Ndugu wana-forum hivi viongozi wetu watajua kuwajibika kwa wananchi lini?
Au ndiyo yale yale ya kudanganyana majukwaani? Walalahoi na wenye uchungu na ile nchi nafikiri mtaniunga mkono kwa hili.
Kinachojionyesha sasa ni kwamba tuna kopi za akina Sumaye, Kigoda kwenye hili baraza la mawaziri la JK. Tofauti ni kuwa hatuna kopi ya BM. Maana JK anajitahidi kuongea lugha ya kuonyesha kuwa anawajali wananchi wakati akiwakumbatia kina Karamagi, Rita Mlaki, Masha na wengine wa aina hiyo.
JK unatupeleka wapi? Mbona unawageuka wavuja jasho wa nchi hii ya TZ?
Sasa hivi kuna watu wanawacheka Nigeria (Mafuta), Wanamcheka Koni wa Uganda. Lakini hakika nakwambia JK kwa mwendo huo wa Mawaziri wako na Serikali iliyopita ya BM tutayapata ya Nigeria na Uganda usipokuwa makini.
Mbona umewatengeneza kina Kigoda na Sumaye tena? Ogopa sana wananchi waliokata tamaa. Maana wao hungojea mwanzilishi.
Mtu mmoja tu katika baraza lako la mawaziri anayetupa matumaini ni Magufuli tu. Anadiriki kuwanyooshea kidole hata mawaziri wenzake. Kinakuzuia nini kumpa uwaziri mkuu huyo mtu? Tanzania inahitaji PM mwenye guts kama hizi.
PM wako ni playboy hamna kitu. Sawa na Sumaye tu. Mng'oe kabla hajakutia aibu. Mambo yake yoote yanajulikana.
Sasa huyu Rita Mlaki unamkawizia nini kumwambia atangaze kujiuzulu? Soma hapo chini.
========
Magufuli Kiboko!
2006-08-11 17:06:29
Na Usu-Emma Sindila, Dodoma
Katika hali inayodhihirisha kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kiboko, amemchenjia hata Naibu Waziri wake Mama Rita Mlaki.
Waziri Magufuli ambaye huwa hamwonei mtu haya awapo kazini, amemtoa michozi Mama Mlaki kwa kumpokonya kiwanja chake.
Kiwanja hicho ni miongoni mwa vile ambavyo havijaendelezwa na wamiliki wake.
Magufuli amethibitisha hilo wakati akijibu hoja za wabunge walizozitoa wakati wakichangia hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2006/07.
Katika watu walionyanganywa viwanja hata Naibu wangu naye yumo,akasema bila hofu.
Akaongeza kuwa watu walionyanganywa viwanja hivyo walipewa notisi ya siku tisini kujieleza ni kwa nini hawaviendelezi katika kipindi chote hicho.
Lakini cha ajabu ni kwamba watu hao wakiulizwa viwanja hivyo ni vya kina nani wanakana na hata Naibu wangu naye alipoulizwa ni cha nani akasema kiwanja hicho sio cha kwake, Mhe. Magufuli akawaambia wabunge.
Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli amewapa mwezi mmoja maafisa ardhi wanaohusika na zengwe la nyumba za NHC Tabora kuhakikisha wanazikabidhi hati hizo kwa wenyewe mara moja.
Kuhusu migogoro iliyojaa Wizara ya Ardhi, Mhe. Magufuli amesem ma mingine imedumu kwa miaka zaidi ya 40.
“Mingine imeanza hata kabla sijazaliwa”, akasema.
Amesema katika hali ya kushangaza matapeli yanadiriki kuuzia watu viwanja huko Mbezi hata kwa shilingi milioni 200.
Tunawaomba wabunge watupe nguvu kuchambua migogoro...mingi imejaa matapeli watupu, akasema.
Aidha amesema maofisa ardhi wengine ni matatizo na kero na amewataka wananchi na wabunge kupeleka majina yao ili watimiliwe kazi mara moja.
Mimi siogopi kufukuza kazi watu wazembe, akatamba.
SOURCE: Alasiri