Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 39,525
- 25,519
Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Kombo ameeleza kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi, imeleta "mtikisiko chanya" wenye athari kubwa ulimwenguni kote, na si kwa Tanzania pekee.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri huyo alikiri na kuthibitisha uzito wa ziara hiyo kiuchumi na kidiplomasia, akibainisha kuwa imefanyika katika wakati muafaka ambapo Urusi inapanua wigo wake wa kiuchumi na kuelekeza nguvu zake katika Bara la Afrika.
"Naomba ndugu zangu waandishi wa habari nikiri mbele yenu na nithibitishe mbele yenu, ziara ambayo imeleta mtikisiko wa kidunia, si wa Tanzania tu... ni ziara hii ya Urusi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan," alisema Waziri huyo, akifafanua kuwa mtikisiko aliouzungumzia ni chanya (positive) na wala si hasi (negative).