Waziri Maige kapata wapi 500M za kumwaga jimboni?

mwizi huyo! biashara gani zisizojulikama hizo? tatizo mitaji ya biashara za viongozi wa nchi hii, zinatokana na pesa za umma. Pia awalipi kodi kikamilifu na biashara zao azikaguliwi, kwa kuwa wao ni waheshimiwa. Baada ya dhurumat hiyo wanajifanya kutoa msaada kwa wananchi.
 
Toka apate uwaziri Misitu hata ile ilikuwa inaitwa Virgin Forest inavunwa kwa hasira kubwa na wamanga na wachina kwa asilimia 50 baada ya miaka minne ijayo hakuna Misitu ya banuai tena kwa ajili ya uwizi wa waziri Maige kiwavi Nzige mkubwa

Mbuga ya seloes yenye tembo wa kipekee wamevunwa nusu toka kwenye 73,000 -2006 -mpaka 23 na kitu hivi mwaka jana ,mtu huyo muuaji mkubwa anasimamia maslahi ya aliyemuweka hapo
Dege limekimbia na wanyama mpaka Twiga nembo ya taifa letu

Mwizi anawarubuni wananchi kwa milioni 500 wakati yeye labda anabilioni 20
upupu mtupu
 
Maajabu ya wanasiasa wengi wa nchi hii huyu jamaa akipigwa chini ubunge na uwaziri ukikutana nae baada ya miezi 6 kachoka mbaya! Sasa jiulize hizo 500M. kazitoa wapi. Rushwa tu!
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia zote. Mh. MAIGE si mwizi, angekuwa kafanya hivyo asingetangaza. Kitendo cha Maige kutoa pesa hiyo yeye si wakwanza, tumeona na kusikia wabunge wa maeneo kadhaa nchini wakitoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya majimbo yao. Isitoshe Mh. Maige ana marafiki wengi UK na USA ambao wengine nimewaona kwa macho yangu wakileta msaada wa vitabu vya mamilioni ya fedha kwa wanafunzi wetu wa sekondari. Nafikiri mtoa hoja aondoe mawazo hasi kwa Mh.Maige. Ok...!
Mzee usikurupuke kinachotakiwa kwa viongozi wetu hasa karne hii ni uwazi (transparency), kama kapokea misaada au kakopa benki au biashara zake zimemwingizia hana budi kuonyesha kwenye fomu za mapato na matumizi yake na mali alizonazoa na je amelipa kodi inavyostahili, ili kumfanya kuwa wazi zaidi kwa wapiga kura wake.. kwakifupi kiongozi wa level yake nchini hapa kuweza kutoa 500million kuna mashaka makubwa sana hivyo hana budi kututoa hofu
 
Kabla ya kuanza kujibu maswali yako mepesi naomba kumpongeza mheshimiwa Mbunge kwa ujasiri wake wa kugawana alichovuna (kimagumashi) na wanachi wake. nashauri wabunge/mawaziri wengine kuiga mfano huu

Tujibu maswali

Maswali ya Kujiulizaa
1. Kapata wapi fedha hizo Milioni 500TZS ?
-Maliasili kuna dili nyingi sana. kwani umeisahau ile biashara ya kusafirisha wanyama pori kwa ndege kwenda nje ya nchi, vitalu vya uwindaji, magogo, posho na safari za kiana. hawa mawaziri wakisafiri wanapata posho mara mbili au zaidi (mfano serekalini ambae ndiyo mwajiri na shirika husika na safari hiyo) n.k
2. Je, hayo siyo majukumu ya serikali ?
-kuleta maendeleo ni jukumu la kila mwananchi ndiyo maana hata kina Reginald Mengi wanachangia maendeleo kwenye jamii
3. Vipi sehemu ambazo hazina watu matajiri kama Maige ?
- Hao itakuwa imekula kwao kama vp wahamie kwa Maige
4. Je, hili haliwezi kujenga hali ya serikali kuachia wabunge majukumu yake ?
-Hapana kwanza ndiyo vizuri kwa kuwa hela zote hizo ni za serekali ila zimepitia kwa third part kwa muda tu
5. Je, hili haliwezi kupelekea wabunge wengine wenye nafasi kushindana kuiba ili nao wapeleke majimboni kwao?
- Tayari limewezekana kwani kwani mbunge wenu hatoi mgao?
 
