Waziri Jafo: Manispaa ya Ilala ndio kinara wa ukusanyaji mapato, ya pili Kinondoni, ya tatu Temeke, ya nne ni Dodoma.

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,542
93,153
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo anatoa taarifa kuhusu matokeo ya Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri zilizofanya vizuri na zilizofanya vibaya.

amesema Manispaa ya Ilala ndio kinara wa ukusanyaji mapato, ya pili Kinondoni, ya tatu Temeke, ya nne ni Dodoma.

Mimi sina la kuongeza Waziri Jafo yupo live TBC anamwaga takwimu sahihi.
 
Inamaana Dodoma imeipita Mwanza, Mbeya, Arusha? sijaelewa?

Ni vyema pia akatuambia vyanzo vya mapato vinavyoweza kuifanya Dom ikashika namba nne kwa ghafla hivyo.
Kuna biashara gani dodoma ukilinganisha na Geita tu pale au Kahama?, Kuna project gani kubwa dodoma iliyoleta Mzunguko wa watu?.. Unataka kutuambia hawa wafanyakazi wa Serikali, Mashirika ya umma kuhamia dodoma ndio wameongeza mzunguko dodoma?.. kwa nini mapato yasishuke Dar kwa maana ya Kinondoni, Ilala na Temeke ambako ndio wafanyakazi wengi wametoka kuhamia dodoma?
 
U have point Mkuu
 
Ilala imeongoza kwa mapato ghafi ila Dodoma imeongoza kupitisha lengo kwa asilimia kubwa, hivyo unavyosema sehemu fulani imeongoza ni vyema ukasema imeongoza kwa kipengele gani mahsusi.
Basi tuwekee katika lugha rahisi(fungua codes) ili tuelewe,inaonyesha kuna kitu unataka kufafanua,ila umetumia lugha ya Kiuchumi zaidi.
 
Juzijuzi ameaongea eti manispaa ya dodoma inaizidi dar kwa makusanyo, sasa jafo leo kupitia tbc amemprove wrong. Alise.a kuna mtu alikuwa anapiga mil 7 kwa dakika mpaka leo hakuna kinachoendelea. Alisema ataajiri watu wengi kwenye bomba la mafuta kule tanga watu wakapeleka cv zap pale posta mpaka leo kimya. Alisema kupitia makonda eti ana ajira temporary za kuhesabu magari dar mpaka leo hamna kitu watu waliishia kuaply tu na mpaka leo kuna mzigo wa aplication pale tanroads geleji hata wahudumu pale ukiwauliza wanakwambia ilikuwa usanii hakuna kitu kama hicho. Kila kitu ni uongo uongo uongo
 
Back
Top Bottom