Waziri Lukuvi asitisha zoezi la bomoa bomoa

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini, Mhe. William Lukuvi amesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku14 katika maeneo ya mabondeni na yaliyovamiwa na kujengwa kinyume cha sheria ili kutoa nafasi kwa watu waliojenga katika maeneo hayo kuondoa wenyewe mali zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi imebainisha kuwa zoezi la bomoa bomoa limesimamishwa kwa muda kuanzia tarehe 22/12/2015 hadi 05/01/2016.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa eneo la mto msimbazi ni eneo hatarishi na ujenzi katika eneo hilo ni kinyume na sheria ya mipango miji na 8 ya mwaka 2007 na sheria ya mazingita na.4 ya mwaka 2004.

Maeneo mengine ambayo serikali imepiga marufuku ni maeneo ya wazi, kingo za mito, fukwe za bahari, maeneo ya hifadhi za barabara na maeneo hatarishi.

Aidha, katika Jiji la Dar es Salaam maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa ambayo ni kama ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111, Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.

VIDEO:
 
Last edited by a moderator:
Serikali imefanya vizuri kusikiliza kilio cha wananchi ili kuwapa grace period ya kuondoka kwa amani.

Kama serikali iliweza kuwapa grace period wezi wa kodi ya nchi katika bandari, kwa nini isifanye kwa wajenzi holela.

Huu ni uamuzi wa busara na hekima.
 
Umefika wakati wewe mwananchi, mjumbe,mtendaji,mwenyekiti wa mtaa,diwani,mbunge hadi mkuu wa wilaya ukiona mtu anajenga, chimba mchanga,fanya biashara, chafua mazingira inuka na umwambie aache, watu wa manispaa huwa wanjua sana kukagua vinali vya ujenzi, mabwqna afya kukagua guest na bar lakini kutambua kwamba huyu mwananchi anaendeleza eneo lisiloruhusiwa kisheria huwa wanakaa kimya sasa yatosha tusafishe mji wetu we need GREEN & SUSTAINABLE CITY
 
Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa
siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia
na kuishi katika bonde la Msimbazi Mkwajuni
kuondoka ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo
kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe
wanaondoka wenyewe.

Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na
maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema
waliojenga katika eneo hilo wapo hapo kinyume na
sheria kwani kwa sabu ni mahali hatarishi.

Akaongeza kuwa kwanzi mwakani wizara yake itagawa
kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango
miji ili waweze kuvisimamia kwa ukaribu ili kuepusha
uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.

ITV ilikwenda katika eneo la Mkwajuni na kukuta
makundi ya watu wakijitahidi kuhamaisha vitu vyao ili
kuepusha uwezekano wa kupata hasara pindi tinga
tinga litakapokuja huku wengine wakisema kuwa
kuisha kwa muda ili kutoa nafasi watu kuhama ni
jambo jema.

Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za
bomoabomoa na kusema kuwa imekuwa na hatua
ngumu lakini muhimu kwani eneo hilo limekuwa
likisababisha vifo vya watu kila mafuriko yanapotokea
hivyo watu kuondolewa hapo wamenusurishwa kwa
mengi.

Katika hatua nyingine waziri wa nchi ofisi ya waziri
mkuu Mh Jenister Mhagama ameziagiza kamati za
maafa katika ngazi za mikoa, wilaya na vijiji
kuorodhesha na kuwapa barua za kuwataka watu wote
wanaoishi maeneo hatarishi kuhama mara moja katika
maeneo hayo na utekelezaji wa agizo hilo uwasilishwe
ofisi ya waziri mkuu haraka iwezekanavyo.

Chanzo: ITV
 
Ila utu na busara inahitajika. Asilimia 80 bongo wamejenga kiholela name miaka yote hiyo serekali ya chama cha makenge ilikuwa wapi? Kuweni na huruma na wananch wenzenubana hata kama IQ zao ni ndogo wanahitaj msaada. Nchi yote hii kama kujengwa upya inabidi gharika kama ya nuhu ije
 
Waseme tu wamepisha siku kuu, kwa sababu wanaenda likizo. Hiyo tarehe 5 si ndiyo ofisi zote ninaendelea na kazi.
 
Unachomwa kisu unalia,aliyekuchoma anakichomoa halafu unamsifu ana huruma na busara amechomoa,kweli kuiondoa ccm ni kazi
 
Ila utu na busara inahitajika. Asilimia 80 bongo wamejenga kiholela name miaka yote hiyo serekali ya chama cha makenge ilikuwa wapi? Kuweni na huruma na wananch wenzenubana hata kama IQ zao ni ndogo wanahitaj msaada. Nchi yote hii kama kujengwa upya inabidi gharika kama ya nuhu ije

Hivi kwa nini wabeba maboksi wengi ni mazuzu sana? Ona sasa upuuzi ulioqeka hapa! Hovyo kabisa.
 
Wapumbavu kabisa.

Wakati watu wanajenga kwenye hayo maeneo serikali ilikuwa wapi?
Ningekuelewa kama ungesema serikali ni wapumbavu kwa sababu wakati wanajenga hakukuwepo na sheria inayowazuia kujenga katika maeneo hayo.

Wamejenga nyumba katika maeneno ambayo sheria haiwaruhusu na kwa maana hiyo, hakuna time limit ya vyombo vya kusimamia sheria kufanya kazi yake.

Kutokumatwa hakuwezi kufuta kosa ulilolifanya.

Upumbavu ni kuilaumu serikali ya Rais Magufuli ambayo inasimamia sheria za nchi.
 
It is too late, damage has been done,

hivi 75% ya wananchi waliojenga viwanja ambavyo havijapimwa nayo ni ujenzi holela?

c'mon, where was the government kupima,kutoa hati,kutekeleza sera ya makazi bora

kuna kata,tarafa hazijapimwa hata mita 1
 
Back
Top Bottom