambi ambayo haijathibitika si kumtendea haki...kwa sasa tumpongeze kwa kazi nzuri aliyofanya ambayo ni dhahiri...naomba kujibiwa maswali haya:-
  Hizo mil 500 alizotumia ni kwa kipindi gani?
  Maige hawezi ku raise mil 500 kwa njia halali (ukiacha salary yake)?anayemjua vizuri aseme.
  Kuna uhakika gani kama hakuna charity organization yoyote ya ndani au nje ya nchi ambayo under hizi influnce inaweza kuwa imemsaidia?
  I am not ready to condemn haya aliyofanya mpaka uchunguzi utakapofanyika nakuthibitisha kuwa hakupata hizi fedha kihalali. Ni dhambi kumtuhumu mtu kwa hear says.
   
 17. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nduguyangu unauliza nini uoni wanyama wanavyosafirishwa kwenda uarabuni na mahotel yanavyoporomoshwa kwenye mbuga
   
 18. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia zote. Mh. MAIGE si mwizi, angekuwa kafanya hivyo asingetangaza. Kitendo cha Maige kutoa pesa hiyo yeye si wakwanza, tumeona na kusikia wabunge wa maeneo kadhaa nchini wakitoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya majimbo yao. Isitoshe Mh. Maige ana marafiki wengi UK na USA ambao wengine nimewaona kwa macho yangu wakileta msaada wa vitabu vya mamilioni ya fedha kwa wanafunzi wetu wa sekondari. Nafikiri mtoa hoja aondoe mawazo hasi kwa Mh.Maige. Ok...!
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  mnataka azile mwenyewe? kapata ndio bora kala na wananchi
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,530
  Trophy Points: 280
  kapata kwenye twiga, tembo, konokono, vipepeo, d. cameroon n.k.
   
Loading...