Akiruhusu kusafirisha tembo moja, chui moja ,simba moja fisi moja, twinga moja, pumdamilia moja , nyati moja, kiboko moja, nyani moja, mamba moja na,,,,,,,,,,,,,,,,moja moja wakiwa hai hiyo TZS 500 million mbona inapatikana kirahisi tu jamani

Nisawa kabisa hujakosea, hebu fikiri kapata wapi? kama wana Jf mtakuwa na kumbukumbu yule kifaru mweusi alie nunulia south africa, alinunuliwa kwa shl ngapi? Mtagundua kuwa hiyo pesa ni ndogo sana kwa mtu huyo. kwanza hata twiga hajagusa kachukua mbega na nyegele tu.
 
Kwani wale twiga washarudi? Tembo,chui,vifaru walisharudishwa kwani? Nani anayeidhinisha ugawaji wa vitaru? Tanapa ipo chini ya wizara gani? Mahoteli yanayojengwa kwenye mbuga za wanyama nani anaidhinisha ujenzi na upatikanaji wa viwanja? Tozo ya utalii na wageni nani wanaokusanya?
 
Hizi fedha zitakua ni za mfuko wa maendeleo jimboni. Wabunge wengi hutumia hizi fedha as if ni mchango wao. Huwaambia wananchi kuwa wao ndo wamezitoa ili kujiongezea umaarufu
 
MBUNGE wa jimbo la msalala wilayani kahama, mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige ametoa shilingi milioni 500, zilizozutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii amesema fedha hizo zimetumika kuboresha elimu katika shule za sekondari za kata, barabara na ujenzi wa zahanati za vijiji.
Tunakoelekea si kwamba tu ni a wrong direction.

Bali tumeshafika ambapo sipo tulipotakiwa tuwepo!

Hakutakuwa na mabadilko kama hatutaanza upya kabisa!

Yani ccm na serikali waondolewe kwa nguvu halafu kila walichokifanya kiwe undone! ie mikataba, kujiuzia nyumba za umma nk.

Otherwise hata tukiwaondoa kwa kura, haitasaidia kwasababu mikataba ya kuwanufaisha wao, itakuwa ikiendelea kwa mujibu wa sheria.

So kuwabadilisha haitakaa isaidie!
 
SIDHANI KAMA KUNA SEHEMU KUNA UFISADI WA KUTISHA KAMA MALI ASILI NA UTALII.

- 1. TUKIANZA NA MALIASILI
- Magogo yanavyotoroshewa nje kimagendo
- Uwindaji, hapa kwenyeuwindaji kuna ufisadi wa kufa mtu, HAWA JAMAA WANAPIGA HATA WANYAMA WASIOLUHUSIWA KUUWAWA KAMA TWIGA NA KAZALIKA
- KULE LOLIONDO ILEKAMPUNI YA OBC, WALE WARABU WANAWINDA KWA KUTUMIA HELCOPTA KITU AMBACHOHAKIRUHUSIWA KABISA, NA WANA UWANJA WAO WA NDEGE PRIVATE WA KUSAFIRISHIAWANYAMA HAI NA WALIO UWAUWA, NA ULE UWANJA INGAWA HAUNA LAMI LAKINI RUN WAYYAKE NI KUBWA KULIKO YA KIA NA ULE WA DR

- Kutorosha wanyamakwenda nje.
HII NDO KAZI INAYOFANYWA NA MALIASILI, MAGARI YAO NDO HUWA YANATUMIKA KUBEBA MAGENDO KAMA MENO YATEMBO, NGOZI ZA CHUI, PUNDAMILIA NA TWIGA,

- WANAO SAFIRISHAHUTUMIA MAGARI YA MALIASILI

- NJIA YA ARUSHA - KIAHAPO KAYIKATI KUNA WARABU WAMEJENGA KITUO CHA KUKUSANYA KILA AINA YA NDEGEWANAOPATIKANA TANZANIA NA KUWASAFIRISHA NJE YA NCHI KUPITIA KIA.

2. UTALII
- Hapa napo kunaufisaidi wa karne- TANAPA NA NGORONGORO WANAFANYA WIZI WA WAZIWAZI LAKINISERIKALI INAWAKINGIA KIFUA,
- ZILE PAYCARD ZAGETINI KUNA WIZI MKUBWA SANA UNAFANYIKA PALE LAKINI SERIKALI IKO KIMYA KANAKWAMBA HAWAJUI.

 
Katika kitu kama hii ndipo unapotegemea kuona TRA wanafanya kazi ya kuprove kuwa wanapinga kwa nguvu zote wakwepa kodi.
 
