Waziri Lukuvi asitisha zoezi la bomoa bomoa

Waziri Lukuvi asitisha zoezi la bomoa bomoa

Serikali kila siku inakurupuka km imetoka usingizini, hiv hamtulizagi vichwa vyenu mnapotaka kufanya jambo mkaliangalia kwa mapana, faida na hasara zake??? Na wakati gani lifanyike? Ni aibu kwa watu wanojiita wasomi kuwa na maamuz ya hivyo hovyo,
 
ninaishangaa hii serikali yaani upimaji wa viwanja uko slow sana,na wakipima wanajipimia mwenyewe na ndugu zao

Hii nguvu inayotumika ktk bomoa bomoa ingetumika ktk kutekeleza Mkakati wa Upimaji Viwanja&Mashamba

mpango huu usingechukua zaidi ya miaka 2 kupima nchi nzima
 
Uamuzi wa kubomoa maeneo yote kama kingo za mito, fukwe za bahari na karibu na barabara, na maeneo hatarishi kama mabondeni, halmashauri zote zinatakiwa kuwa makini na kuzuia pindi mtu au watu wanapojenga kwani wapo mitaani kila siku na wanayaona na kazi yao kuhakikisha mpango mji unakaa unavyotakiwa.

Unakuta vibanda vimejengwa kila sehemu mbele au pembeni mwa maduka yote hayo serikali inalifumbia macho halafu inakuja siku ya kutanua barabara wanaanza kubomboa sasa gharama yote ya nini ingawa unaweza kuzuia kabla.

Kuhusu hili la bomoa bomoa mabondeni hilo linafanyika sasa ni uamuzi wa serikali lakini ni lazima iingie gharama ya kutengeneza ili hayo maji yapite salama yanakotoka na kandokando wapande miti mingi ili pawe mahali pa kupumzika watu
 
Sheria ya mwaka 2007? Waliojenga kabla ysa hiyo sheria wanakosa gani, binafsi ni mkaz maaeneo hayo lkn kila nikichukua 4m za viwanja naambulia kulipa nonrefundable fee ile elf
 
Duh kumbe watu wengi wataumia hivi, yaan kwa DSM maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa ambayo ni kama ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111, Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.
 
hiyo inaonyesha kwamba,serikali ilikurupuka, kwa kifupi serikali hii inaweza kuitwa ya kukurupuka

Ujue Unaposema Serikali Inakurupuka Nashindwa Kukuelewa,kwa Sababu Hili Jambo La Kuhama Watu Wa Mabondeni Halikuanza Leo Wala Jana..

Jamani Hii Si Serikali Ya Kikwete Ya Kubebembelezana Na Kuchekeana,tulihitaji Mtu Wa Kutenda Sio Wa Kutoa Maagizo Yanayoishia Palepale.
 
Lukuvi ha stahiki ku nina alonena
Ilipaswa ajiuzuru tu.
 
Ningekuelewa kama ungesema serikali ni wapumbavu kwa sababu wakati wanajenga hakukuwepo na sheria inayowazuia kujenga katika maeneo hayo.

Wamejenga nyumba katika maeneno ambayo sheria haiwaruhusu na kwa maana hiyo, hakuna time limit ya vyombo vya kusimamia sheria kufanya kazi yake.

Kutokumatwa hakuwezi kufuta kosa ulilolifanya.

Kwa nini hawakuchukuliwa hatua wakati wanajenga?
 
Yaani ukianza kuiba wakato serkali ipo ndiyo inakuwa haki yako kuiba? What kind of reasoning is this? Siku za mwizi ni arubaini, maana yake ni kwamba wewe jidanganye uibe na uvunje sheria kwa siku 39 siku ya 40 lwako.

Wewe ni juha kabisa.

Hivi hilo hitimisho lako umelifikiaje?
 
Walikuwa wamelala, na walikuwa wakichanganya shughuli za kiserikali na siasa! Tatizo la ujenzi holela lina historia ndefu sana hapa Duniani na hatima yake ilikuwa kule Rio de Janerio mwaka 1992. Aidha pamoja na Tanzania kushiriki mkutano huo, bado halmashauri nyingi za miji na majiji wameshindwa kabisa kufuata yale yaliyopendekezwa...

