Waziri Maige kapata wapi 500M za kumwaga jimboni?

:A S embarassed:
KAHAMA, 05 Jan 2012

MBUNGE wa jimbo la msalala wilayani kahama, mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige ametoa shilingi milioni 500, zilizozutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii amesema fedha hizo zimetumika kuboresha elimu katika shule za sekondari za kata, barabara na ujenzi wa zahanati za vijiji.
Akizungumza katika kata ya Busangi, Waziri Maige amesema fedha hizo zimetumika kujenga Mabweni kwenye shule ya sekondari ya kata ya Isaka, Lunguya na Segese na madawati300 yaliyogawiwa kwenye shule tisa za sekondari katika jimbo la msalala.
Amesema katika fedha hizo, pia zimesaidia ununuzi wa mifuko 1200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za vijiji pamoja na ufungaji umeme wa Sora kwenye shule ya sekondari ya kata ya Ntobo na Ngaya pamoja na utafiti wa majiya visima virefu kwenye vijiji 32.
Kutokana na idadi ya ufaulu kuongezeka wilayani kahama, Waziri Maige amewataka wananachi kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa madarasa mapya ya shule za sekondari. ...

hawa jamaa wamechakachua mahesabu, hizo ni zahanati ngapi? hiyo mifuko mingi sana
 
Kwani wale twiga washarudi? Tembo,chui,vifaru walisharudishwa kwani? Nani anayeidhinisha ugawaji wa vitaru? Tanapa ipo chini ya wizara gani? Mahoteli yanayojengwa kwenye mbuga za wanyama nani anaidhinisha ujenzi na upatikanaji wa viwanja? Tozo ya utalii na wageni nani wanaokusanya?

You have all the answers!!!
 
Ndio maana JK alisema kwamba uwaziri hausomewi.

Sincerely speaking mimi wala sielewi huyo bwana kama waziri anafanya kazi gani. Sioni impact yake, yupo kama hayupo, haina tofauti.
wakenya, very proudly wanasema kwamba Mt. Kilimanjaro uko kwao, Serengeti is part of Kenya. If he intelligent enough, those are some of the areas he should make impact. Still, jamaa, anajionyesha kwa kutoa pesa yote hiyo ili kuwatisha wanaotaka Ubunge 2005!

Baadhi ya Mawaziri wa JK! Sijui hata amewapata wapi!
 
Back
Top Bottom