Ukuliza hivyo na mimi nukuulize ulikuwa wapi siku zote kwa kukwepa sheria. Kulingana na Sheria ya Ardhi kuna sehemu ili uweze kutumia ardhi lazima umilikishwe kisheria-"any urban land must be granted"
Nadhani ingekuwa vizuri kama ungenieleza upumbavu wa serikali ya awamu ya nne unatoka wapi wakati inafanya kazi zake kisheria.Huna umakini kabisa.
Hebu rudi ukurasa wa kwanza bandiko namba 4 usome nilichoandika.
Kama huwezi kurudi hilo hapo nimekuwekea.
Hivyo futa kauli yako. Nimeuliza hilo swali tokea mwanzo kabisa.
Nadhani ingekuwa vizuri kama ungenieleza upumbavu wa serikali ya awamu ya nne unatoka wapi wakati inafanya kazi zake kisheria.
Kwa hiyo ulitaka waachwe tu waendelee kuvunja sheria?
Sielewi mantiki ya hoja yako hasa ikichukuliwa huu ni utawala wa awamu nyingine ambao moja ya Ilani yake ilikuwa ni kuhakikisha inasimamia kikamilifu sheria za nchi.
Ila utu na busara inahitajika. Asilimia 80 bongo wamejenga kiholela name miaka yote hiyo serekali
like.
Mngeichagua chadema msingekumbwa na hayo mambo
Mkuu pamoja na kwamba uko upande huo wa hovyo hovyo wa" kuzungusha mikono" lakini huu mfano wako ni kiboko-ulitulia sana acha nikupe tano.
Usikimbie hoja ya msingi kwa kutafuta sehemu ya kujisetiri ili ujenge hoja ya nguvu.Nimesema wewe huna umakini na unaendelea kudhihirisha nilichokisema.
Hii ni serikali ya awamu ya nne au tano?
Wamesahau kwamba sheria inakata kote kote kwa makontena na kwa wavamizi wa ardhi. Nchi haina mae eo ya wazi utadhani hatuna maafisa mipango miji. Wanapima maeneo na kuacha ya wazi lakini waroho wanayavamia na kuwanyima watoto wetu sehemu za kucheza.Wananishangaza sana wanaoilaumu serikali ya Rais Magufuli kwa kutenda kazi yake ambayo ni pamoja na kusimamia sheria za nchi.
Kwa hiyo wanataka kutuambia kama kuna watu walitenda makosa na hawakushughurikiwa, wasishughurikiwe. Kwa maana nyingine, wanatuambia wale jamaa wa TPA & TRA na pia wale ambao walikwepa ushuru wa makontena inafaa waachwe kwa kigezo kuwa, serikali ilikuwa wapi wakati wanatenda hayo makosa mpaka makontena zaidi ya 2000 yakapita bila kulipiwa ushuru. Ni upumbavu kuanza kuwashughurikia sasa!
Kuna fikra zingine za ajabu kweli.
I know si kwamba unatetea hao jamaa coz' ulichosema wote sisi huwa tunasema ila tu nilitaka kukumbushia upande wa pili wa wananchi tulivyo. Yaani sisi si watu wa kutii sheria za makaratasi na maagizo... ni hadi tushurutishwe!Kwanza, mimi sitetei kabisa watu wa aina hiyo.
Pili, nalia na serikali kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
Serikali ingekuwa makini huyu mtu asingenyanyua hata huo msingi wa huo mjengo wake.
Kwa hiyo, hapo utaona kabisa kuwa serikali nayo ni chanzo cha baadhi ya haya matatizo.
Ujue Unaposema Serikali Inakurupuka Nashindwa Kukuelewa,kwa Sababu Hili Jambo La Kuhama Watu Wa Mabondeni Halikuanza Leo Wala Jana..
Jamani Hii Si Serikali Ya Kikwete Ya Kubebembelezana Na Kuchekeana,tulihitaji Mtu Wa Kutenda Sio Wa Kutoa Maagizo Yanayoishia Palepale.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi amesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku14 katika maeneo ya mabondeni na yaliyovamiwa na kujengwa kinyume cha sheria ili kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi imebainisha kuwa zoezi la bomoa bomoa limesimamishwa kwa muda kuanzia tarehe 22/12/2015 hadi 05/01/2016.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa eneo la mto msimbazi ni eneo hatarishi na ujenzi katika eneo hilo ni kinyume na sheria ya mipango miji na 8 ya mwaka 2007 na sheria ya mazingita na.4 ya mwaka 2004.
Maeneo mengine ambayo serikali imepiga marufuku ni maeneo ya wazi, kingo za mito, fukwe za bahari, maeneo ya hifadhi za barabara na maeneo hatarishi.
Aidha, katika Jiji la Dar es Salaam maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa ambayo ni kama ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111, Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.
VIDEO:
Wapumbavu kabisa.
Wakati watu wanajenga kwenye hayo maeneo serikali ilikuwa wapi?
Unachomwa kisu unalia,aliyekuchoma anakichomoa halafu unamsifu ana huruma na busara amechomoa,kweli kuiondoa ccm ni kazi
kwani magu si anatekeleza ilani ya chadema,au ndio unaanza kumkana?
hiyo inaonyesha kwamba,serikali ilikurupuka, kwa kifupi serikali hii inaweza kuitwa ya kukurupuka
The 'Occupier Liability Act' 1968
2.1 The rules enacted by this Act shall have effects, in place of the rules of common law, to regulate the duty which an occupier of the premises owes to his visitors in respect to dangers due to the state of the premises or to things done or omitted to be done on them
2.2 The rules so enacted shall regulate the nature of the duty imposed by law in consequence of a person's occupational or control of premises and of any invitation or permission he gives (or is to be treated as giving) to another to enter or use the premise, but they shall not alter the rules of common law as to the person whom a duty is imposed or to whom it is owed: and accordingly for the purpose of the rules so enacted to the persons who would at common law be treated as an occupier and has his invitees or licencees.
Usikimbie hoja ya msingi kwa kutafuta sehemu ya kujisetiri ili ujenge hoja ya nguvu.
Hoja yako ya msingi umedai Serikali ya Rais Magufuli ni wapumbavu kwa sababu wanabomoa nyumba ambazo hazikubomolewa mapema au haikuwazuia kujenga mapema. Kwa maana nyingine, serikali iwaache tu waendelee kuvunja sheria.
Hoja yako ya msingi ni sawa na kusema, kwa nini serikali inawafungulia mashitaka wale waliopitisha makontena zaidi ya 2000 bandarini kwa sababu wamefanya hivyo kwa muda mrefu wakati serikali haikuweza kuwachukulia hatua mapema au kuzuia makontena kupita bila kulipa ushuru.