What????? Ni sahihi kulisaidia jimbo lako lakini mimi nachouliza kila siku kwa nini iwe ni mtu binafsi anafanya hivyo na si serikali? Huu mtindo wa kusaidia majimbo ni kujinadi lakini serikali ilipashwa kuuliza wanapata wapi pesa zote hizi? Hii nchi bana ina mazingaombwe acha kabisa
 
Why kuwa so sceptic jamani kwa mbunge kusaidia maendeleo jimboni kwake? si afadhali hata kama kapiga hayo madili AT LEAST ametumia kwa shughuli za kuwasaidia wananchi? Bila taarifa za uhakika kuwa hizo pesa ni za ki magumashi mjadala huu utakuwa ni wa kutengeneza majungu, kutomtendea haki maige na kushusha integrity ya JF. Kwani hizo milioni 500 amezitoa kwa kipindi gani? Ina maana Maige hawezi kuwa na milioni 500? level yake ni kuwa na milioni ngapi?
Bila kujali zimetoka wapi, mie nampongeza Maige kwa kazi kubwa aliyoifanya ambayo haina ubishi.


Mkuu jaribu kusoma vizuri post! Hizo hela ametoa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Alikuwa akielezea mafanikio na mchango wake katika jimbo. Suala la msingi ametoa wapi hizo hela na kwa kipindi cha mwaka mmoja tu? Nashangaa hata waandishi wana report tu Maige amwaga mamillion ya hela jimboni lakini hawamuulizi ametoa wapi hela zote hizo? Aseme alikozitoa?
 
Tungekuwa na Tume ya kweli ya maadili ya viongozi tusingekuwa na sababu ya kujiuliza maswali yote haya. Kwa kuwa haipo kimantiki bali kinadharia basi tuache tu akina Maige na wateule wengine wakiwemo GGM wapige kazi kwani utajiri wa tanzania unaisha leo?

Na hata kama unaisha nani anajali? Kwani nchi hii bado ina watu ambao tunaweza tukawaita wazalendo? Demokrasia yenyewe tuliyonayo sehemu kubwa ni ya nyuma ya vioo kama hii ninayoitumia sasa! Ukitoka kusemea front utakuwa Kibanda.

Katika hali kama hii ndipo tungetegemea kwamba kama tungekuwa na taasisi zinazofanya kazi yenye upendo na nchi hii ingewekwa wazi background ya Maige ki uchumi na hapo ndipo tungeweza kujua na pengine kujiuliza tajiri kama huyu amefuata nini katika siasa hapo ndipo tungepata jibu.
 
Hivi iterns wa mnh wamelipwa shs ngapi? Huyu atoe maelezo kafanya biashara gani na tra kalipa kiasi gani.
Bila maelezo jk amfukuze kazi na afikishwe mahakamani, bila hivyo tuhesabu jk ni mshiriki wa dili
 
:A S embarassed:
KAHAMA, 05th, Jan 2012

MBUNGE wa jimbo la msalala wilayani kahama, mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige ametoa shilingi milioni 500, zilizozutumika katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii amesema fedha hizo zimetumika kuboresha elimu katika shule za sekondari za kata, barabara na ujenzi wa zahanati za vijiji.
Akizungumza katika kata ya Busangi, Waziri Maige amesema fedha hizo zimetumika kujenga Mabweni kwenye shule ya sekondari ya kata ya Isaka, Lunguya na Segese na madawati300 yaliyogawiwa kwenye shule tisa za sekondari katika jimbo la msalala.
Amesema katika fedha hizo, pia zimesaidia ununuzi wa mifuko 1200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za vijiji pamoja na ufungaji umeme wa Sora kwenye shule ya sekondari ya kata ya Ntobo na Ngaya pamoja na utafiti wa majiya visima virefu kwenye vijiji 32.
Kutokana na idadi ya ufaulu kuongezeka wilayani kahama, Waziri Maige amewataka wananachi kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa madarasa mapya ya shule za sekondari.

Maswali ya Kujiuliza

1. Kapata wapi fedha hizo Milioni 500TZS ?
2. Je, hayo siyo majukumu ya serikali ?
3. Vipi sehemu ambazo hazina watu matajiri kama Maige ?
4. Je, hili haliwezi kujenga hali ya serikali kuachia wabunge majukumu yake ?
5. Je, hili haliwezi kupelekea wabunge wengine wenye nafasi kushindana kuiba ili nao wapeleke majimboni kwao?

NB: Tukumbuke moja ya kazi za Mbunge ni kuongoza shughuli za maendeleo kutokana na fedha zinazotolewa na Serikali, na sio kugharamia shughuli za maendeleo.

...

Huyu ni mtanzania anauliza hili swali? Hujui nchi yako ilivyo
 
Back
Top Bottom