Kwa kutoa siku 14, bado naona ni uonevu tu kwa wakaazi hayo! at least wangepewa siku sio chini ya 270!

Serikali makini ilipaswa kuhakikisha kuwa sehemu zote ambazo hazitakiwi kujengwa kiholela hazijengwi kiholela.

Lakini siyo kuachia watu kuvamia na kujenga kwenye hizo sehemu [hadi kuvuta umeme na maji] halafu baadaye eti ndo mnakuja kustuka kuwa kuna watu wamejenga kiholela.

Hivi siku zote hizo mlikuwa wapi? Mlikuwa hamjui kuwa watu wanajenga kwenye hizo sehemu?

Halafu leo hii ndo mnakuja na kuanza kuwavunjia watu miji yao ambayo nyinyi wenyewe [serikali] ndo mmechangia uwepo wake.

Huo ni upumbavu kabisa.
 
Kila siku mimi huwa nasema hivi vyuo vya Ardhi kila mwaka watu wanavaa kofia na majoho ya masuala ya ardhi ikiwemo mipango miji,matumizi bora ya ardhi nk,lkn hao watu hawaonekani wanachofanya hata jambo dogo la kugawa kata na akakabidhiwa afisa kuiangalia huku akiwa na Master plan ya eneo lote,akapewa Toyo ya kuzungukia maeneo yake yote kuangalia nani anaanza kuchimba japo msingi amjue ni nani na kama anajenga eneo husika,kila wiki apeleke taarifa ya maandishi kwa Mkuu wake akionyesha nani yuko wapi na anafanya nini ktk plot fulani,Yule mbunge mzungu Bryson aliipangaje Sinza ambayo inaonekana leo?tatizo la nchi yetu kila mtu akitoka chuo anataka aonekane mkubwa na mikwara tele hamna lolote,watu ambao kutokana na Taaluma zao wanapaswa kuwa site full time ndiyo hao wamejazana maofisini mbele ya computer wanacheza karata tu,mfano unakuta mhandisi wa umeme ktk Halmashauri au Manispaa hajui nini kinaendelea huko mtaani,nguzo ya umeme imegongwa au taa haiwaki anasubiri Kaburu alete fedha wkt ki vitendo mtaalamu kama huyo muda wa usiku ndiyo mzuri wa kuzikagua njia zake zote na kujua kasoro ziko wapi ktk barabara fulani ili asbh atume mafundi kuangalia tatizo,sometimes waweza kukuta tatizo ni balbu imeungua,jee hiyo nayo kuibadilisha hadi msaada utoke Nordic countries?Mungu atupe utashi wa kujitoa kuitumikia Jamii iliyotupa nyadhifa hizo,Mungu ibariki nchi yetu na mama Tanzania
 
tulimchagua ma padlock aturudishe kwenye upangaji au? kwa nionavyo mimi sio sahihi
 
Wapumbavu kabisa.

Wakati watu wanajenga kwenye hayo maeneo serikali ilikuwa wapi?
Ila sometime na sisi raia wenyewe ni watata kishenzi!! Kuna nyumba ambayo naifahamu ambayo iko barabarani kabisa na wakati inajengwa, kabla haijafika mbali Manispaa wakaja kuipiga X!! Jamaa nikadhani angebomoa lakini akafanya kama kuwasikilizia hivi na alipoona kimya, jamaa akaendelea wasiwasi hana na sasa ni bonge la hotel~~~!! Huyu nae cku akija kubomolewa tutahoji vilevile kwamba serikali ilikuwa wapi!!!

Usisahau, hii ni nchi ambayo hata chini ya umeme mkubwa utakuta wafanyabiashara kibao ingawaje takuta mabango kibao vilevile ya kukataza watu! I remember years back nilienda Kusini wakati huo barabara ilikuwa haijafunguka na hamna usafiri wa uhakika zaidi ya meli! Basi bhana, wakati wa kurudi nikapata meli lakini baada ya kung'oa nanga na tukiwa kina kirefu meli ikazima.... baada ya saa kadhaa kupita, jenereta nalo likazima kwahiyo tukawa kama tupo kwenye mtumbwi ndani ya giza totoro!

