Prodigal Son
JF-Expert Member
- Dec 9, 2009
- 1,080
- 744
Watu wengi hapa JF wamemsifu sana Magufuli kwa kupata Phd hapo UDSM.
Kwa hiyo Mhe Nchimbi akipata Phd toka Mzumbe say,tushishangae sana.Naona kuna hypocricy hapa ,ni sawa kigogo kupata Phd Udsm lakini kuna watu watachallenge kigogo kupata Phd toka Mzumbe.
Thread yangu ni obectivity ya Phd ya Magufuli.labda mnaomjua zaidi huyu Mhe mtudokezee :
1.any standard Phd toka top class university ni 3 yrs for full time,na 5-6 yr for
for part time.Tunasikia Magufuli alichukua 3 yrs kumaliza tunaassume,alikuwa full time.Wote tunajua kipindi hiki alikuwa waziri !full time maana yake mwaka wa kwanza darasani,miaka 2 ni research na kupresent papers mbali mbali,au kuwa Tutorial assistant.
2.tunasikia supervise wake aliuwa classmate wake.je hapa kuna uhalali?
kwa sababu ni waizri mnategemea nani angesema ana walakini na research yake?
Hii trend imeanza kwa mawaziri kufanya Phd vyuoni!Kama Nchimbi na wenzake
wakipata Phd za Mzumbe watu wa UDSM msilalamike,maana trend imeanzishwa
na akina Magufuli.Miaka yote alikuwa wapi,mpaka awe waziri ndio awe na Phd?
Au ni kuwa sambamba na akina nagu,makogoro,matayo,dialo etc
ukumbuke uvumbuzi wake ni sifa hata kwa UDSM, ........, kumbuka finding ya dr magufuli tayari imeshaongeza value ya Korosho, mkulima ataweza uza korosho pamoja na maganda yake, kitu ambacho kilikuwa hakijulikani kabisa, sasa ndo unalinganisha na hizo za kina nchimbi na nagu ambazo hata title zao hazijulikani na hazina impact yeyote katika jamii???TUBADILIKE WABONGO NA TUACHE WIVU
Hii trend imeanza kwa mawaziri kufanya Phd vyuoni!Kama Nchimbi na wenzake
wakipata Phd za Mzumbe watu wa UDSM msilalamike,maana trend imeanzishwa
na akina Magufuli.Miaka yote alikuwa wapi,mpaka awe waziri ndio awe na Phd?
Au ni kuwa sambamba na akina nagu,makogoro,matayo,dialo etc
Umeme ukikosekana kwenye Train ya kati, lazima TANESCO ilaumiwe.... tetetetee 🙂
Sawa, hongera Dr. Kwani tofauti ya Docta na Prof ni ipi? Tuwape tu wote u-Prof na kijulikane kimoja. Prof. Kikwete, Magufuli, Mwakyembe, Makinda, Makongoro, Malecela, Makamba, Nchimbi, nk na wale wote wasiofundisha sasa kama Mwandosya, Sarungi,........................
Mkuu,
Unaweza ukatupasha habari zaidi juu ya uvumbuzi wa jamaa? Mbona hii sijaiona?
Mwaga hapa habari zake ili Ngosha asifiwe kwa kazi yake......
zitto Kabwe anafanya Phd wapi?
Hivi kama mtu hufundishi, kwa nini unajiita Dr?
Hivi ataanza kuandika vitabu na takataka nyingine ili kui-keep hiyo Dr au inabaki jina tu?
Hizi Tittle sasa zimekuwa za kwenda kuchumia uyoga msituni (bunsolele)...
SIKONGE kama kuna sehemu nimegusia huo uvumbuzi wake, na hata ukienda pale UDSM Library ukiomba chapisho lake PHD thesis ya dr Magufuli ipo
Alichokivumbua ni namna gani Maganda ya Korosho yanaweza tumika kuondoa tatizo la KUTU. Ukimbuke Kutu na tatizo kubwa saana kwa nchi za ulimwengu wa kwanza hasa marekani,na kikubwa ni kwamba hayo maganda yakianza kutumika tayari mkulima wa kurosho atakuwa anauza korosho pamoja na maganda yake, so atapata faida mara mbili, Kumbuka yeye aliweza kuprove kabisa kwamba kisayansi kwamba maganda yakorosho yanaweza kutumika kuondoa hilo tatizo
ni swala la kujivunia na kumpongeza na sana saana UDSM hususani idara ya kemia wanatakiwa wapongezwe kwa kuweza kumwongoza vyema akaweza maliza utafiti wake ontime
Msomi mmoja maarufu alisema hivi, kama mvua inanyesha na haionyeshi kama imenyesha basi hakuna maana ya mvua hiyo kwepo.
Mhe. Magufuli siyo tu kwamba anajua anachokifanya bali kila anapopita anaacha "ATHALI HASI" Mfano:
1. Alipokuwa Waziri wa Ujenzi - Kajenga Nyumba ngapi ambazo Mawaziri wengine wala hawakuthubutu hata kuzifanyia Ukarabati zile zile zilizopo. BaraX2 ngapi amezisimamia na siyo hilo tu bali hata kujua urefu wake na maendeleo yake ya kazi yanavyoendelea.
2. Alipokuwa Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi, Tazama NHC ilivyobadilika kiutendaji hata Ofisi zao zilianza kubadilika.
3. Kapelekwa Mifugo na Uvuvi- Vile vyuo vyote vya Mifugo amevifufua, zile Ranchi zote za Taifa amezifufua.
Mimi sijuwi wengine wanashindwa Nini.
Waziri Magufuli namfahanisha na Mhe. Celina Kombani - Waziri wa Serikali za Mitaa kuna mengi ameyafanya katika Serikali za Mitaa tangu alipokuwa Mhe. Naibu Waziri na hadi sasa kuwa Waziri kamili. hao ndiyo watendaji tunaowataka.