Hawa ndiyo viongzo tulio nao,wewe haushangai ukienda pale Club 84 dodoma utawakuta wakivizia watoto wa CBENaona si vyema kumshambulia mleta mada, badala yake tumuombe atupe data zaidi ili tumkome nyani vizuri. kwamfano katika mada yake kuna issue kuu mbili na mawili yatokanayo:
1) -Waandishi walikatiwa mshiko wa alfu 20 ili wasiandike maswali ya wapiga kura wake ya kwanini aliisajiri Deep Green? je aliwajibu majibu ya kutosheleza?
---Je waandishi kwa kupokea hiyo alfu 20 mkaacha kuandika habari nzito namna hii mnatutendea haki watanzania wenzenu?
2)-Jambo la pili ndo hilo la kutoa zawadi binafsi kwa ma miss, je ni jambo jema kwa waziri mwenye dhamana kufanya hivo? je anapo toa pesa hiyo kwa shughuli kama hiyo wakati wapiga kura wake kuna watoto wana shindwa kwenda shule kwa kukosa uniform ya alfu 5 ni sawa?
----Jambo la mwisho linatokana na baadhi ya wachangiaji wanao uliza kwamba alitoa sh ngapi na kama alikuwa kaisha onja mbili tatu kwani wanamjua tabia yake, wasi wasi wangu ni je, waziri mwenye dhamana hatakiwi kuwa na maadili fulani ya kulinda heshima yake na pengine kuwa katika mazingira na hali ambayo haihatarishi maslahi ya taifa?, mfano kama akionja anakuwa 'out of himself' hawezi kuliingiza Taifa mkenge kwakutoboa siri, ama kufanya maafikiano fulani ambayo hayana tija kwa Taifa?
Sijui inawezekana kuwa na viongozi wa namna hii ni maendeleo, na huenda alichokifanya kinastahili kuungwa mkono kwa mtazamo wa wengine. Lakini kamwe zawadi binafsi kutoka kwa Masha kama , shilingi 150,000 na Seti ya Tv, shilingi laki moja kwa mshindi wa Urembo wa Pili na Laki Moja kwa mshindi wa Tatu, na shilingi 50 kwa kila mmoja kati wengine tisa waliobakia, na hapo hapo kuna zawadi tayari zilikuwa zimetolewa na muaandaaji, lakini pia kuna wahitaji wengi wenye shida katika jimbo lake, hili haliingii akilini.
Lakini Pia tuangalia aina ya viongozi ambao tunawatarajia linapokuja suala la vitendo, mienendo na yale ambayo jamii inatarajia iwafanyie.
Jamaa huyu ukimuona anaongea utadhani zimejaa, lakini nachelea kusema hapo alipo hazitoshi.
Natumia kigezo kimoja cha mauaji ya Albino. Inatosha maana hata kama ni makosa, tangu March mambo haya yalipoanza, angerekebisha kitambo.
Ktk mahojiano na BBC alionyesha hana lolote. Anachosema ni kueleimisha umma. Wakati umma unaelimishwa nini kifanyike maana haya ni mauaji na elimu yaweza kuwa ya miaka.
Naona anaendesha wizara kama kikosi cha wanasheria na kesi zao mahakamani.
Siombei mabaya mtu yeyote, lakini akiwa bado ni Waziri naomba kifo cha waziri mmoja kwa imani yoyote ile! Hapo nadhani tutaona nchi nzima ikitanda Polisi.
Au ndo matokeo ya uwaziri wa bakshishi?
Kamanda mkuu kwanza hongera kwa kufikisha post 1.
Nadhani hapa humtendei haki Mh Masha, kweli kuna matatizo kufuatia vifo vya maalbino na hatua kadhaa zishachukuliwa na Wizara, jambo muhimu hapa ni kuwa suala hili ni matokeo ya imani za kishirikina ktk jamii na namna ya ku deal nalo kunahitaji ushirikiano wa pamoja baina ya serikali na sisi sote. Kuanza kunyoosha kidole kwa mtu mmoja kama ndio chanzo/solution ya jambo complex kama hili nadhani humtendei haki Mh Masha
Nionavyo, siyo ajabu Waziri kutwishwa mzigo.
Kwa nini kuzima maandamano ya wanafunzi isiwe complex.
Kwa nini kupambana na CUF Pemba isiwe complex. Au majambazi. Mimi kama MchunguZI, nawezaje kuisaidia serikali ktk hili?
Kwa utendaji wa serikali zetu, Wizara inaweza kwenda vizuri kama una waziri mzuri na inaweza kuwa mbovu kama una waziri mbovu. Tumeyaona ELimu!
Tatizo langu kubwa siyo Masha ila tu naona sasa image ya nchi iko pabaya kabisa. Vyombo vikuu vya Habari Dniani vimelidaka hili. BBC wameonyesha ya kwao. Aljazeera wameahidi kuieleza Tz sunday.
Kwa takwimu, inaonyesha sisi TZ na Zimbabwe tunaongoza kwa idadi ya Albino Africa. Kweli hatusituki kuwalinda kwa njia za dharula.
Mchunguzi,
Hivi unathubutu kufafanisha mauaji ya albino na maandamano ya wanafunzi? lets be serious for a minute.... sasa ikiwa jambo ambalo linaiweka "image" ya nchi pabaya na linashadidiwa na vyombo vya nje vikiwemo BBc na Aljazeera bado una thubutu kulifafanisha na maandamano ya wanafunzi!
Narudia hili jambo limechukua sura ya kitaiafa na linahitaji juhudi za kila mmoja wetu, mnakotupeleka ni sawa na kusema kwa kuwa watu wanakufa kwa Malaria au ukimwi basi waziri wa afya hana uwezo!
Masatu,
Hebu niseme hivi;
If everybody is responsible then nobody is irresponsible and vice versa.
Usifanye kazi ikawa ni ya kila mtu. ikisha kuwa hivyo basi amini, hakuna wa kuifanya, na hakuna mwenye makosa. Waache wanasiasa waseme hivyo wanaposhindwa lakini mtendaji anayejua wajibu wake hawezi kusema hivyo.
Mtoa mada anaweza kuwa amekosea au kaonyesha hasira yake lakini hata mimi nasema Juhudi ya serikali ktk jambo hili hailinganmi na ukubwa wa tatizo. na Serikali kwa upande huo ni Wizara husika na ni Waziri muhusika, Lawrence Masha.
Tena ningependa tusiseme ni mauaji ya Albino. Tuseme ni mauaji ya raia wenzetu. Huko mbeya hatukusema mauaji wa Wanyakyusa au Wasafa au Wandali. Mtu akichunwa ngozi, akikatwa mkono, nk. ni raia basi!
Si vema ku-judge utendaji wa mtu kwa kuangalia suala moja tu. Kama mkiruhusu kufanya hivyo, basi mimi nitawatolea mfano wa mahabusu ambao siku hizi hupelekwa mahakamani katika mabasi yenye viyoyozi na muziki mkubwa, yaani hakuna kabisa makarandinga
Mtu mmoja tu katika baraza lako la mawaziri anayetupa matumaini ni Magufuli tu. Anadiriki kuwanyooshea kidole hata mawaziri wenzake. Kinakuzuia nini kumpa uwaziri mkuu huyo mtu? Tanzania inahitaji PM mwenye guts kama hizi.
PM wako ni playboy hamna kitu. Sawa na Sumaye tu. Mng'oe kabla hajakutia aibu. Mambo yake yoote yanajulikana.
SOURCE: Alasiri