Tukaa hapo cku tatu hadi ilipofika meli nyingine na kutuvuta kurudi Lindi Mjini!! Abiria ikabidi turudishiwe nauli zetu!! Baada ya kama siku 5 hivi tukasikia ile meli imepona na inarudi Dar lakini haichukui abiria hata mmoja! Guess what... yote ambayo yalitukuta baharini tukasahau na bado tukalazimisha lakini jamaa wakakaza! Hapo vikaanza kutembea vimemo... mimi mwenyewe nilienda na kimemo toka kwa RPC!!!! Sasa hiyo jeuri ya kumwacha mtu mwenye memo ya RPC mkononi unaitoa wapi?! Nikapanda na mule ndani tukawa kama abiria 50 ambao tuliruhusiwa na vimemo vya wakubwa!!

Ilipofika jioni tukaondoka kurudi Dar lakini kama ilivyokuwa safari ya kwanza, tukiwa Dar mbali Lindi mbali; mzigo ukagoma kwa mara nyingine kwenda mbele wala nyuma!Tukaa hapo siku 3 tunawatia short ya kutulisha bure manake ilikuwa ni wajibu wao!!! Ile meli hiyo ilikuwa ndo safari yake ya mwisho kabisa kusafiri na hadi leo ime-RIP pale bandarini!!!!

Nimekupa hiyo simulizi kukumbusha Watanzania ni watu wa aina gani.... ndo vile tu CCM yenyewe imechokwa ndo maana tunaweza kusema kama ulivyosema lakini ukitaka Mtanzania umkataze mahali basi labda uweke kikosi cha jeshi hapo hapo kipige mzigo 24/7!!!
 
Wanajamvi kwa wenyeji wa Dar-es-salaam watakuwa wanaelewa sana kuwa bonde la msimbazi,Jangwani na Kinondoni kulipo bomolewa ni maeneo HATARISHI kwa kuwa wakati wa masika mvua zikinyesha na mto msimbazi ikikutana na Bamvua (wenyeji wa Pwani watanielewa kutumia neno hilo) kuna tokea mto kujaa.Hivyo eneo hili lilikuwa hakuna mwenyeji ambaye anaweza kujenga makazi zaidi ya kulima mpunga. Kilichotokea wajanja walipozidi kuingia jijini wakauziwa na walipokuwa wana onywa majibu walikuwa wanasema "MAJI YANAKIMBIA WATU" lakini tumekuwa tukishuhudia kila mara wakati wa masika mafuriko yanavyo waadhiri na kuomba msaada wa serikali na wapo watu wanapoteza maisha yao,wameambiwa wahame hawahami! wamepewa viwanja wameuza sasa waachwe au waondolewe kwa nguvu kama hawataki kuondoka kwa hiyari jibu ndiyo hapo Serikali ifanye maamuzi magumu sasa uamuzi umepita wamepewa siku 14 wahame mengine ni HISTORIA.
 
Ila sometime na sisi raia wenyewe ni watata kishenzi!! Kuna nyumba ambayo naifahamu ambayo iko barabarani kabisa na wakati inajengwa, kabla haijafika mbali Manispaa wakaja kuipiga X!! Jamaa nikadhani angebomoa lakini akafanya kama kuwasikilizia hivi na alipoona kimya, jamaa akaendelea wasiwasi hana na sasa ni bonge la hotel~~~!! Huyu nae cku akija kubomolewa tutahoji vilevile kwamba serikali ilikuwa wapi!!!

Kwanza, mimi sitetei kabisa watu wa aina hiyo.

Pili, nalia na serikali kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Serikali ingekuwa makini huyu mtu asingenyanyua hata huo msingi wa huo mjengo wake.

Kwa hiyo, hapo utaona kabisa kuwa serikali nayo ni chanzo cha baadhi ya haya matatizo.
 
Back
Top Bottom