MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
- Thread starter
- #61
Nadhani ungeuliza swali hili kwenye comment yako ya mwanzo badala ya kusema Serikali ya Magufuli ni wapumbavu kwa sababu inasimamia sheria.Kwa nini hawakuchukuliwa hatua wakati wanajenga?
Nina uhakika Rais Magufuli hataishia kuvunja nyumba bila kuwachukulia hatua hasa wale waliruhusu ujenzi sehemu za wazi zilizotengwa kisheria na fukwe za bahari.
Ni kweli kuna makosa yalifanyika wakati wa awamu za utawala kabla ya awamu ya Rais Magufuli lakini vile vile hata sisi wananchi lazima tujifunze kutii sheria bila shuruti na pia tujifunze kutumia wataalam katika masuala ambayo hatuna fani zake kwa sababu ignorance of law excuses no one.
Kwenye nchi za ''wenzetu'', Ma-consultant wanaheshimika sana kwa sababu wanasaidia kuepuka kadhia kama hizi za kuvunjiwa nyumba kwa sababu hukufahamu kama sehemu unayojenga hairuhusiwi au documents unazopata ni feki. Sisi tunawaona kama hawana faida na maana yoyote katika kufanikisha mipango yetu.
Kuilaumu serikali ya Rais Magufuli kwa sababu inasimamia sheria ni upumbavu!
Ninaipongeza serikali kwa kusikiliza kilio cha wananchi na kusitisha zoezi kwa muda ili wananchi wapate wasaa wa kuondoa vifaa vyao kwa amani na utulivu.